Samwely kisinga
Member
- Mar 22, 2018
- 12
- 26
JINSI MITI INAVYOKAUSHA MTO RUVUMA.
Jumamosi hii imekuwa ngumu sana kwangu.Nimepata shida sana kuwaeleza na wakaelewa marafiki wa mazingira wa shirika la Tdeso we care,ambao tulikuwa tunawapa mafunzo ya uhifadhi wa mazingira.
Ugumu nilioupata unatokana na dhana ya wengi kujua kila mti unaweza kupandwa popote na ukawa Rafiki Kwa mazingira,hivyo nilivyowaambia mto ruvuma unakaushwa na miti,walianza kunongona na kupelekea ukumbi kupoteza mwelekeo Kwa muda,ila nashukuru MUNGU mwisho walinielewa na kunishukuru pia.
Miti ni muhimu sana Kwa uhai wetu,na ina mchango mkubwa sana kuhakikisha mazingira yanakuwa salama.Lakini pamoja na umuhimu wake,miti hii ikipandwa bila kufata utaratibu inakuwa hatari sana.kwani inakuwa haisaidii mazingira bali inayaharibu.Si kila mti au mmea unaweza kupandwa popote.
Kupungua maji Kwa MTO ruvuma ambao ni tegemeo kubwa Kwa wakazi wa mkoa huu ,Kwa kiasi kikubwa kunatokana na kitendo cha serikali ya awamu ya kwanza kungoa miti asili kwenye milima ya matogoro na kupanda miti ya kigeni ya mikaratusi ambayo inanyonya maji sana.
Kitendo cha kungoa miti ya asili kwenye milima ya matogoro ambayo ndio chanzo cha MTO huu ,kilikuwa ni kosa kubwa sana.
Kwa mujibu wa Mzee josephat Komba,mkulima katika kijiji cha ndirima litembo,aliyehojiwa na gazeti la mwananchi la tarehe 1/3 mwaka 2012 ,anasema kipindi cha nyuma MTO huo ulikuwa unafurika maji hadi kiangazi,lakini sasa hata kifuku hayajai.
Lengo la makala hii si kuwalaumu wale waliosababisha hilo,kwani nafahamu jitihada kubwa zinazofanywa kuhakikisha MTO ruvuma unarudi kwenye hali yake.
Lengo la makala hii ni kuwaomba wadau wote wa mazingira,hasa wakati huu ambao tunaelekea mwezi wa kwanza ,mwezi ambao Kwa taifa letu ni mwezi wa kupanda miti,ni vizuri Kwa pamoja tukatoa Elimu ya kutosha juu miti gani ni mizuri kupanda na ipandwe wapi.
Samwely Kisinga.
E.A
Tdeso we care
0744408606