Jinsi Viongozi wa Serikali wanavyokula Kodi na Pesa za Mikopo

Jinsi Viongozi wa Serikali wanavyokula Kodi na Pesa za Mikopo

Mfano kabisa ni kuhusu suala la Sukari linalomuhusu yule bwana wa kujiita Husein bashe, ambaye alishiriki wizi wa aina hiyo, wa kuinyakua tenda ya deal la sukari kwa kampuni fake ambayo haina hata sifa ya kuagiza pipi nje ya nchi (Stationary). Hii nchi tulipo ni Miujiza tu ndio itakayobadili hii mifumo ya kishetan kutoka kwa CCM.
 
upo sahihi kabisa, yani watu wanapiga dili hazarani
 
Mimi ningekuwa huko Serikalini kwa kweli mngekoma nafikiri kwa aina ya ufisadi ningefanya wenyewe mngetoka na kuandamana na kupindua serikali🤣
 
Nakiri kabisa ni kweli Mange anavyosema kuwa Viongozi wa Serikali wanajilimbikizia mali, kupitia mikopo na kodi za Serikali.

Viongozi wa Serikali licha ya kunufaika kwa kuwaingiza watoto wao Serikalini na kuwapa ajira na teuzi za upendeleo, huo ni upande mmoja wa namna wanavyojinufaisha.

Njia nyingine kubwa inayowapa utajiri mkubwa viongozi wa Serikali ni kupitia zabuni zinazotolewa na Serikali. Taasisi zote kubwa za Serikali zinazoongoza kutoa zabuni kubwa, huwa kila kitu kinakuwa controlled na Ikulu kupitia wizara husika. Hata ishu ya Richmond ilianzia Ikulu na kusimamiwa na Lowassa.

Kinachofanyika, Serikalini kwa kuona umuhimu, ama ikijisikia tu inaanzisha mradi au miradi, mingi ambayo kwa kweli ina manufaa kwa wananchi — Serikali ikianzisha miradi hiyo inaenda kukopa pesa kwa niaba ya wananchi ili kutekeleza miradi hiyo. Hapo tayari ikiwa na kampuni zao mifukoni (za hao mafisadi) ambazo ndizo zitakazofanya kazi hizo.

Taasisi au Serikali zikitangaza zabuni, ni mambo yale yale ya NEC na tume zao za maigizo. Bodi za zabuni na wakuu wa taasisi hupewa maelekezo kampuni fulani zipatiwe hiyo kazi, hivyo mchakato wa utoaji zabuni haupo huru. Na huku ndiko wanakopata huo utajiri mkubwa. Hili ni jambo kubwa la mgongano wa maslahi.

Ishu nyingine ni ya uchaguzi. Pale ni maslahi tu. Tena maslahi ya kupata madaraka na pia ya kupata fedha nyingi. Viongozi wa Serikali na CCM wametenga bilioni 700 za uchaguzi na wameshagawana tenda za zabuni mbalimbali za mambo ya uchaguzi. Hivyo, lazima walazimishe uchaguzi ufanyike tena ule usio wa wazi.

Sukari nayo ni hivyo hivyo.

Nalia machozi kwa uchungu. Nchi ipo mikononi mwa wachache. Msione Makonda anawapenda sana, ni ubunge wa maslahi binafsi.
Ulichoandika ni kweli na sahihi.
Mimi binafsi nina ushahidi wa hili.

Siki moja (mwaka 1990), nimefika hom - Uzunguni hapa Dom, namkuta marehemu mzee wangu na watu watu wawili.
Akanitambulisha kwao (mmoja alikuwa ni KM wizara fulani na mmoja alikuwa ni mhadhiri mwandamizi pale UDSM).
Wale watu ndio walikuja kuwa mentors wangu kwenye mfumo wa zabuni za serikali, na ndio wamenifikisha hapa nilipo.

Hizi tenders almost zote, hawa viongozi wana mikono yao, hili naishi nalo mpaka kesho.
 
Angalau umeongea kitu wanaweza kuelewa watu, usishangae kwanini Watu wanataka ubunge, ukipata ubunge, ukawa waziri , madili ni wazi wazi, hadi zabuni za bungeni hata kuhudumia mgahawa wa bunge , wamempa mbunge sijui nani, sisi raia tunabaki kulima na kuendesha boda boda
 
Kwa bahati mbaya sana wenye serikali hawajui haki zao.Kwenye chaguzi wanaishia kupewa viTshirt na vijora
 
Back
Top Bottom