Jinsi ya kubadili mwajiri kwenye suala la mafao (NSSF)

nusuhela

JF-Expert Member
Jan 26, 2014
5,736
6,972
Habari zenu wakuu?

Leo nimekuja kwenu kutaka kujua taratibu za kufuata ili kubadili mwajiri kwa ajili ya issue ya NSSF.

Wakati najisajili na NSSF nilikua na kampuni X Ambayo nilifanyia kazi mwezi mmoja. Baada ya hapo nikapata kibarua kingine kwenye kampuni Y ambayo nimeifanyia kazi miaka miwili.

Kampuni X ilipeleka mafao ya mwezi huo mmoja. Na kampuni Y inadai wamepeleka mafao ya miaka yote miwili tangu mwezi wa kwanza mwaka huu. Lakini nikiangalia details zangu kwenye NSSF online statement nakutana na details za kampuni ya kwanza niliyoifanyia kazi.

Sasa shida yangu nataka kujua taratibu zipi nifuate ili kuweza kuingiziwa hiyo hela ambayo mwajili wangu wa kampuni Y amesema tayari zipo NSSF.

Mikataba ya kazi ninayl yote miwili maana ilikua ni kila mwanaka mna-renew mkataba.

Natanguliza shukrani
 
Simple mkuu, kama mwajiri wa pili ulimpa namba ambayo ulikua unaitumia kwa mwajiri wa kwanza na anadai amepeleka michango, mwambie akuonyeshe sheet ambayo huwa ina details zote na nssf wakipokea huwa wanagonga mhur na copy kumrudishia mwajiri. Pia, anaweza kuwa kweli amepeleka ila muda mwingne NSSF wao ndio huchelewa kuingiza, ukienda NSSF pia unapata uthibitisho mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom