Jinsi ya ku-design Blog inayolipa (Part 2):
Tunaendelea na sehemu ya pili ya somo letu
2. UNIQUENESS (UPEKEE)
Blog inayolipa lazima iwe ni ya kipekee (Unique). Hapa uwe makini kidogo maana hili ndilo lililo mhimu kuliko yote. Kama huwezi kumshawishi mtembeleaji mpya wa blog yako kuiona blog yako ni ya tofauti, nini kitamfanya aendelee kubaki hapo akisoma au arudi tena kesho kuona kama kuna jipya?
Njia pekee ya uhakika ya kuifanya blog yako ni tofauti na blog nyingine ni UPEKEE. Kama hakuna vitu vya kipekee kwenye blog yako usitegemee mtembeleaji wa kwanza au mpya wa blog yako kurudi tena au kuitafuta tena hiyo blog.
Ninaposema upekee kwenye blog naongelea vitu vikuu viwili ambavyo ni;
1. UNIQUE DESIGN/MUONEKANO WA KIPEKEE
Blog yako ili ilipe lazima iwe na muonekano wa kipekee. Muonekano wake kwa maana ya rangi, menu zake, namna inavyowasiliana na kujibizana na watembeleaji uwe ni wa kipekee na usiobadilika kila mara, mfano leo nimetembelea blog yako nakuta in background ya blue, kesho nakuta ina background nyekundu!, hapana, haiwi hivi. Unaweza kubadili muonekano wa blog yako baada ya miezi 6 au mwaka mmoja au miaka kadhaa, lakini siyo kila mara kwa sababu inaweza hata kuathiri kiasi cha uaminifu wa wasomaji wako kwako.
Hivyo unapofikiria kuanzisha blog yako fikiria pia juu ya kumpata mtengenezaji au designer wa blog atakayekutengenezea blog yenye muonekano wa pekee kwa maana kwamba blog yako haifanani fanani na blog nyingine kirahisi ili kukufanya wa tofauti.
2. UNIQUE CONTENT/MAKALA ZA KIPEKEE ORIJINO
Hapa ndiyo penye shida sana hasa kwa bloggers wengi wa Tanzania. Yaani Bloggers wengi wanachofanya ni kusubiri website ya gazeti fulani au blogger fulani aandike makala na wengine wote wana-copy na ku-paste kwenye blog zao kwa kichwa cha habari kile kile na maelezo yale yale!. Ni vigumu kuwa na blog inayolipa kwa staili hii.
Ili kuwa na Blog inayolipa, blogger unatakiwa ushiriki kwenye kutayarisha, kuandaa na kuandika makala za blog yako wewe mwenyewe. Sasa kuna sababu gani ya mimi kutembelea blog yako kama makala zako zote una-copy toka blog ya Shigongo?, ni heri nifunguwe kila siku blog ya Shigongo ambako nitapata orijino stori badala ya kuja kwako. Hii inaathari nyingi ikiwemo kukosa traffic kutoka search engines kama vile google.
Kuna vitu vingi sana unavyoweza kuviandika. Lakini wengi wanapenda kuandika tu juu ya mapenzi, michezo na siasa. Unaweza kuandika juu ya somo lolote iwe ni hesabu au biolojia, unaweza kuandika kuhusu kilimo, ufugaji, ujasiriamali, uchumi, afya, utalii, hoteli, shule, saikolojia, ushauri, malezi, na mengine mengi bila idadi na ukaeleimisha jamii inayokuzunguka.
Kwanini watu wanatembelea blog yako? Kwa sababu kuna jambo wanataka kusoma au kujifunza. Ukiwa blogger huna tofauti na mwalimu. Mwalimu au profesa wa chuo kikuu analipwa mshahara kwa sababu kuna kitu fulani anachofundisha.
Anzisha blog, chagua mada maalumu na udumu kwenye mada hiyo ukiifundisha kila mara kidogo kidogo. Andika habari au makala ambayo haifanani na wengine lakini yenye msaada kwa msomaji. Andika jambo likakamilika.
Kuna ushindani mkubwa na unaozidi kuongezeka siku hadi siku kwenye sekta hii ya uandishi. Andika kitu cha pekee (unique story) na mhimu kuliko yote, stori iwe ni yenye kumsaidia au kumuongezea thamani msomaji wako.
Kwa ufupi, sehemu hii ya pili inagusia kwenye jambo la UPEKEE, Upekee kwenye muonekano wa blog, kazi ambayo siyo yako wewe blogger bali ni kazi ya msanifu/designer wako na upekee kwenye makala au stori zako, kazi ambayo ni yako moja kwa moja.
UVIVU ndilo neno pekee linaloweza kusomeka na likaleta maana ukianzia kulisoma upande wowote iwe ni kushoto au kulia.
Tutaendelea na sehemu ya tatu
Karibuni kwa michango