Jinsi ya "Kubakwa"... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jinsi ya "Kubakwa"...

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Tuko, Jun 18, 2011.

 1. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #1
  Jun 18, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 395
  Trophy Points: 180
  Najua inatia uvivu kusoam posts ndefu kwenye MMU. Hata hivyo kutokana na unyeti wa lecture yenyewe, sitaweza kuifupisha zaidi ya hapo.

  Tando la ubakaji au jingine lolote la kudhalilisha kijinsia ni tendo baya ambalo mbali na madhara ya kimwili anayopata muathirika, pia huleta madhara makubwa ya kisaikolojia. Nimewahi kujiuliza kuwa ni kwa nini baadhi ya wanawake wanafariki au kuumia sana wanapobakwa hasa na zaidi ya mtu mmoja? Nilijiuliza hivyo kwani najua kuna wanawae wanaweza kuingiliwa na wanaume zaidi ya mmoja kwa hiari na wasipatwe na matatizo makubwa.

  Baada ya kujifunza mambo tofauti, katika sehemu tofauti, nimepata jibu kuwa asilimia kubwa ya wanawake (sijui wanaume) wanaoumia au kufa wakibakwa, inatokana na jinsi wanavyoreact dhidi ya tendi lenyewe.
  Hivyo, mafunzo kadhaa ya jinsi ya kukabiliana na mbakaji/ubakaji (kwa mfano UN field security course) yanatoa mbinu za kukabiliana na ubakaji kwa mwanamke
  Kwanza jihadhari sana na matendo au mazingira yanayoweza kukupelekea kubakwa. Hata hivyo, inapokuwa imetokea na huna jinsi ya kujikinga, fanya yafuatayo

  Kwanza, angalia kama kuna uwezekano wa kusaidiwa endapo utapiga kelele, kama haupo, usipige kelele.
  Hii itasaidia wewe usitumie nguvu nyingi, itamfanya mbakaji asikudhuru au kukukaba. Baadhi ya watu hapata madhara makubwa kutokana na jinsi anavyodhibitiwa na mbakaji, hasa kutokana na kupiga kelele.


  Pili, angalia uwezekano wa kuongea na mbakaji, kama inawezekana, ongea nae kwa upole na umsihi afanye hilo tendo kwa utaratibu.
  Madhara makubwa kimwili hutokea pale mbakaji anapotumia nguvu nyingi. pia mbakaji hajali kuwa mbakwaji amekaa position gani au amelalia nini. Madhara pia huongezeka pale mbakaji anapofanya tendo kwa muda mrefu. Inafahamika kuwa endapo mwanamke akimpa nafasi nzuri mwanaume, basi mwanaume hufika kileleni mapema, lakini mwanamke akimsumbua mwanaume, mwanaume huchelewa sana kufika kileleni.


  Kama haonyeshi dalili za kukusikiliza, basi wewe mwenyewe toa ushirikiano kadiri unavyoweza, ili tukio hilo lifanywe kwa utaratibu
  Hili linaweza kuonekana kuwa ni jambo gumu katika mazingira ya kubakwa. Hata hivyo kwa faida yako mwenyewe, ni bora ukatoa ushirikiano wa kujenga mazingira ya utaratibu, ili usitumie nguvu nyingi. Asilimia kubwa ya wanaokufa kwa kubakwa, ni kutokana na kukosa hewa, hali inayosababishwa na vurugu au kuzibwa mdomo

  Usijaribu kutumia nguvu ya aina yeyote kama huna uhakika kuwa nguvu hizo zitakunasua kutoka kwa mbakaji
  Kama ilivyoelezwa hapo juu kuwa madhara hutokea pale mwanamke anapotumia nguvu na kusababisha mwili kuhitaji oxygen nyingi, wakati huohuo akiwa ama amelaliwa kifuani, au amezibwa mdomo, hali inayompunguzia uwezo wakupata hewa ya kutosha

