Alvin Slain
JF-Expert Member
- Aug 30, 2011
- 6,375
- 3,665
Mkuu hizo bidhaa ulizokua unazalisha ni bidhaa gani?
karibu.
karibu.
Nimekuelwea mkuu ila kuna baadhi ya nyuzi niliitaja biashara so kulinda identity kwa mawazo yangu madogo nikaamua kuficha baadh ya vitu ikiwemo bidhaa pamoja na locationMkuu pole sana ...ila nikushauri kitu njia bora ya kusaidiwa ni wewe kutoficha mambo muhimu .Mfano umesema kuna bidhaa ulikua unatengeneza hujataja jina la hiyo bidhaa kumbuka pengine kuna mtu anazo hizo bidhaa ila labda hana pa kuuzia au hajui kutengeneza ungeitaja ingekuja njia moja wapo ya kusaidiwa....
Kisa chako hakiko mbali mimi nilitapeliwa mwaka 2018 na jamaa nilimtrust ile mbaya kwa kushirikiana na mshikaji wangu, nilipoteza kila kitu almanusura nipoteze na nafasi ya elimu yangu..lakini M/Mungu alinitoa kule na leo alhamdulillah rizki napata nashukuru japo binadamu hariziki tunataka zaidi.
Sure mkuu yaani mpaka nimekuja kukubali hali halisi imenichukua muda sana yaani kila siku naona giza linazidi tu.Mkuu wewe ni MWANAUME! Hela ina formula Moja, NJIA YAKE NI ILEILE! Kama mto wa msimu vile, unaweza kukauka ila siku mvua ikinyesha maji yatapita njia ile ile tu!
Nakuombea mvua inyeshe tena kwako Mkuu.
Bad times don't last forever. There is always another door, keep fighting mdogo wangu.
Leather and culture productMkuu hizo bidhaa ulizokua unazalisha ni bidhaa gani?
karibu.
Pole sana Mwamba! Niamini mimi wewe utaingia kaburini ukiwa tajiri, it's a matter of time tu, usikate tamaa! YA MUNGU MENGI, KUKU YAKE MAYAI TU.Sure mkuu yani mpaka nmekuja kukubali hali halisi imenichukua mda sana yan kila siku naona giza linazid tu
Ulichosema cha kweli boss, changamoto wengi tunafanya biashara na hatuna mtu wa kutu guide unaweza ona unaenda mbele kumbe unachokifanya ilibid usubili kwanza ila kuwai kukakuponza ukakata mtaji mpemaWabongo wengi wana mapungufu kwenye ushirika kwa sababu ya uvivu na tamaa, ila sio wote, na muhimu ni kuweka kila kitu kwenye karatasi mwanzoni kabisa, na lazima uwe na mwanasheria, na auditor wa kukushauri, sio mpaka uwe na company.
Iwe hivyo mkuu👊Pole sana Mwamba! Niamini Mimi wewe utaingia kaburini ukiwa tajiri, it's a matter of time tu, usikate tamaa! YA MUNGU MENGI, KUKU YAKE MAYAI TU.
