Jinsi nchi masikini zinavyotajirisha nchi tajiri

Princemwalejr

JF-Expert Member
Nov 9, 2017
496
500
Mwaka 2012 nchi zinazoendelea zilipokea dola trilion 1.3 za misaada, vitega uchumi. Lakini mwaka huo huo nchi hizo zilitoa dola trilioni 3.3 kwenda kwenye nchi zilizoendelea. Kwa maana nyingine nchi masikini zilizipa nchi tajiri dola trilion 2 kwa mwaka huo. Kuanzia mwaka 1980 kiasi cha dola trilion 16.3 zimetolewa kutoka kutoka kwa nchi masikini kwenda nchi tajiri. Katika hizo trilion 16.3 kiasi cha dola trilion 4.2 zimetolewa kulipia riba za madeni.

Kitu kingine kinachohamisha fedha kutoka nchi masikini ni kipato wanachokipata wawekezaji na kukihamishia kwao. Fikiria faida wanayopata BP kwenye uchimbaji wa mafuta Nigeria. Fikiria faida wanayoipata Anglo-Ameican kwenye uchimbaji wa madini Afrika ya kusini.

Tukiacha hayo kuna fedha zinazochukuliwa kwa wizi. Mashirika na makampuni makubwa huandika bei za uongo kwenye risiti ili kukwepa kodi (trade misinvoicing). Na pia wizi huu hutumika kutorosha fedha chafu (money laundering). Mashirika haya yanaweza kukwepa kodi kwa kuhamisha fedha zao kwenye matawi ya kampuni zao yaliyopo nje ya nchi.

Fedha zinazotolewa kutoka nchi zinazoendelea ni zaidi ya mara 24 ya fedha zinazoingizwa kwa misaada. Hii ina maana kwa kila dola moja ya msaada nchi zinazoendelea zinapoteza dola 24 kwenye mzunguko wa fedha zinazotoka nje.

Unyonyaji huu wa fedha kwa kiwango kikubwa unakwamisha maendeleo ya nchi zinazoendelea. Kwa kifupi nchi zinazoendelea zinazitajirisha nchi zilizoendelea.

Makampuni yanayodanganya kwenye risiti yangeweza kukamatwa kwenye ukaguzi wa forodha (customs) lakini World Trade Organization imetoa muongozo risiti zisichunguzwe uhalali wake kwa madai kuwa kufanya hivyo kunazorotesha biashara.

Nchi zinazoongoza kutoa misaada pia zinaongoza kwa kuwa na “tax havens” ambazo zinatumika kama maficho ya kukwepea kodi kwa fedha zilizoingizwa kutoka nje nchi. Suala la misaada linawafanya wachukuaji kuonekana watoaji.

Nchi masikini hazihitaji misaada zinahitaji haki. Nchi tajiri zingeweza kusamehe madeni ya nchi masikini. Hii ingewezesha nchi masikini kuwa na fedha za kufanyia maendeleo badala ya kulipa madeni ya zamani. Nchi tajiri zingeweza kufunga vyombo vya siri vinavyotumika kukewepea kodi za nchi masikini, zingeweza kutoa adhabu kali kwa mabenki na wahasibu wanaosaidia utoroshwaji wa fedha kutoka nchi maskini. Mashirika ya kimataifa duniani kote yangeweza kuwekewa angalau kiwango cha chini cha kulipa kodi ili yapunguze kukwepa kulipa kodi.

Aid in reverse: how poor countries develop rich countries | Jason Hickel

Ufumbuzi wa matatizo haya unajulikana lakini nchi zinazoendelea hazitachukua hatua za kuzikomboa nchi maskini. Mwewe halaumiwi akila kuku. Akale wapi? Ni juu yetu sisi tunaodhulumiwa kuamka na kuchukua hatua za kukomesha unyonyaji huu.
 

JOHNKEKE

JF-Expert Member
Mar 30, 2011
1,071
2,000
Yes ni kweli. Ndiyo mana wako wanaoamini kwenye fair trade, NOT aid.
Sababu misaada mara zote inaambatana na conditions za kupelekea kuinyonya zaidi Africa.
 

KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
15,642
2,000
dah! my Afrika!!
umaskini wetu upo vichwani,tunajididimiza na kudidimizwa tusikatae tukiitwa bara la giza. na ndo kwanza tunapata viongozi wabaya kwa juhudi za wazee wetu kupambana na ukoloni zilizua matumaini sasa je juhudi za kupambana na ukoloni mamboleo zitazua matumaini..?
umaskini afrika
rushwa afrika
matumizi mabaya ya madaraka afrika
magonjwa afrika
makundi ya kiasi na kigaidi afrika
vita afrika
njaa afrika
uduni na ujinga afrika!

mkia unatuhusu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom