Jinsi nilivyofanikiwa kutengeneza Sh. Milioni 19.9 ndani ya siku 35 kwa kutumia Milioni 3.8

Afterthought 2:

Biashara na uchawi.

Kule nilivyoingia uziguani, wale wazee wa ofisini wakanitahadharisha siku ya kwanza tu - kijana kuwa makini sana, umejiandaa lakini?

Sikuelewa maana yake, ama either nilijifanya sijaelewa ili walieleza kiundani. Mzee m1 akaniita pembeni akanieleza. Akanitisha sana suala la uchawi, ushirikina, husda za watu, akaniambia inabidi nijilinde. Mimi nikamweleza wazi yule mzee kuwa siamini juu ya uwepo wa hivyo vitu, akasema kama mimi siamini basi nimpe yeye elfu 30 ataenda kujua jinsi gani atanilinda, bila mimi kuwa involved. Mimi kiukweli nilimgomeshea tukaachana, akasema nisubiri nijionee.

Nilivyoanza kazi nilifata protocols zote za utunzaji wa chombo, kila tukimaliza kazi tunapiga grease ya kutosha, nikanunua oil litre 40, kila baada ya heka 40 napiga chini oil, filter ya oil na diesel nabadilisha kila wiki. Yani sikutaka utani, mtu angeweza kusema vile ni vyombo vyangu japo nilivikodi.

Pale tulifanya kazi bila itilafu za nje ya technical issues, kuna kitu kilizingua nikamwita fundi kutoka Moro, hatukufanya kazi kwa siku 3, lakini lilikuwa tatizo la kiufundi.

Mchawi wa mafanikio ni umakini, kujituma na kuipenda kazi yako. Hakuna ndumba, unachoma tu pesa zako.
nimekukubali mkuu wajinga ndo waliwao
 
Uzi wa ukweli.. Kuna vijana wengine sana wamemaliza vyuo wako mtaani wanasubiri ajira za Magu bila mafanikio.
 
Ni kijana wa kitanzania ambaye napambana sana katika maisha haya ya kila siku, nashindwa kushea na wadau hapa kwakua ukileta uzi wa maendeleo utaitwa mwizi ni tapeli na kukatisha tamaa hata kwa wengine.

Watakaotaka kujifunza kutoka kwako nalisema hili kwa uzoefu mkubwa sana kwa baazi ya mabandiko ya maendeleo niliyoyasoma hapa kwa mfano kuna bandiko lipo hapa la huyu mdau ONTARIO.

Mimi pia natamani sana kushea nanyi napata uoga wa hali ya juu sana kwakua mtu kama huyo anaetaka kutupatia maarifa kupingwa kwa nguvu kubwa kiasi kile. Je mimi ninaetaka kushea nanyi jambo langu la kheri ni mafanikio makubwa sana. Na nisiejua kujieleza vizuri sana kama ONTARIO nitabakia salama.

Hongera sana kwa kushea nasi ONTARIO na wengine wengi.
 
Ndivyo hivyo kiongozi. Lakini kipimo reliable zaidi ni kupima kwa hatua. Ukichukua mita imekula kwako. Pia kuna njia nyingine ya kienyeji watu wa pwani wanaita 'Nzera/Nzela', yani kinakatwa kijiti, kisha mtu anapanua mikono (tuseme kama yesu msalabani) kisha hicho kijiti kinapitwa kuanzia mwanzo wa mkono mmoja hadi mwisho. Sasa nzera 35 ni heka 1. Pia ukitumia hii njia inakula kwako, tumia hatua ndio utaona faida.
ila dogo uwe makini na afya yako maana naona tb kwako ipo nje nje.unywe maziwa sana
 
Mkuu nimekuelewa saanaa,, Upo vizuri saanaa . Kwenye kilimo kuna PESA Sana binafsi na dil na zao la korosho Kusini, mwaka Jana nimepata pesa ambayo sikutarajia kabisa... Jins unavyosubiria wewe msimu wa mwenz wa 6-8 kirombero, sawa na Mimi navyosubiri mwenz wa 9-12 Kusini.
Viaz vikichanganyikiwa namm nitakuja kusini, niweke kwenye ratiba hii miez
 
Mkuu weka mambo hadharani tujifunze kitu, watu vichwa maji kila mahali wapo, uwepo wa watu hao ndiyo ambao unaingezea ladha ya jf
 
Back
Top Bottom