Jinsi nilivyonusurika kutapeliwa iPhone yangu

instagram

JF-Expert Member
May 27, 2014
2,091
4,715
Ilikuwa 2010 enzi hizo ninauza iphone 3 Gs yangu kupitia mtandao wa gazeti la Advertising Dar, jamaa moja kapiga simu anadai yeye anafanya kazi Barclays Mbeya yupo likizo Dar. Sharp tukapatana bei laki sita basi jamaa tumepanga tukutane Mwenge.

Kufika mwenge jamaa katokea na teksi akadai twende Slipway Masaki ndo hoteli alikofikia kuna ATM akatoe hela.

Tumefika Slipway jamaa kamuacha dereva kaniambia tushuke, basi tumeenda hadi kwenye restaurant, jamaa kamuita waiter "oya msikilize jamaa hapa unakunywa nini bro? Agiza chochote mimi naenda mara moja hotelini kuchukua hela then tumalizane"

Jamaa kachukua simu yangu kanipa boksi nishike nikimsubiri. Akili yangu ikaniambia huyu mwanzo alisema kuna ATM atachukua hela then sasa anasema akachukue hela hotelini.

Nikamuambia oya nipe kwanza simu niondoe contact zangu kwanza na vitu vyangu nikupe ikiwa tupu, akadai haina shida nitatoa mwenyewe.

Nikaona huyu mbona mbishi nikamuambia nipe simu yangu, nikaona sura inabadilika nikachukua simu yangu. Nikakaa pale muhudumu kaniuliza unakunywa nini? Nikamuambia hapana sinywi chochote.

Nikanyanyuka nikaenda nje parking nakuta ile gari ishaondoka.

Nampigia simu jamaa hapokei alafu akazima kabisa.

Kumbe mjinga alitaka niagize kitu pale ili nizuiwe kutoka kwenye mgahawa wakati yeye kasha niibia.

Nikikumbuka hii ishu huwa nacheka sana mjinga alinikodia hadi teksi aje kunitapeli yani angemkuta boya boya hivi angemdhulumu aisee.
 
Yani alafu sikuwa hata na hela ya kulipia chakula pale
Pesa kwako siku hiyo ilikuwa sio muhimu kutembea nayo si ulikuwa inaenda kuvuta mzigo? 🤣🤣🤣. Ungesahau Hadi jina lako, huku unasikilizia maumivu ya iPhone huku muhudumu kasimama na Shati lake jeupe anataka pesa.
 
Pesa kwako siku hiyo ilikuwa sio muhimu kutembea nayo si ulikuwa inaenda kuvuta mzigo? . Ungesahau Hadi jina lako, huku unasikilizia maumivu ya iPhone huku muhudumu kasimama na Shati lake jeupe anataka pesa.
 
Pesa kwako siku hiyo ilikuwa sio muhimu kutembea nayo si ulikuwa inaenda kuvuta mzigo? . Ungesahau Hadi jina lako, huku unasikilizia maumivu ya iPhone huku muhudumu kasimama na Shati lake jeupe anataka pesa.
Yani sikuwa na wasiwasi najua naenda kuvuta mpunga na budget zinajipanga zenyewe kichwani, enzi hizo laki sita ni kama millioni ya leo au zaidi.
 
Pole sana mkuu, town wajanja wengi nahisi alidhani kapata kitonga wake kumbe tayari we machare yashakucheza...wabongo sio wema
 
Wezi huwa wanajichanganya sehemu ndogo sana....ukiwa makini unashtuka kama ulivyoshtuka awali alisema kwenye ATM
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom