el nino
JF-Expert Member
- Nov 5, 2013
- 4,712
- 5,064
MUZIKI ni biashara kubwa sana katika karne hii ya 21 ambapo tumeshuhudia vijana wadogo wakitajirika kwa namna ya ajabu. MUZIKI umefanikiwa kukamata nyanja mbali mbali za uchumi, kupitia biashara ya muziki vitu kama vinywaji, nguo na bidhaa nyingine zimekuwa zikiuzwa sana kutokana na kuwa promoted na muziki.
Biashara ya Muziki imeambatana na uongo na ujanjaujanja mwingi ambao watu wengi hawaufahamu kutokana na namna biashara hii inapambwa kupitia video za muziki, mitandao pamoja na vyombo vya habari.
Mnamo mwaka 2002, mwanamuziki mkongwe na Mfalme wa muziki wa Pop (marehemu)"Michael Joseph Jackson" aliwalipua vibaya kampuni ya Sony Music, Kampuni inayomsimamia katika shughuli za muziki. MJ aliielezea jinsi siri za Sony Music na fitna walizomfanyia kwa makusudi kabisa walikataa kupromote album yake iliyojulikana kwa jina la "invincible" kwa kuwa MJ alikataa katukatu kuzunguka kuipromote album hiyo (kufanya music tour USA) kwa sababu kuwa Sony walifanya fitna kuhakikisha MJ anapata masilahi madogo kutoka kwenye mauzo ya kazi zake kwa kushirikiana na wakili wa MJ walihakikisha vipengele vya mikataba vinamkaba MJ kinyume na matakwa yake.
MJ alilipua kwa kuweka bayana kuwa wasanii wengi wakubwa nchini marekani hufariki wakiwa na stress kutokana na ujanja na fitna zinazofanywa na Music Labels zinazowasimamia kiasi cha kuwaacha wasanii hao wakiwa maskini na wamefulia, inafahamika kwamba utofauti wa MJ na wasanii wengine wengi ni kuwa licha ya ubora wake katika muziki alikuwa bora sana kwenye biashara ya muziki hii ilipekea MJ mwanamuziki aliyefanikiwa zaidi kwenye biashara ya muziki kwa kulamba mikataba minono na kumiliki haki zake kwenye mikataba.
SONY MUSIC na makampuni mengine makubwa nchini USA hawakupenda namna Michael Jackson alikuwa akiwapiga chenga kwenye mikataba yao ya kinyonyaji kwa kuwa alikuwa ananufaika kushinda kampuni husika tofauti na wasanii wengine ambao ukiwaangalia kwenye video zao wanavyotumia mahela , pombe, magari na wanawake utahisi wanaingiza kiasi kikubwa cha fedha kumbe kiasi kikubwa kinachukuliwa na makampuni makubwa ya muziki ambayo yamejificha nyuma ya wasanii hao......
Namna pekee iliyobakia ilikuwa ni kuhakikisha MJ anashushwa kimuziki kwa gharama yeyote ile, kwa maana kwamba MJ akishuka kimuziki hatakuwa na uwezo wa kubargain wenye mikataba vilevile SONY MUSIC walikuwa wakifukuzia catalog( ni kama hatimiliki) ya kazi zote za MICHAEL JACKSON (CATALOG YA MJ ina thamani zaidi ya mwanamuziki yeyote aliyewahi kuishi chini ya jua)hivyo basi kupitia kufinance kashfa za uongo kama kubaka watoto, kuacha kupromote album zake na kuwekeza zaidi kwa wasanii wachanga ambao ni replica ya MJ SONY MUSIC walikuwa wapo mbioni kufanikisha adhma yao ovu.
Mpaka kufikia mwaka 2002, dunia ilikuwa imefichwa kilichokuwa kinafanyika nyuma ya pazia, kumbe muziki sio tuu biashara ambayo tunaiona ipo fair na inafanyika based on talent, kuna mambo mengi sana yapo nyuma ya biashara ya muziki na wasanii wengi ni watumwa wa haya makampuni ya kinyonyaji, angalia msanii mwenye talent kama chriss brown au drake, kwa uwezo na soko la kazi zao kiasi wanachoingiza ni kidogo sana tofauti na kinachokwapuliwa na haya makampuni, unaweza ukawaona wanaendesha ferrari na magari mengine ya kifahari lakini ujue kuwa kiasi kikubwa kinachukuliwa na makampuni na wakati mwingine vitu hivyo wanakopeshwa kwa kusaini mikataba ya maisha kuyatumikia makampuni haya.
Kimsingi muziki wa sasa huko USA haujali sana kipaji , bali ni nani yupo nyuma yako (kampuni ipi ipo nyuma yako), nadhani wote ni mashahidi kwenye gramy za mwaka huu 2019) tumeona ajabu la mwaka kwa cardy b kushinda best rap album wakati kimsingi album ya rap iliyopeform zaidi mwaka 2018 ni album ya drake ambayo haikuwemo kabisa kwenye hiyo category!!
Ili uweze kuendelea kuwa juu ni lazima ukubali kulaliwa na makampuni haya, huku kwetu Tz biashara ya muziki inakuwa kwa kasi, soon and very soon tutaanza kusikia vilio kutoka kwa wasanii wetu, kutokana na ujanja wa makampuni haya ambayo yanahakikisha yanamiliki haki zote za mwanamuziki kwa njia yeyote ile.