jinsi watu wa tiba asili wanavyoua taaluma yao kwa ujanja ujanja na usanii mwingi

pakamwam

JF-Expert Member
May 28, 2013
516
653
sita sahau mwaka 2011 pale jamaa yangu alipolazwa kwa mtu wa tiba asili baada ya kupata gono. baada ya wiki mbili bila nafuu na hali kuzidi kuwa mbaya ndio akanipigia nimpe ushauri afanye nini?. wazee wetu vijijini wanajua dawa sana lakini huwakuti kudharau hospitali na kujitangaza sana kwa kuwadanganya watu kuwa wanatibumagonjwa yote. hawa watu wa tiba asili utasikia wanaweza kutibuhata ukimwi na kansa,

tuwe makini na hawa watu wa tiba asili wa mjini na hata vijijini baadhi , wengi ni wababaishaji na wasomaji wazuri wa wikipedia ndio waje kwadanganya watu. ajabu ni kwamba mtu wa tiba asili hanaga ugonjwa anaoshindwa kabisa. utakuta mtu hazai baadala ya kutafuta sababu ya kutokuzaa ana mpa bla bla nyingi na kumlia pesa nyingi sana au mgonjwa wa ukimwi baadala ya kumsaidia anakula pesa nyingi sana.mtu anaanza kuwambia watu eti baada ya muda fulani akitumiajuice yake atapungua unene na anatumia pesa nyingi baadaye unaona kitambi pale pale

moja ya sababu za ongezeko la watoto pori ndani ya ndo linaweza kuchangiwa na hawa wanaojiita waganga wa tiba asili. nimekutana na watu wengi sana, akiendakupima kwa waganga wa tiba asili utamkuta ana UTI, sijui upungufu wa vitamini na wisho wa siku anapewa dawa za gharama kubwa, nenda ukampime utakuta hana kitu

sikatai kuwa dawa asili zinaweza kuponya ila nasema wengi walioingia hukoni wajanja wajanja tu. mtu anasema vitamini au matunda kwa ni wapi au nani asiyejua umuhimu wa hivyo vitu kwenye mwili?

ebu jamani anzeni na hospitali na tena za serikali katika kutafuta suluhisho la matatizo yetu maana wataalam wengi wazuri wako huko, ikishindikana ndio nendeni huko kama imeshindikana kabisa. kama kuna shida kwenye hospitali zetu za serikali basi tuzirekebishe, haiwezekani watoto wetu wataalam mbali mbali wa afya tusomeshe kwa gharama kubwa alafu washindwe kutusaidie. kama kuna shida kwenye mfumo wetu wa matibabu basi tukae pamoja na kuufuma ili kila mtu awajibike sawa sawa

pia serikali yetu ina mfumo mzuri sana wa tiba kuanzia zahanati mpaka hospitali ya taifa, shida ni kuondoa ile imani kuwa tiba ni siku moja hadi wiki, ni vizuri kulewa kuwa tiba huchuukua mlolongo mreefu na inaweza pia ikachuka hatamiezi kadhaa

pia namalia kumpongeza kigwangara kwa kazi nzuri ya kutuondolea matapeli mitaani.
 
Back
Top Bottom