Jinsi nilivyowahi kuumbuka

Hii imenikuta juzi hapa hapa nilipata kidosho toka Iringa nikapiga sound mtoto akaingia laini tukapeana promise siku tuonane siku ya siku ikafika mzee mzima nimeulamba nikakutana na kidosho basi nikawa natafuta kiwanja mulua cha kupoa nae mtoto wa kihehe nikapata kiota mulua naingia tu nakuta kiti akatokea mzee mmoja wa makamu sana akanishika mkono akaniuliza huyu kwako nani kabla sijajibu akashika mkono wa kidosho akamuuliza huyu nani wako akasema ndugu yangu mm nikawa mdogo pale pale yule mzee nikamwangalia ni babu yangu kumwangalia binti ni 21yrs dingi akaaanza kukoloma huyu ni mke wangu nimegaramia kutoka Iringa mpaka hapa wewe unajibebea kiulani ikabidi watu waingilie kati wakajua mm na uhusiano na mwanafunzi kuja kusikia maelezo ya babu yule akasema mke wake. Nilichoka nikaishiwa pumnzi pale pale.
Watu nao pale wakachoka ikabidi waanze kumzomea mzee yule ooof FATAKI huyoo.
 

Hahaaahaaa! we ulinusurika kifo pia!
 
Pole sana mheshimiwa, ila nimecheka mbavu sina. Jambo moja linalonishangaza, yaani ukakubali risk ya kuruka watu wote hao ukamfuate huyo Suzy pembezoni alikolala? What if watu wengine wangestuka in the process?

Dina ndugu yangu, ilikuwa nimshitue anifuate turudi pale kivulini. Lile jangwa lilinitia upofu! Hata wapi ningemfuata! Lakini ah! sijui na zile bia zilinichanganya! AU Akili ya ujana tuu, sikuweza kujiuliza kitu!
 

Mhhh! angekuchoma mkuki!
Kumbe hivi visa huwakuta watu wengine pia ee? afadhali bwana kifo cha wengi harusi!
 
Mhhh! angekuchoma mkuki!
Kumbe hivi visa huwakuta watu wengine pia ee? afadhali bwana kifo cha wengi harusi!

Mkuu mpaka leo siamini kile kibabu kinaweza kika niloga hivi hivi sijiamini kabisa.
Nilikoswa koswa angekuwa na sime angenimwaga damu.
 
MwanajamiiOne, darasa la tatu unasome twisheni....au ndo mmesoma juzi juzi hapa hizi shule za akademi manake hazina dogo, unalijua azimio la arusha? LOL
 
MwanajamiiOne, darasa la tatu unasome twisheni....au ndo mmesoma juzi juzi hapa hizi shule za akademi manake hazina dogo, unalijua azimio la arusha? LOL

Mbona sie tuition ilikuwa tangu std 2!! Si unajua tena shule za kapumua nani, mwalimu anataka ahemee hapo hapo. Ilikuwa tuition ya lazima ndugu yangu.
 
Mbona sie tuition ilikuwa tangu std 2!! Si unajua tena shule za kapumua nani, mwalimu anataka ahemee hapo hapo. Ilikuwa tuition ya lazima ndugu yangu.

MJOne, ndo maana nikapata picha kuwa ni za siku za karibuni za ubepari-ujamaa, enzi zetu za mwalimu hakuna mwalimu alikuwa anajua tuisheni....lol
 

....Mjamii, inaelekea ulikuwa umejazia jazia hivi! yaani uko darasa la tatu na bado njemba zinakukomalia??
 
Kwa maana halisi ya neno hilo Mzizi wa Mbuyu- nilikuwa nasoma kwa wanyantuzu kanda ya Ziwa!

Alaah! wale jamaa nasikia ni wataalamu sana wa mambo yale, kuna kamchezo wanakaita CHAGULAGHA! Yaani ni usombaji tu..pole sana ulinusurika!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…