Mdogo angu usikate tamaa, hata siku moja, amini bado unaweza na bado una uwezo wa kutimiza ndoto zako, jiami, wekeza katika kutimiza malengo yako. No matter how many times you will fail, believe in yourself and don't hesitate to start again. Everything in life happens according to our time, and for a reasons, labda haikuwa muda wako sahihi wa kutoboa lakini naiona kesho yako iliyojaa mafanikio, muhimu kutokukata tamaa. And Do not let anyone rush you with their timelines, still at the age of 25 you have a lot to accomplish. Enjoy the rest of the day and stay strong.Wahenga walisema mbuzi wa masikini hazai hata akizaa ana zaa dume, ni msemo wa mda mrefu ila naamin unaishi,
Mwaka 2016 nilifanikiwa kumaliza kidato cha 6 ila matokeo yalivyotoka sikufanikiwa kuwa na pass mark za kunifanya niendelee mbele katika kipindi hiko nilihisi kuchanganyikiwa kwasababu nyumban mimi ndo mkubwa na wazazi walikua wameweka mategemeo makubwa kwangu na kwakua nyumbani hata msosi msosi ulikua wa kuunga unga hivyo sikua na option ya kuendele atena mbele kuhusu maswala ya elimu
Kipindi bado niko shule nilipokua nikirud likizo kuna rafiki angu alikua chuo kuna bidhaa X alikua nauza so baada ya yeye kuona sina ishu ya kufanya na kipindi hiko alikua yuko mwaka wa 3 aliniambia nikimbize ile biashara yeye kwa kipindi hiko alikua na mambo mengi ya kufanya akiwa chuon hivyo asingeweza kuwafikia wateja kwa urahisi
Japo haikua rahis ila nilikimbiza ile biashara kiasi cha kwamba ilikua kwa haraka na pale nyumbani mchango wangu ukawa unaonekana kwa 70% badae nikaja kupata wazo badala ya kwenda kununua hizo bidhaa X kwann nisi fanye production mwenyewe nikajaribu kufanya utafiti wa vifaa na kuanz kununua mdogo mdogo basic tools zote
Wateja wangu kwa 97% nilikua nawapata online kipindi nawatafuta wateja nilipata kufahamiina na jamaa mmoja yeye alikua anatoka mkoa Y ambapo aliniambia yeye anaweza kuzitengeneza hizo bidhaa hivyo wakati nafikiria kuzalisha mwenyewe nilijua kuna mtu ntaungana nae mwisho wa siku alifanikiwa kuja dar dar tukafanya kazi pamoja
Kazi ya uzalishaji haikua rahis kama nilivyotarajia maana ilikua na changamoto nyingi na inabidi uwe smart sana kuwez kui manage upande wa production kuja usimamizi wa kazi mpaka unapokuja kuuza na mwisho wa siku uione faida yako baada ya kutoa matumizi yote,mtaji na kuweka faida pembeni nashukuru niliweza kumudu vizuri kwa muda wa miaka 2 biashara ikawa imekua kubwa pia nilikua nmeshaanza kupata wateja nje ya nchi kama INDIA,BRAZILI,USA,OMAN NK kwa nchi za Africa nchi zote za SOUTHEN AFRICA(SA,BOTSWANA,NAMIBIA,ZIMBABWE,ZAMBIA) nan chi nyingine z hapa jirani
Mikosi ilipoanza
Wakati biashara ipo kwenye peak nilipata mteja mmoja aliyekua nchi Z alikua ni m tz ila makazi yake pamoja na biashara yake yalikua huko tulianza biashara vizuri na alikua mteja wangu wa nguvu sana kabla ya kuwa ananunua kwangu alikau anatoa Kenya hizo bidhaa ila alipoanza kwangu wateja wake walizipenda sana so speed ya jamaa kuagiza mzigo kwangu ilikua kubwa mpaka nikaamin huko kuna fursa kubwa ya kutoboa zaid kwa biashara yangu ikabid nionge na jamaa akakubali kua atanipokea
Kabla sijatoka huku kulikua na jamaa angu ambae alikua nilikua nafanya nae kazi nikampanga yeye abaki mm nikifika kule nitacheki mazingira yakiwa mazuri mimi nirudi yeye aende ili tuwe tunakimbiza huku na kule jamaa alikubali ila kwakua hakuna anayejua kesho kumbe nilikua najichimbia shimo kubwa mbelke yangu
Safar ikaanza ya kwenda kule miaka miwili iliyopita nikafika salama na nikapokelewa vizuri nilienda na bidhaa kidogo ili kuangalia mazingira yapoje, baada ya kufika nikaona kwa nature ya biashara ilivyo ili kujitofautisha na wengine siwezi kuuzia chini maana ntapunguza value ya bidhaa pia nikacheki nikaona kuna uwezekano wa kupata fremu bei ilikua 200USD kwa mwezi almost 460000 ya kitanzania na sio kubwa sana kulinganisha na huku kwetu za street ambapo huku unapata kwa 70K ambayo haipo center ila kwa kule ya ukubwa huo utapata kwa 500USD kwa mwezi na kwa nature ya biashara yangu kutoa 200USD sikuwaza maana nilijua nikiuza bidhaa 20 tu nmepata hela ya kodi na hizo naweza uza hatakwa mtu mmoja
