Jinsi nilivyoanza kuwa msomaji wa biblia

Jinsi nilivyoanza kuwa msomaji wa biblia

Baba Kabunyee

Member
Joined
Jul 30, 2024
Posts
11
Reaction score
14
KARATU, ARUSHA
Mwaka 1996,

Sikumbuki ilikuwa ni mwezi gani ila ninachokumbuka ilikuwa kwenye miezi ya kiangazi wakati kanisa la kisabato lilipoandaa mkutano mkubwa wa injili (effort) mjini Karatu mwaka 1996. Ninachokumbuka ni kuwa makanisa matatu ya kisabato yalishirikiana ambayo ni SDA Karatu, Arusha mjini kati na Burka. Kwa upande wangu ndo nilipoanza kuwafahamu wasabato kiundani. Nilikuwa nikiona watu wakienda kanisani hasa marafiki zangu wa shule ya msingi wakati huo ila sikuwa nachukulia serious. Kwa wakati ule nilikuwa naona kama makanisa ni matatu tu yaani RC, KKKT na TAG. Wengine niliona ni wasindikizaji.

Mhubiri mkuu alikuwa Mchungaji Geoffrey Mbwana akishirikiana na mchungaji Byceson Youze wa Karatu na Mchungaji Panga wa Arusha. Hawa wachungaji walikuwa wa moto mno na bado kwa wakati ule walikuwa bado damu ya moto kwa maana ya kuwa sio wazee. Jinsi walivyoichambua biblia ilikuwa sio kawaida. Ndo kwa mara ya kwanza maishani nilisikia ile kauli ya TUYACHUNGUZE MAANDIKO. Kwa wiki tatu Karatu ilisimama. Mimi kila nikitoka shule ilikuwa lazima nipitie uwanjani kusikiliza neno na kwaya. Kimsingi Karatu "ilitekwa". Nilishuhudia watu wengi walioshindikana kwa tabia mbaya kama ulevi wakibatizwa na kuwa watu wapya. Kwa kumbukumbu zangu ni kuwa ubatizo wa kwanza walibatizwa watu 113. Kwa mwaka 1996 ilikuwa ni watu wengi sana.

Kwa upande wa kwaya zilikuwepo kwaya ya Karatu, Nuru kwaya ya Mjini kati na Burka. Zote zilikuwa za moto mno. Bahati mbaya kwaya ya Karatu kwa wakati ule haikuwa na vyombo vya muziki. Pamoja na kutokuwa na vyombo kwaya ya Karatu ilikuwa inasismua sana kwasababu ya wananchi kuipa sapoti. Tulikuwa tunashangaa kumbe fulani akiwa kanisani kwao ni mwanakwaya 😂. Simon Gara, Ana Philmon, Philemon Amri, Peter Amri, Daudi Amri, Nafika Youze na wanakwaya wote mliokuwepo 1996 mbarikiwe sana. Dada Nafika na ile sauti yake ya pili alikua wa moto sana. Kwa ujinga wangu nilijiambia nikiwa mkubwa nitaoa mwanamke anayejua kuimba ili nifaidi nyimbo atakazoimba 😄. Sababu ilikuwa huyu Dada Nafika.

Burka ilikuwa nayo haishikiki kutokana na uwepo wa mama mchungaji Panga aliyekuwa na sauti yake ya kipekee. Yule mama sijui yuko wapi kwa sasa lakini alitisha sana na hatakaa asahaulike. Mara nyingi wakati mchungaji anatoa wito wa watu kuja mbele na kuyakabidhi maisha yao kwa Yesu basi Burka choir walikuwa wakiimba wimbo wao wa "Mbona unasitasita kuja kwa Yesu".. nadhani lilikuwa ni jukumu lao maalum. Mtu mwingine ninayemkumbuka kwenye kwaya ya Burka anaitwa Zawadi. Yule jamaa nadhani hadi leo hii yuko Burka. Miaka michache iliyopita nilimwona pale Burka.

Nuru choir nayo ilikuwa funga kazi. Walikuwa wakiongozwa na dada mmoja aa kiiraqw ambaye jina lake limenitoka. Sauti ya yule dada ilikuwa inaweza kusikika kilometa kadhaa. Kivutio kingine kilikuwa ni wapiga vyombo wa Nuru choir. Shukrani sana kwa jamaa mpiga gitaa anayeitwa Rama. Nuru walikuwa wana wimbo wao unaitwa AKUITA NJOO ila ulikuwa pia kwa kimasai na kipare. Kimsingi hadi leo hii nazitafuta zile albamu za kwaya ya Nuru na Burka za miaka hiyo. Bado nazikumbuka baadhi.

Binafsi ile effort ilinisaidia kujua kitabu kiitwacho Biblia. Nakumbuka baada ya ule mkutano nikawa msomaji mashuhuri wa biblia. Hata madarasa mengi sana ya biblia nilihudhuria pale kanisa la Sumawe. Kuna wakati walikuwa wana darasa linaitwa darasa la waberoya. Shukrani kwa Pastor Youze na Pastor Lomai. Ile effort iliacha kumbukumbu nzuri za kuvutia kwenye mioyo ya wanakaratu.
 
Umebarikiwa sana mwana wa Mungu aliye hai🙏
 
Back
Top Bottom