Jinsi ya kuchagua mtoto wa kike, wa kiume au mapacha soma hapa

Sasa kama chromosomes zote X na Y ni za kwangu kwanini nijihangaishe kuchagua jinsia ya mtoto?

Mimi nitagonga muda wowote atakayekuja atakuwa wa kwangu maana ni mtoto wangu.
 
MTOTO WA KIUME AU WA KIKE ANATOKEAJE?
Katika urutubishaji yai la mwanamke linabeba chromosome X yani XX
Na mbegu ya mwanaume inabeba chromosome XY
Chromosome X kutoka kwa mwanamke ikikutana na Y kutoka kwa mwanaume mtoto wa kiume hupatikana
Chromosome X kutoka kwa mwanamke ikikutana na X kutoka kwa mwanaume mtoto wa kike hupatikana
FAHAMU SIFA ZA CHROMOSOMES X na Y za mwanaume
Ili uweze kufanikiwa kuchagua mtoto wa kiume au wa kike lazima ujue sifa za chromosomes hizi zinazoamua jinsia ya mtoto
SIFA ZA CHROMOSOMES Y
1.Zina spidi kubwa sana kwahiyo kama yai lipo tayari zenyewe zitawahi kwenda kurutubisha
2.Zina maisha mafupi sana kulinganisha na X
SIFA ZA CHROMOSOMES X
1.Zina spidi ndogo sana
2.Zina maisha marefu kulinganisha na Y
Baada ya kujua sifa za chromosome ambazo ndo zinatusaidia kuamua jinsia twende moja kwa moja kwenye jinsi ya kupata mtoto wa jinsia unayotaka
MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA KUAMUA JINSIA
1.Lazima mwanamke ajue mzunguko wake (menstrual cycle)siku ya 1-28
2.Lazima mzunguko wako uwe na mpangilio sahihi(unaweza ukachunguza mzunguko wako kwa miezi minne mfululizo)
3.PH ya uke lazima iwe kiwango sahihi 4-5.5(Tumia neplily pad kwa kuwa na PH sahihi
4.Ushirikiano kati ya mwanamke na mwanaume

JINSI YA KUPATA MTOTO WA KIUME
Ili uweze kupata mtoto wa kiume kisayansi unashauriwa kushiriki tendo la ndoa siku ambayo yai litakuwa limetoka kama mzunguko wako uko sahihi ni siku ya 14
Njia nyingine ya kujua yai limetoka baba anaingiza vidole viwili ukeni wakati wa asubuhi na ukikuta uteute ujue yai limetoka kwahiyo jioni mnashiriki tendo la ndoa kwa ajili ya kupata mtoto wa kiume

KWANINI USHIRIKI TENDO LA NDOA WAKATI YAI LIMETOKA ILI KUPATA MTOTO WA KIUME?
Kisayansi chromosome Y ambayo inahusika katika kutunga mimba ya mtoto wa kiume ina spidi kubwa sana ni nyepesi na haiwezi kisihi mda mrefu kwahiyo ukishiriki tendo la ndoa wakati yai limetoka maana ake unaongeza nafasi ya kupata mtoto wa kiume

JINSI YA KUPATA MTOTO WA KIKE
Ili ufanikiwe kupata mtoto wa kike utatakiwa ushiriki tendo la ndoa siku tatu kabla ya yai kupevuka yani hapa ni baada ya kujua mzunguko
KWANINI USHIRIKI TENDO LA NDOA SIKU TATU KABLA
Hii ni kwasababu chromosome X ambazo ndo zinaunda mtoto wa kike huwa zina sifa ya kuwa na maisha marefu na kutembea taratibu hivyo yai likitolewa litakuta chromosome X ziko hai

KUNA BAADHI YA WAZEE WA ZAMANI WANAAMINI HAYA KATIKA KUPATA MTOTO WA JINSIA UNAYOTAKA
KUPATA WA KIKE
Kula samaki ,mboga za majani,matunda,bidhaa za maziwa,mbegu za matikiti majia na alzeti nk
Wakati wa kufanya tendo la ndoa mwanamke akae juu nk

KUPATA WA KIUME
Kula nyama, ndizi ,Vyakula vya chumvi kama chips ila usizidishe chumvi,karanga na vyakula vingine vya potassium na sodium
Chromosomes Y zinahitaji pH ya alkane kuliko asidi ndio maana wazee waliona hili
Kuna mengi kuhusu wazee wa zamani ila nmeongelea haya ya mlo kwa maana yana mantiki kibaiolojia

MAMBO YANAYOWEZA ATHIRI KUPATA MTOTO UNAYEMTAKA
1.Kushindwa kuhesabu siku( tumia chart niliyokuwekea)
2.Mzunguko mbovu wa hedhi(Tumia neplily pad)
3.KUtokuwa na PH sahihi ukeni tumia Neplily

mwisho
PUNYETOOOOO....PUNYETO........PUNYETOOOOO
 
Na wale wanaokuwa na watoto wa jinsia moja vp tena wengine ni madktari ila unakuta ana vibinti vyote ndo kwamba huwa hawataki madume au inakuaje?
 