Changamoto ilianza kuja baada ya jamaa niliyemuacha huku alikua anashindwa ku manage vzuri pia tulianza process ya kumtafutia passport huku ila mchakato ulikua mrefu sana hivyo mpaka mda wa mm kurud huku baada ya miez mi 3 ya kukaa kule ilikua bado hajapata, nilifanikiwa kurudi japo kwa njia za panya maana nilizidisha siku za kukaa kule hivyo ningerudi kihalali ingejua shida kwangu so nilipofika huku ikabi nirudishe ofisi kama mwanzo huku nikisubiri jamaa apate passport aende kule na kipindi chote hiko frem ilikua imefungwa na kodi ilikua inahesabiwa kama kawaida
Mpaka mwaka unakaribia kuisha jamaa alikua hajapata passport na mm kadri mda ulivyokua unazid kwenda nilijua jamaa mda wa kupata passport unakaribia hivo sikuwaza na kwakua sikukuu zilikua zinakaribia nika target soko la kule pia nili target ku clear makosa ya mwanzo maana soko la online hata ukiwa na bidhaa mbili unauza ila kwenye frem inahitaji uwe na mzigo mkubwa na upangilie vizuri ili mteja akipita mzigo umuite na umvutie kwa mpangilio wake
Nikaingiza 90% ya mtaji wangu wote nikiamini naenda kuuaga umasikini maana nchi niliyokua naenda ilikua ni center ya nchi nyingine za ukanda wa kusini na wengi wao walikua wankauja kuchukua mizigo hapo baada ya kila kitu kukamilika nikatuma mzigo na mm nikafika nkapanga mzigo vizuri ila safar hii ofisi ya dar niliifunga kwa mda ili jamaa akija kule nirudi kuifungua, nilivyofika ikabidi nilpe miezi niliyokua na daiwa baada ya hapo nikaanza kuuza mwaka jana mwanzon jamaa kapata passport so ikabdi mi nirud ye aje huku ila hata nilipofika huku mambo hayakua kama nilivyotarajia maana jamaa alisema hatoweza kwenda daah ilinikata sana nikiwaza 90% ya mtaji upo kule nikiwaza niende kule maana nakua naua ofisi ya huku na nikisema nibaki huku pia naua ofisi ya kule
Kila option nilyofikiria ili niweze ku maintain ofisi zote mbili ilifeli ikabid niongee na jamaa aliye nipokea mwanzo nikamuomba anitolee mzigo wote anitumie huku na nikamtumia hela ya usafirishaji ila mwisho wa siku mzigo haukutumwa na kipindi hiko corona ilikua ishaanza kuingia tz na mipaka yote ika fungwa so option ya kutuma mzigo ikashindikana na huku biashara ikaanza kudolola ikafikia stage nikawa nakosa hata hela ya pango nikiongea na jamaa kuhusu mzigo ananipiga chenga nikamwambia uza nitumie hela anadai biashara hakuna ila badae kwenye uchunguzi wangu nikaja kugundua jamaa aliuza inshort ameniingiza kwenye mataa na huo ndo ukawa mwisho wa biashara yangu
Kipindi biashara inafanya vzuri nilikua naona fursa nyingi za kibiashara nilikua nashaangaa kuona kijana anashindwa vipi kupanga mtu anakosaje hela ya vocha n.k ila saiv maisha yamebadilika ss ndo nimejua mtu anashindaje njaa na anakosaje kazi ya kufanya maana imefikia hatua kula yang tu ya shida fursa zote sizioni naishi kwa mshikaji tu nayy anakaribia kunichoka yani kila nikiwaza hatma ya maisha yangu siion
Nipo hapa wakuu kama mtu anafursa ya kazi iwe kibarua au parmanent sichagui kazi pia ninauzoefu wa mambo ya online marketing kama mtu ana bidhaa zake na anahitaji kuongeza sales naweza kufanya kazi hiyo pia, nipo dar, umri miaka 25 jinsia ya kiume na nipo tayar kwenda kufanya kazi mkoa wowote ule
Shukrani mkuu, binafsi bado sijakata tamaa kwenye ndoto zangu ila kwanza nilikua naangalia namna hata ya kupata basic needs kabla sijaanza kupanga mengineMdogo angu usikate tamaa, hata siku moja, amini bado unaweza na bado una uwezo wa kutimiza ndoto zako, jiami, wekeza katika kutimiza malengo yako. No matter how many times you will fail, believe in yourself and don't hesitate to start again. Everything in life happens according to our time, and for a reasons, labda haikuwa muda wako sahihi wa kutoboa lakini naiona kesho yako iliyojaa mafanikio, muhimu kutokukata tamaa. And Do not let anyone rush you with their timelines, still at the age of 25 you have a lot to accomplish. Enjoy the rest of the day and stay strong.