  Tukio likimalizika, onyesha tabasamu, jifanye umefurahia, lakini usijiinue haraka ulipo, na usimwangalie sana mbakaji usoni
  Mbakaji anapofika kileleni, sexual emotion nayo huisha. Ni katika mazingira hayo anaanza kuwaza kuhusu kufungwa jela nk. Unatakiwa umzuge kuwa hujamaindi sana bali umefurahia. Baadhi ya wabakaji huwauwa victims pale anapohisi kuwa kutakuwa na ushahidi wa yeye kushitakiwa. Baadhi ya wabakaji, humtisha victim kuwa ukienda kusema nitakuua, na kwa hasira baadhi ya victims hujibu hapo hapo kuwa lazima nitasema, hali inayowahatarishia maisha yao.

  Kama umebakwa na mtu zaidi ya mmoja, jitahidi kuonyesha ushirikiano zaidi.
  Mara kadhaa. wanawake hubakwa na kundi la wanaume! Unatakiwa ujiweke katika hali ambayo wabakaji hawatatumia nguvu sana kukubana, kwani wanaweza kukuongezea madhara. Na kama ilivyoelezwa kabla, jinsi utakavyoonyesha ushirikiano, ndivyo watakavyofika kileleni mapema na kupunguza muda wa wewe kuumia. Tii kila watakalokutaka ufanye, kama una uwezo wa kufanya, uli kuepusha kukulazimisha, kwani itakuongezea madhara.

  Mara tu baada ya kubakwa usioge au kujifuta kabla ya kwanda polisi
  Mojawapo ya ushahidi mkuu wa ubakaji,ni kupatikana mbegu za mwanaume katika mwili au nguo ya mwanamke.

  Baada ya kubakwa, kabla ya kufanya chochote, anza kutumia dawa maalumu za ARV
  Zipo ARVs maalumu (hata huku kwetu zipo) ambazo endapo zikitumika kabla ya masaa mawili baada ya maambukizi, huzuia maambukizi ya HIV. Hizi ndizo wanazotumia watoa huduma za afya pale anapoji-inflict kwa bahati mbaya akihudumia muathirika au mtu asiye na imani nae. Hivyo baada ya kubakwa, jitahidi uwahi haraka kuzipata hizo ARV kabla ya masaa mawili

  USIMWAMBIE mtu yeyote kuhusu kubakwa kwako, hata kama ni ndugu au mume
  Madhara makubwa ya kisaikolojia humpata mtu aliyebakwa, pale anapohsi kuwa jamii imefahamu kuwa amebakwa. Jizuie kumwambia mtu yeyote kwanza, hadi akili yako itakapotulia

  Nenda polisi, na ukifika polisi, omba kama unaweza kusikilizwa na polisi mwanamke, kama haiwezekani, omba usimulie tatizo lako kwa polisi mmoja tu.
  Hii nayo inapunguza hatari ya muathirika kuumia zaidi kisaikolojia

  Kama umebakwa katika mazingira ambayo unahisi mbakaji au wabakaji hawawezi kukamatwa kirahisi, ripoti tatizo lako polisi, lakini waombe polisi wasianzishe uchunguzi kwa wakati huo
  Zaidi ya asilimia 60 ya madhara ya kubakwa, ni kutokana na kuathirika kisaikolojia kutokana na tukio lenyewe. Unasahuriwa kuwa, mara baada ya kuripoti polisi, tatizo lisianze kushughulikiwa mara moja, ili kutoa muda wa akili yako kutulia, na vile vile kukupa mda wa kujifitisha tena katika jamii na familia yako

  Usiamue kufanya chochote angalau kwa siku kumi na nne baada ya kubakwa
  Huu ndio mda mbao angalau yale madhara ya moja kwa moja ya kiakili yanakuwa yanapona. Kujiongezea mawazo kwa kuamua kufanya chochote (mfano kuacha kazi, kuhama, kuvunja ndoa, kulipa kisasi nk) kutakuongezea tatizo. Pia huu ndio muda utakaokuwa unatumia dozi ya ARVs hivyo mwili unahitaji kupumzika


  Ubakaji ni tatizo kubwa, tuungane kuutokomeza.   
Loading...