ubarinolutu
JF-Expert Member
- Oct 22, 2012
- 2,711
- 5,641
Nakiri kabisa ni kweli Mange anavyosema kuwa Viongozi wa Serikali wanajilimbikizia mali, kupitia mikopo na kodi za Serikali.
Viongozi wa Serikali licha ya kunufaika kwa kuwaingiza watoto wao Serikalini na kuwapa ajira na teuzi za upendeleo, huo ni upande mmoja wa namna wanavyojinufaisha.
Njia nyingine kubwa inayowapa utajiri mkubwa viongozi wa Serikali ni kupitia zabuni zinazotolewa na Serikali. Taasisi zote kubwa za Serikali zinazoongoza kutoa zabuni kubwa, huwa kila kitu kinakuwa controlled na Ikulu kupitia wizara husika. Hata ishu ya Richmond ilianzia Ikulu na kusimamiwa na Lowassa.
Kinachofanyika, Serikalini kwa kuona umuhimu, ama ikijisikia tu inaanzisha mradi au miradi, mingi ambayo kwa kweli ina manufaa kwa wananchi — Serikali ikianzisha miradi hiyo inaenda kukopa pesa kwa niaba ya wananchi ili kutekeleza miradi hiyo. Hapo tayari ikiwa na kampuni zao mifukoni (za hao mafisadi) ambazo ndizo zitakazofanya kazi hizo.
Taasisi au Serikali zikitangaza zabuni, ni mambo yale yale ya NEC na tume zao za maigizo. Bodi za zabuni na wakuu wa taasisi hupewa maelekezo kampuni fulani zipatiwe hiyo kazi, hivyo mchakato wa utoaji zabuni haupo huru. Na huku ndiko wanakopata huo utajiri mkubwa. Hili ni jambo kubwa la mgongano wa maslahi.
Ishu nyingine ni ya uchaguzi. Pale ni maslahi tu. Tena maslahi ya kupata madaraka na pia ya kupata fedha nyingi. Viongozi wa Serikali na CCM wametenga bilioni 700 za uchaguzi na wameshagawana tenda za zabuni mbalimbali za mambo ya uchaguzi. Hivyo, lazima walazimishe uchaguzi ufanyike tena ule usio wa wazi.
Sukari nayo ni hivyo hivyo.
Nalia machozi kwa uchungu. Nchi ipo mikononi mwa wachache. Msione Makonda anawapenda sana, ni ubunge wa maslahi binafsi.