Jinsi taa hizi zinavyotumika vibaya!

Jinsi taa hizi zinavyotumika vibaya!

chambimagaka

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2017
Posts
288
Reaction score
338
*MADHARA YA KUWASHA DOUBLE HAZARDS KWENYE ZEBRA NA MAKUTANO YA BARABARA*
(Hazard Warning Lights)
*Utangulizi*
Mara kwa mara tumekutana na madereva ambao wakiwa wamesimama kwenye zebra kupisha watu wavuke au wakiwa kwenye makutano ya barabara ya msalaba (cross junction) yasiyoongozwa na taa huwasha taa mbili zenye kumweka mweka (kuwaka na kuzima) maarufu kama double hazards. Matumizi ya taa hizi yamekuwa yakichanganya sana, na wakati mwingine tumesikia madereva wakilalamikia kulazimishwa na askari kuwasha double hazards wanaposimama kwenye zebra kuwapisha waenda kwa miguu. Lakini swali ni je, sheria inalazimisha kuwasha taa hizo katika mazingira hayo? Na je endapo utawasha, nini yaaweza kuwa madhara yake?

*Kabla ya kujibu swali hili* kwanza tukumbushane kuwa tunaishi kwenye ulimwengu wa kimataifa ulio na mtangamano (integrated world) ambapo barabara za nchi moja hazitumiki na watu wa nchi hiyo tu bali hutumika pia na wageni. Hii ndio sababu alama za msingi za barabarani zinafanana karibu duniani kote. Alama ya STOP utakayoiona Tanzania ndiyo hiyo hiyo utakutana nayo penginepo ulimwenguni. Tunachotofautiana sana ni zile alam za ziada (secondary signs). Jambo hili litupe picha ya madhara tunayoweza kupata barabarani ikitokea kuna mchanganyiko wa watu wa mataifa mbalimbali.

*Matumizi ya double hazards na madhara yake*
Taa za double hazards hutumika kuashiria dharula aliyonayo dereva anayeziwasha taa hizo. Hivyo kuonesha uhitaji wake wa msaada au kuashiria hatari anayokabiliwa nayo. Sasa endapo dereva huyu atakuwa barabarani akawasha double hazards huku akiwa amesimama au kuegesha gari, moja kwa moja dereva wa nyuma atatafsiri kuwa dereva huyo wa mbele ana dharula.Hivyo atakachofanya ni kumpita (ovateki).

Na kwa upande wa makutano, endapo dereva anayenyoosha moja kwa moja akiwasha double hazard anaweza kusababisha dereva wa nyuma ampite au dereva wa upande mwingine asiyeiona taa ya upande wa pili ya huyu dereva kudhani dereva huyu anataka kupinda kulia au kushoto. Matokeo ya mkanganyiko huu ni ajali. Na baada ya ajali madereva hawa wakiulizwa, kila mmoja atasema *nilidhani…..nilidhani….ndio maana nikapinda huku au nikampita*. Kuondoa mkanganyikop huu na hatari ya kugongana au kugonga,sio vizuri kuwasha double hazards kwenye zebra au kwenye makutano.Brake lights zinatosha sana kumuashiria dereva wa nyuma kuwa umesimama.

*Sheria ya Usalama Barabarani*
Sheria mama ya Usalama barabarani(THE ROAD TRAFFIC ACT Cap 168) na hata Highways Code ya Tanzania ipo kimya katika jambo hili, kwa maana ya kwamba haioneshi popote kama ni lazima dereva kuwasha hazards. Maana hata katika alama tulizofundishwa za kuonesha uelekeo (direction indicators) double hazards hazimo. Ishara zilizopo ni ishara za indiketa (Direction indicator signal), ishara za brake (Brake light signals) na ishara za mkono (arm signlas).
Kwa mujibu wa kanuni ya 116 ya Highways Code ya Uingereza, hazard warning lights zinatakiwa kutumika pale t ugari likiwa limesimama, halitembei ili kuwapa tahadhari watumiaji wengine wa barabara kwamba gari limesimama linazuia mtiririko mzuri wa magari. Taa hizi hazitakiwi kutumika
(a) Kwaajili ya kuhalalisha wrong parking au parking yoyote ya hatari;
(b) Unapoendesha au kuvutwa na gari jingine barabarani isipokuwa tu pale unapokuwa katika barabara kuu na unataka kuwaonya wengine kuwa gari lako linaweza kuwa kipingamizi kwao;
Nimelazimika kurejea kwenye sheria za uingereza kwa sababu sheria yetu sisi ya usalama barabarani asili yake ni Uingereza, kwa hiyo kunapotokea jambo fulani katika sheria zetu halina tafsiri ya moja kwa moja au halina kipengele inabidi turudi Uingereza zilikoanzia sheria zetu tuone wenzetu wanasemaje kwenye sheria yao.
Ili kuwahakikishia usalama waenda kwa miguu, ukisimama kwenye kivuko cha waenda kwa miguu (zebra) tumia ishara ya mkono (arm signal) kumzuia dereva wa nyuma asikuovateki na sio kutumia hazards.

RSAadmin1
RSA TANZANIA
USALAMA BARABARANI NI JUKUMU LETU SOTE.
 
Nimeelewa naomba kuuliza kidogo nje ya mada: je ni kosa kisheria kuwasha taa za usiku wakati wa mchana!?
 
Back
Top Bottom