Jinsi Kampuni za Simu zinavyowaibia wateja wao!

Imefikia wakati napiga simu customer care..akipokea anajitambulisha...nachukua jina lake alafu nakata simu. Naanza kumpekua mitandaoni nikimfahamu namfuatilia.....ngoja niishie hapo. Ila hili jukumu nilianza baada ya kuona watoa huduma wengi wanavikauli vibaya pindi nipigapo simu...yaani naibiwa alafu napewa na maneno ya kejeli.....ngoja ninawe maji nitoe povu....ila hao one day watakufa
 
Wakuu ni takribani miaka 4 iliyopita tangu nianzishe uzi huu lakini mpaka leo TCRA hawajachukua hatua zozote kuwaadhibu hawa wezi wanaowaibia wananchi kila kukicha.

Takribani miezi 3 iliyopita mtakuwa mmegundua kwamba Vodacom Tanzania nao wameanza wizi kwenye bundles kama ilivyo kwa Halotel. Niliwakimbia Halotel nikahamia huku Vodacom lakini sasa naona ni afadhali nirudi Halotel kwa kuwa wizi wa Halotel unaonekana sio mkali sana kama huu wa Vodacom.

Kama mtakuwa wafuatiliaji wazuri, hasa wale wateja wa kudumu wa Vodacom, bila shaka mtakuwa mmegundua kuisha kwa bundle kusikokuwa kwa kawaida. Zamani nilikuwa nikinunua GB 2 za vodacom na kuzitumia kwa wiki nzima....nikidowload YouTube, kutazama TV, na kuperuzi mambo kibao...na bado chenji inabaki. Sasa hivi bundle hili huisha ndani ya siku moja na kama litadumu sana basi huchukua siku 2 tu (wakati matumizi ni yaleyale ya zamani).

Hii tasfiri yake ni nini? Tafsiri yake ni kwamba huu ni wizi wa mchana kweupe. Kuna uwezekanao mkubwa kwamba zile GB tunazopewa ni kanyaboya...ni maandishi tu lakini kiuhalisia unaweza ukute umepewa MB 100 tu! Tunaomba serikali iingilie kati wizi huu, otherwise wananchi tutaendelea kuibiwa na hawa makaburu hadi Yesu atakaporudi.

Nawasilisha.
 
Wakuu wizi mwingine huu hapa:

Rais Magufuli nakuomba uwashughulikie wahujumu uchumi hawa hapa!

Wakati kesi inayowakabili mabosi wa Haloteli kwa kutakatisha fedha na kuhujumu uchumi ikiwa haijafika tamati, kampuni hii ya simu imeanza tena wizi na utapeli kwa wateja wake. Nasema hili kwa kuwa mimi ni mteja wao na nina kipande cha ushahidi (a piece of evidence) na maelezo ya kutosha kuthibitisha haya ninayoyasema.

Mimi ninatumia data za Halotel kwenye modemu kwa takribani miaka mitano sasa. Hili neno “takribani|” naomba ulibold na kupigia mstari kwa kuwa hapa ndipo wizi wa Haloteli unapoanzia. Wakati naanza kutumia data za haloteli, mara kwa mara nilikuwa naambiwa kisi cha MB zilizobaki na muda zitakapoisha. Nilikuwa natumia meseji za kunikumbusha, hasa bando inapokaribia kuisha. Baada ya kuanza mchakato na hatimaye utekelezaji wa wizi wa bando za wateja, siku hizi hawatumi meseji tena. Wanachofanya ni kutuma meseji moja tu yenye utata na wizi ndani yake kama inavyoonekana hapo chini:



Mtu mwenye akili timilifu ukisoma hii meseji unaona kabisa ina wizi ndani yake kwa 100%. Kwanza imeandikwa kwa mafumbo na haionyeshi uhalisia wowote wa data zilizotumika na jinsi matumizi hayo yalivyofanyika. Twende taratibu. Mimi huwa nanunua bando ya Tsh 1500 yenye ujazo wa 1524 MB. Sasa tuje kwenye hiyo percentage yao. 90% ya 1524 MB = 1371.6 MB. Hii ina maana kuwa baada ya kutumia 1371.6 (90%) ya data kiasi kinachobaki ni 1524 - 1371.6 = 152.4 MB. Sasa tazama upya meseji yao kwennye kielelezo hapo juu. Kiasi cha data kinachotakiwa kubaki baada ya kutumia 90% ni 152.4 MB lakini wao wanasema ni 45 MB! Wezi wakubwa! Hapa wananipiga 152.4 MB - 45MB = 107.4 MB kwa mkupuo mmoja! Ina maana nikinunua bando ya Tsh 15000, kwa mfano, napigwa 10.74 GB. Huu ni wizi mchana kweupe pee!

Na kibaya zaidi, hii meseji inatumwa mwishoni kabisa. Kama sio wezi kwanini wasitume meseji kila ninapotumia labda 100 MB, kwa mfano? Na kwanini saliola data kwa mfumo wa asilimia? Je, ni wananchi wangapi wanaoweza kukokotoa hiyo asilimia? Kwa ujumla hawa jamaa ni wahuni, matapeli, na wezi wakubwa!

Aidha, kwenye meseji yao wanasema nimetumia takribani 90% ya kifurushi. Maana yake ni kuwa hata wao wenyewe hawana uhakika na kifurushi kilichobaki. Kama hawana uhakika mimi nitawaaminije? Hii ni sawa na kumpa shetani amlee mwanao. Ujanjaujanja na wizi wa aina hii haukubaliki hata kidogo hapa nchini Tanzania. Ikiwa sisi wananchi tunaibiwa kiasi hiki, je TRA wanaibiwa mapato kiasi gani?

Natoa wito kwa serikali, kupitia TCRA na TRA kuwachunguza Halotel ili kubaini kiasi cha fedha walizoiba tangu waanze wizi huu na kuwaamrisha wazirejeshe hazina pamoja na kuchukuliwa hatua kali za uhujumu uchumi haraka iwezekanavyo. Hatuwezi kukubali kuwafuga wezi, matapeli, na wahujumu uchumi wakati serikali haina fedha za kuleta maendeleo ya wananchi.

Nawasilisha.
 
Sasa hivi vifurushi vya mchongo ambavyo Nape na genge lake wameamua kuvifumbia mambo vitatuumiza aisee!!😱🙄😳🙄
 
Sasa hivi wamekuja na mtindo wa kukaa wote meza moja kupanga bei za vifurushi zinazofanana ili kuwabana wateja wakose mahali pa kukimbilia wakamuliwe vizuri. Mungu anawaona.
 
Hawa HALOTEL ni majizi wa kutupwa. Mkumbuke pia mkurugenzi wa Halotel aliwahikukamatwa na serikali kwa shu ya utapeli. Ikiwa anaweza kuitapeli serikali atashindwaje kutapeli wateja?
 
Hivi huu wizi unaofanywa na tiGO na Halotel utakoma lini katika nchi hii ya kusadikika? Inauma sana.
 
Tpaulo@ mimi najua kuwa wewe ulifurushwa kazini ila huku Jf unadanganya ! Yafaa nini?
 
Tpaulo@ mimi najua kuwa wewe ulifurushwa kazini ila huku Jf unadanganya ! Yafaa nini?
1. kufurushwa kazini kuna uhusiano gani na hoja inayohusu wizi wa kampuni za simu?
2. Kama nasema uongo nipinge kwa hoja sio kwa porojo. Hoja haipigwi rungu bali hupingwa kwa hoja iliyo bora/kweli zaidi (JK, 2020)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…