Umetumia nguvu kubwa kuandika ujumbe wako,Ibara ya 30 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano inaongelea mipaka kwa Haki na Uhuru.
Chadema wanakuwa wanaongea sana huku Katiba ikiwaumbua wazi wazi.
Tuanze sasa:-
30.-(1) Haki na uhuru wa binadamu ambavyo misingi yake
imeorodheshwa katika Katiba hii havitatumiwa na mtu mmoja
kwa maana ambayo itasababisha kuingiliwa kati au kukatizwa
kwa haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma.
(2) Ifahamike kwamba masharti yaliyomo katika Sehemu hii
ya Katiba hii, yanayofafanua misingi ya haki, uhuru na wajibu wa
binadamu, hayaharamishi sheria yoyote iliyotungwa wala kuzuia
sheria yoyote kutungwa au jambo lolote halali kufanywa kwa
mujibu wa sheria hiyo, kwa ajili ya -
(a) kuhakikisha kwamba haki na uhuru wa watu wengine
au maslahi ya umma haviathiriwi na matumizi
mabaya ya uhuru na haki za watu binafsi;
(b) kuhakikisha ulinzi, usalama wa jamii, amani katika
jamii, maadili ya jamii, afya ya jamii, mipango ya
maendeleo ya miji na vijiji, ukuzaji na matumizi ya
madini au ukuzaji na uendelezaji wa mali au maslahi
mengineyo yoyote kwa nia ya kukuza manufaa ya
umma;
(c) kuhakikisha utekelezaji wa hukumu au amri ya
mahakama iliyotolewa katika shauri lolote la madai
au la jinai;
(d) kulinda sifa, haki na uhuru wa watu wengine au
maisha binafsi ya watu wanaohusika katika mashauri
mahakamani, kuzuia kutoa habari za siri; kutunza
heshima, mamlaka na uhuru wa mahakama;
(e) kuweka vizuizi, kusimamia na kudhibiti uanzishaji,
uendeshaji na shughuli za vyama na mashirika ya
watu binafsi nchini; au
(f) kuwezesha jambo jingine lolote kufanyika ambalo
linastawisha au kuhifadhi maslahi ya taifa kwa jumla.
(3) Mtu yeyote anayedai kuwa sharti lolote katika Sehemu hii
ya Sura hii au katika sheria yoyote inayohusu haki yake au
wajibu kwake, limevunjwa, linavunjwa au inaelekea litavunjwa na
mtu yeyote popote katika Jamhuri ya Muungano, anaweza
kufungua shauri katika Mahakama Kuu.
Hapo kwenye bold.
Hapa ni elimu tu. Ili mkipata mkong'oto msisingizie katiba kuvunjwa.Umetumia nguvu kubwa kuandika huo ujumbe wako lakini ukichoandika ni pu.... mba plus.
Sasa hapo Chadema wameadhirika Wapi?
Anayeisigina Katiba anafahamika, lakini kwa bahati mbaya watu wengi wagamgwaya......
Inaelekea hizi post za mfululizo za kuishambulia Chadema bila hoja zenye mashiko ni kuonyesha kuweweseka kwa watawala kutokana na vuguvugu la operesheni Ukuta.
Acha kuingilia fani za wana sheriaIbara ya 30 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano inaongelea mipaka kwa Haki na Uhuru.
Chadema wanakuwa wanaongea sana huku Katiba ikiwaumbua wazi wazi.
Tuanze sasa:-
30.-(1) Haki na uhuru wa binadamu ambavyo misingi yake
imeorodheshwa katika Katiba hii havitatumiwa na mtu mmoja
kwa maana ambayo itasababisha kuingiliwa kati au kukatizwa
kwa haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma.
(2) Ifahamike kwamba masharti yaliyomo katika Sehemu hii
ya Katiba hii, yanayofafanua misingi ya haki, uhuru na wajibu wa
binadamu, hayaharamishi sheria yoyote iliyotungwa wala kuzuia
sheria yoyote kutungwa au jambo lolote halali kufanywa kwa
mujibu wa sheria hiyo, kwa ajili ya -
(a) kuhakikisha kwamba haki na uhuru wa watu wengine
au maslahi ya umma haviathiriwi na matumizi
mabaya ya uhuru na haki za watu binafsi;
(b) kuhakikisha ulinzi, usalama wa jamii, amani katika
jamii, maadili ya jamii, afya ya jamii, mipango ya
maendeleo ya miji na vijiji, ukuzaji na matumizi ya
madini au ukuzaji na uendelezaji wa mali au maslahi
mengineyo yoyote kwa nia ya kukuza manufaa ya
umma;
(c) kuhakikisha utekelezaji wa hukumu au amri ya
mahakama iliyotolewa katika shauri lolote la madai
au la jinai;
(d) kulinda sifa, haki na uhuru wa watu wengine au
maisha binafsi ya watu wanaohusika katika mashauri
mahakamani, kuzuia kutoa habari za siri; kutunza
heshima, mamlaka na uhuru wa mahakama;
(e) kuweka vizuizi, kusimamia na kudhibiti uanzishaji,
uendeshaji na shughuli za vyama na mashirika ya
watu binafsi nchini; au
(f) kuwezesha jambo jingine lolote kufanyika ambalo
linastawisha au kuhifadhi maslahi ya taifa kwa jumla.
(3) Mtu yeyote anayedai kuwa sharti lolote katika Sehemu hii
ya Sura hii au katika sheria yoyote inayohusu haki yake au
wajibu kwake, limevunjwa, linavunjwa au inaelekea litavunjwa na
mtu yeyote popote katika Jamhuri ya Muungano, anaweza
kufungua shauri katika Mahakama Kuu.