Ishu nilikata mtaji na kwenye production mm sikua mzalishaji ila nilitafuta watu wanaoweza kupiga kazi ambapo nilikua na cover cost zote za production so mda mwingi nilikua na deal kutafuta wateja na kuangalia ofisi isiyumbe na kwa jinsi gani nitajitanua niwafikie watu wengi zaidi so huwezi ukaanza mdogo mdogo bila kuwa na kianzio ikiwa saiv tu kupata mahitaji muhimu ni shidaKwa nini usirejelee production ukaanza mdogo mdogo
Shukrani bossPole asee,ila maisha yako hivyo
Nilichojifunza tatizo sio partnership ila biashara imefika katika hatua gan mpaka ufanye partnership kumbuka hakuna biashara kubwa utakayo weza kufanya ukiwa ww kama ww
Naichukua hiiMkuu wewe ni MWANAUME! Hela ina formula Moja, NJIA YAKE NI ILEILE! Kama mto wa msimu vile, unaweza kukauka ila siku mvua ikinyesha maji yatapita njia ile ile tu!
Nakuombea mvua inyeshe tena kwako Mkuu.
Bad times don't last forever. There is always another door, keep fighting mdogo wangu.
Mkuu juu huko umesema ulinunua hadi vitendea kazi, Kwahiyo vitendea kazi unavyo bado? Na vipi biashara kwa soko la ndani bado lipo vzr? au nasoko sio zuri kwa sasa?ishu nilikata mtaji na kwenye production mm sikua mzalishaji ila nilitafuta watu wanaoweza kupiga kazi ambapo nilikua na cover cost zote za production so mda mwingi nilikua na deal kutafuta wateja na kuangalia ofisi isiyumbe na kwa jinsi gani nitajitanua niwafikie watu wengi zaidi so huwezi ukaanza mdogo mdogo bila kuwa na kianzio ikiwa saiv tu kupata mahitaji muhimu ni shida
Sure mkuu kingine cha kuongezea ni bora kufanya kazi na mtu kwa malipo kuliko ile tufanye tukitoboa tunatoboa wote ni ngum sana kumpata mtu atakae ona maono yako na kuyaishi ili muweze kufika inapotakiwa la sivyo unaweza kupiga hesab ya watu wawili na mkapanga vizuri kumbe mwenzako amejishikiza tu kwako kwa mda ana hesabu zake kichwaniJibu zuri sana. Kosa la biashara nyingi za Kitanzania ni mtazamo kama wa huyo jamaa wa kwanza. Mtu anataka kila kitu afanye yeye anaishia kukwama. Anapata pressure sukari anakufa kwa madeni.
Angalizo unahitajika umakini sana kuchagua partner wa biashara. Usichague partner kwa sababu tu mmesoma wote, chagua partner kwa kuangalia wekness zako na strength za partner kwenye biashara yako, mkishirikiana mnatoka?
Vitendea kazi vipo niliuzaga mashine moja tu ila haiathir sana uzalishaji, soko la ndani lipo vizuri bado japo mm siku base sana na la ndan maana niliona ushindani mkubwa na huwa sipend competition so nilijikita na kutafuta nje zaidiMkuu juu huko umesema ulinunua hadi vitendea kazi, Kwahiyo vitendea kazi unavyo bado? Na vipi biashara kwa soko la ndani bado lipo vzr? au nasoko sio zuri kwa sasa?
Vitendea kazi vipo niliuzaga mashine moja tu ila haiathir sana uzalishaji, soko la ndani lipo vizuri bado japo mm siku base sana na la ndan maana niliona ushindani mkubwa na huwa sipend competition so nilijikita na kutafuta nje zaidi
Nakutumia mawasilaino yangu pm mkuu but basically ni mtaji na ntakupa raman nzima uone kuna fursa kiasi ganiKwa hiyo kwa sasa hivi ili wewe uamke tena mkuu unahitaji nini na nini? Kama hutojali tuwasiliane tuone kama tunaweza amka pamoja.