KUHUSU KUPATA MTOTO WA KIKE AU KIUME WAKATI WA KUJAMIIANA

Nadharia inasema hivi,Mbegu ya kiume[XY] ni ndogo kiumbile,ina kasi sana kutokana na udogo wake lakini tatizo lake ni dhaifu[less resilient],inawahi kufa.
Mbegu ya kike[XX] ni kubwa kiumbile,haina kasi sana ukilinganisha na ile ya kiume lakini inauwezo wa kuwa hai kwa muda mrefu kuliko ile ya kiume.

KUTOKANA NA SIFA HIZO

1. Mwanaume mwenye uume mrefu[LONG SHAFT],au staili ya NGONO ambayo itaufanya uume kuingia ndani zaidi yaani karibu na shingo ya kizazi(cervix) ana nafasi kubwa ya kupata mtoto wa kiume kwasababu mbegu za kiume kwa speed zilizonazo zitawahi kulifikia yai mapema kabla hazijachoka kwasababu zitakuwa zimesafiri umbali mfupi tu.
Sasa wale wenye MAUMBILE MADOGO ina maana mbegu zitamwagwa kina kifupi tu karibia na uke,zitalazimika kuogelea umbali mreeefu hatimaye zile za kiume zinapitwa njiani na mbegu za kike kwasababu za kiume zitawahi kuchoka mapema.

2. Kutegemeana na muda ngono ilipofanyika:inaaminika ukifanya ngono siku kadhaa kabla ya ovulation[kupevuka kwa yai kutoka kwenye ovary],mbegu za kiume kwasababu ni dhaifu zitawahi kufa na kubakiwa na mbegu za kike ambazo huleta mtoto wa kike.
Lakini ukifanya ngono siku ya ovulation[yai linapokuwa tayari],uwezekano wa kupata kidume ni mkubwa kwasababu mbegu za kiume zitakuwa zingali hai.
Sasa kuijua sawasawa siku ya ovulation ni shughuli pevu.

3. Mwanamke kufika kileleni[Female orgasm]
Mwanamke anapofika kileleni,viungo vyake vya uzazi kwa mfano vagina,cervix ,uterus,fallopian tubes vyote vina vibrate[involuntary muscle contractions].kukaza huku na kuachia kwa misuli ya sehemu hizo husaidia mjongeo wa mbegu za kiume kwenda vizuri mpaka sehemu ya urutubishaji[fallopian tubes].
Hivyo basi kumfikisha mwanamke kileleni ni suala la muhimu sana kwa kupata mtoto wa KIUME.

HAYA KAZI KWAKO MSOMAJI.
 
asante
 
Kwanza ujue mzunguko wa mwanamke. Tuchukulie ni siku 28 za mzunguko kutoka hedhi hadi hedhi..

Siku ya Mtoto wa kiume ni kuanzia siku ya katikati ya mzunguko namaanisha siku ya 14 toka hedhi. Unaposex siku ya 14, 15 kwa mzunguko wa hedhi wenye siku 28 uwezekano wa mtoto wa kiume ni mkubwa sana.

Kwa mtoto wa kike ufanye mapenzi siku kuanzia ya 11 na 12 yaani kabla ya siku ya peak hii ni kwa sababu mbegu za mtoto wa kike zinachelewa kufa kuliko za mtoto wa kiume. Hivyo uwezekano wa mtoto wa kike ni mkubwa.
 
taez ndo nini Mkuu. .Kuwa serious kwenye vitu serious basi .unaandika kama mtoto mdogo kumbe ni Baba mtarajiwa.
usilete mambo ya Insta hapa .Ebooooo
Athante nilimanisha taezaje/tawezaje kupata mtt WA kike au kiume
 
Kwanza ujue mzunguko wa mwanamke. Tuchukulie ni siku 28 za mzunguko kutoka hedhi hadi hedhi..

Siku ya Mtoto wa kiume ni kuanzia siku ya katikati ya mzunguko namaanisha siku ya 14 toka hedhi. Unaposex siku ya 14, 15 kwa mzunguko wa hedhi wenye siku 28 uwezekano wa mtoto wa kiume ni mkubwa sana.

Kwa mtoto wa kike ufanye mapenzi siku kuanzia ya 11 na 12 yaani kabla ya siku ya peak hii ni kwa sababu mbegu za mtoto wa kike zinachelewa kufa kuliko za mtoto wa kiume. Hivyo uwezekano wa mtoto wa kike ni mkubwa.
Umenitosha tajitahid sana kutumia huu utaalamu wako mkuu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom