Nzi Chuma
JF-Expert Member
- Jun 21, 2015
- 475
- 1,176
Wakuu nawasalimu.
Ni mambo ya mitandaoni tu, nimekutana nae. Mrembo sana. Kwakua familia iko mbali kidogo, nikaona nitume nauli aje mkoani tuponde raha. Professionally ni nurse, na nliwasiliana nae kwa miezi zaidi ya mitatu nikajiridhisha kuwa ni mtu mzuri ameshika dini hana shida. Siku ikafika, nauli nkatuma, basi likapandwa. Katika kujihakikishia usalama wa afya zetu, alinambia atakuja na vipimo vya "HIV rapid test". Nikasema sawa.
Alipofika, kabla hatujaanza mambo yetu akatoa vipimo..akanitoboa akatoa damu akaweka kwenye kipimo akaweka vile vimaji akaweka chini kusubiri matokeo. Muda huo nikatoboa kidole chake tukaweka damu kwenye kipimo kingine. Majibu yangu yakatoka negative na yeye akaona dalili za kutoka positive.. akaanza kuzuga anashika kipimo.. nikampokonya nikaweka pale.. goma likasoma vistari viwili vya HIV-1, ambayo ndiyo HIV common kwa huku kwetu. Pozi likaniishia. Hamu ikakata. Nikamwambia lala mpaka asubuhi, nitakupa nauli uondoke kwa amani. Kulipokucha tu nikampandisha gari za kwao.
Tukirudi nyuma kidogo, najiuliza, ingekuaje kama asingekuja na vipimo na mimi nisivyoweza kutumia kondom? Ningefanyaje?! Si ningeikwaa ngoma kirahisi sana. Nimejifunza kuwa makini!. Vijana tuwe makini tutunze afya zetu na tuzidi kumuomba Mungu, ana kawaida ya kutuepusha na majanga tusiyoyatarajia.
Siku njema wakuu!