The Consult
JF-Expert Member
- Jan 20, 2017
- 220
- 252
Makisio ya gharama kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi, hufanyika mwanzoni kabisa katika hatua ya uibuaji wa mradi (Project Planning Stage). Andiko la Mradi huweza kuonyesha tu jumla ya kiasi kinachohitajika kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi (total bottom-line cost ) au kuonyesha kwa kina kila kinachohitajika katika Mradi na gharama zake ( detailed breakdown of various costs ). Hii kwa kiasi kikubwa hutegemea muongozo wa mfadhili (Donor's Guide).
Kipengele cha makisio ya gharama katika Mradi huusisha vitu mbalimbali ambapo uwepo wa vitu hivyo, hupelekea mafanikio ya Mradi husika. Vitu ambavyo hupaswa kujumuishwa katika kipengele cha makisio ya gharama ya mradi ni kama ifuatavyo;
- Nguvu kazi (labors) hapa utapaswa kwanza kutambua aina ya watu unaowahitaji katika utekekelezaji wa Mradi wako, kwa maana ya ujuzi wao, uzoefu na viwango vyao vya elimu. Katika kupanga makasio ya kuwalipa hawa watu, ni vyema ukazingatia viwango vya malipo vilivyowekwa na mamlaka, pia viwango vya malipo vinavyofanywa na Taasisi zingine kwa aina ya watu wa namna hiyo.
- Vitendea kazi (Materials) hapa utaangalia vitendea kazi vinavyohitajika kwa ajili ya ukamilifu wa mradi. Kwa mfano; ununuzi wa kumputa, gari, mashine, vifaa vya stationary n.k. Wakati wa kufanya makadirio ya vitu hivi jitahidi kuzingatia ubora kwa sababu ufanisi/ubora wa Mradi hutokana na ubora wa vifaa vitumikavyo katika mradi huo. Pia makisio ya lazima ya we na uhalisia (Ila kumbuka kuzingatia mabadiliko ya thamani ya pesa; Shilingi moja ya leo ina thamani kubwa kuliko shilingi moja ya kesho)
- Usafiri (travel), kuna miradi ambayo utekelezaji wake huwalazimu watendaji kusafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Sasa hapa kuna mawili ima unaweza kufanya makisio ya gharama ya chombo cha usafiri (ununuzi wa gari/pikipiki) au makisio ya nauli kwa ajili ya kufika maeneo husika, itategemeana na kiasi ulichoruhusiwa kuomba.
- Kodi na malipo mbalimbali (facilities rental), Taasisi nyingi hutumia majengo ya kukodi kwa ajili ya kuendesha shughuli zao, hivyo hulazimika kufanya malipo baada ya kipindi fulani cha muda, lakini si majengo pekee, pia kuna baadhi ya huduma kama mawasiliano, maji, umeme, intaneti n.k hupaswa kulipiwa baada ya muda fulani. Hivyo katika ufanyaji wa makisio ya gharama ya mradi, unapaswa kujumuisha vitu vyote hivi, cha msingi makisio yako yawe halisi, na mwisho wa siku katika ufanyaji wa Tathmini ya mradi, mfadhili atahitaji uthibitisho juu ya matumizi haya.
- Mzabuni msaidizi/Mshauri (Subcontractor/consultant), huwa inatokea watendaji wa Mradi au Taasisi husika kukosa utaalamu au zana fulani ambazo zinahitajika katika utekelezaji wa Mradi, kwa mfano utengenezaji wa mifumo ya komputa, au uandaaji na utoaji wa mafunzo, hivyo haina budi kuazima kutoka nje, sasa basi; katika ukadiriaji wa gharama, ni lazima gharama za hawa watu wa nje (consultants/sub constructors) zijumuishwe pia.
- Gharama za dharura (contingencies), inashauriwa kwamba katika ufanyaji wa makadirio ya gharama, kuweka gharama za dharura pindi litokeapo jambo ambalo halikutarajiwa basi gharama hizi ziweze kutumika. Hapa inategemea na aina ya mradi unaofanya, pia na aina ya mfadhili. Wafadhili wengi katika Miradi ya Maendeleo ya Jamii, hawaruhusu ukadiriaji wa gharama ya dharura. Unachotakiwa kufanya katika uandaaji wa mradi wako ni kuhakikisha unakuwa na "RISK PLAN" hapa wewe na timu yako mtafanya "brainstorming" ili kutambua "possible risks", wakati wa utekelezaji wa Mradi, ukubwa na uwezekano wa hizo "risks" kutokea na kama zikitokea ni kwa namna gani mtazi-mitigate; kwenye "mitigation" hapa ndipo makisio ya gharama yatafanyika.
Ahsante
The Consult; +255 719 518 367
E-mail : theconsult38@gmail.com
Dar es Salaam
Tanzania
Home of Project Management, Strategic Management & Fundraising Strategies