Hapo kwenye bold.
Katiba ya chadema haitambui mahakama,kwa hiyo kifungu hicho kwa mujibu wa katiba ya chadema,hakifai kuheshimiwaHiyo hiyo ibara ya 30:
(4) Bila ya kuathiri masharti mengineyo yaliyomo katika
Katiba hii, Mahakama Kuu itakuwa na mamlaka ya kusikiliza kwa
mara ya kwanza na kuamua shauri lolote lililoletwa mbele yake
kwa kufuata ibara hii; na Mamlaka ya Nchi yaweza kuweka
sheria kwa ajili ya-
(a) kusimamia utaratibu wa kufungua mashauri kwa
mujibu wa ibara hii;
(b) kufafanua uwezo wa Mahakama Kuu katika kusikiliza
mashauri yaliyofunguliwa chini ya ibara hii;
(c) kuhakikisha utekelezaji bora wa madaraka ya
Mahakama Kuu, hifadhi na kutilia nguvu haki, uhuru
na wajibu kwa mujibu wa Katiba hii.
(5) Endapo katika shauri lolote inadaiwa kwamba sheria
yoyote iliyotungwa au hatua yoyote iliyochukuliwa na Serikali au
mamlaka nyingine inafuta au inakatiza haki, uhuru na wajibu
muhimu zitokanazo na ibara ya 12 hadi 29 za Katiba hii, na
Mahakama Kuu inaridhika kwamba sheria au hatua inayohusika,
kwa kiwango inachopingana na Katiba ni batili au kinyume cha
Katiba basi Mahakama Kuu ikiona kuwa yafaa au hali au masilahi
ya jamii yahitaji hivyo, badala ya kutamka kuwa sheria au hatua
hiyo ni batili, itakuwa na uwezo wa kuamua kutoa fursa kwa ajili
ya Serikali au mamlaka nyingine yoyote inayohusika kurekebisha
hitilafu iliyopo katika sheria inayotuhumiwa au hatua inayohusika
katika muda na kwa jinsi itakavyotajwa na Mahakama Kuu, na
sheria hiyo au hatua inayohusika itaendelea kuhesabiwa kuwa ni
halali hadi ama marekebisho yatakapofanywa au muda
uliowekwa na Mahakama Kuu utakapokwisha, mradi muda mfupi
zaidi ndio uzingatiwe.
Sasa wewe uliyoisoma mara nyingi hebu toa tafsiri ya vifungu nilivyovitaja.Mimi naona mtoa post ndo mara yake ya kwanza kuisoma katiba kwa hy alipoona hapo tena bila kujua tafsiri ya kisheria akakimbilia Jf. Soma tena alafu urudi humu
Bro, claw back clause ndo kama hizo alizokutajia mleta Mada, mfano Article 30, hiyo ni claw back clause, ambayo imeweka limitations on the enjoyment of the rights provided under part 3, mbona Lissu hawambii hili, anawaambia tu mna haki, hawaambii kama mnawajibu pia!Annaeli unajua "Doctrine of claw back"?
Hiki chama mnachoabudu kimewaharibu to the root!
hapo ni kama sheria inaongelea mtu binafsi.naomba uniwekee sheria za vyama vya siasa pamoja na katiba inasemaje?Madaraka ya Pekee ya Mamlaka ya Nchi
31.-(1) Mbali na masharti ya ibara ya 30(2), sheria yoyote
iliyotungwa na Bunge haitakuwa haramu kwa sababu tu kwamba
inawezesha hatua kuchukuliwa wakati wa hali ya hatari, au
wakati wa hali ya kawaida kwa watu wanaoaminika kuwa
wanafanya vitendo vinavyohatarisha au kudhuru usalama wa
taifa, ambazo zinakiuka masharti ya ibara ya 14 na ya 15 za
Katiba hii.
(2) Ni marufuku kwa hatua zilizotajwa katika ibara ndogo ya
(1) ya ibara hii kuchukuliwa kwa mujibu wa sheria yoyote wakati
wa hali ya hatari, au wakati wa hali ya kawaida kwa mtu yeyote,
isipokuwa tu kwa kiasi ambacho ni lazima na halali kwa ajili ya
kushughulikia hali iliyopo wakati wa hali ya hatari au wakati wa
hali ya kawaida kushughulikia hali iliyosababishwa na mwenendo
wa mtu anayehusika.
(3) Ifahamike kwamba masharti yaliyomo katika ibara hii
hayataidhinisha mtu kunyang'anywa haki yake ya kuwa hai
isipokuwa tu kwa kifo kama matokeo ya vitendo vya kivita.
Note sentence ya kwanza kabisa inayosema bila kuathiri.....Mamlaka ya Rais
148.-(1) Bila ya kuathiri masharti yatakayowekwa na sheria
yoyote iliyotungwa na Bunge, miongoni mwa madaraka ya Rais
akiwa kama Amiri Jeshi Mkuu ni kuyaamuru majeshi ya nchi
yatende mambo yanayohusika na vita vya ulinzi wa Jamhuri ya
Muungano, mambo ya kuokoa maisha na mali ya watu katika
hali ya hatari na mambo mengineyo ambayo Amiri Jeshi Mkuu
ataona yahitajika, na kwa ajili hiyo Amiri Jeshi Mkuu aweza
kuyaamuru hayo majeshi yatende mambo hayo ama ndani au
nje ya Tanzania.