Jinsi CCM inavyoua vipaji na ajira za watu

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
25,138
Reaction score
48,364
CCM ni chama ambacho kimekuwa kinaua vipaji na ajira za watu kila uchwao na uchao.

Maelfu ya watanzania ajira zao au vipaji vyao vimeuawa na CCM ama kwa kuiunga mkono au kuipinga.

Nani anakumbuka zama zile za TMK wanaume na kundi la vichekesho la Zekomedi walipokuwa kama ndiyo alama ya sanaa Tanzania.

Hao jamaa waliposhiriki Kampeni za CCM mwaka 2010 ndiyo ukawa mwanzo wa kupoteza muelekeo. Hata msanii Marlaw aliwahi kusema kupotea kwake kimuziki kulitokana na yeye kuruhusu nyimbo zake kutumika na CCM kwenye Kampeni zao mwaka 2010.

Orodha ni ndefu lakini isemwe tu wasanii wengi wamepoteza wafuasi wao kisa walikubali kutumiwa na CCM kwa namna Moja ama nyingine.

Lakini vyombo vya habari Tanzania kwa Kasi ya ajabu vimepoteza watu wanaovifuatilia kwa kuwa watanzania wameamini hivyo vyombo vinatumiwa na CCM kama zana kuisadia kubaki madarakani.

Hizo ni ajira zinazouawa na CCM kisa yenyewe iendelee kubaki madarakani.
 
Hata Waandishi wa habari pia hawako huru. Uminywaji umekuwa mkubwa kiasi wanashindwa kuwa wabunifu. Sidhani kama tutazalisha wakina Kikeke wengine kwa miaka hii.

CCM imeshikilia Mateka sekta nyingi sana asee. Kwa akili ya kawaida tu unahisi Simba na Yanga hazikupenda kuombeleza maisha ya Watanzania waliouwawa October 29?

Kwa kila siku ambayo CCM itaendelea kuwa madarakani maisha kiujumla, ubunifu, uzalishaji, sanaa itaendelea kuwa ya wasiwasi hivi hivi.
 
CCM ni chama ambacho kimekuwa kinaua vipaji na ajira za watu kila uchwao na uchao.

Maelfu ya watanzania ajira zao au vipaji vyao vimeuawa na CCM ama kwa kuiunga mkono au kuipinga.

Nani anakumbuka zama zile za TMK wanaume na kundi la vichekesho la Zekomedi walipokuwa kama ndiyo alama ya sanaa Tanzania.

Hao jamaa walipishiriki Kampeni za CCM mwaka 2010 ndiyo ukawa mwanzo wa kupoteza muelekeo. Hata msanii Marlaw aliwahi kusema kupotea kwake kimuziki kulitokana na yeye kuruhusu nyimbo zake kutumika na CCM kwenye Kampeni zao mwaka 2010.

Magazeti ndo yamekufa kabisa, haya yalikuwa yanatoa ajira kubwa sana kwa vijana mijini. Kampuni za magazeti kwanza zilikuwa zinaajiri waandishi wengi, pia zilikuwa na correspondance lukuki kila kona ya nchi, kulikuwa na idara za usambazi magazeti, nazo zlikuwa zinaajiri vijana kibao na mawakala kila kona ya nchi halafu walikuwepo vendors wa mitaani kibao. Bado watu wa matangazo na masoko.
Ingawa kuna athari ya mitandao kupunguza soko la magezeti, lakini kwa kiasi kikubwa CCM imechangia kwa kiasi kikubwa kuua magazeti nchini. Kwanza imeyalazimisha magazeti kuandika habari za ccm ambazo hazina mvuto hata kwa wanachama wao wenyewe, pili chama kimewageuza wandishi kuwa machawa matokeo yake watu hawataki kuyaona hayo magazeti yao.
Unaua kiwanda cha magazeti chenye uwezo wa kuwaingiza vijana zaidi ya laki moja kwenye ajira rasmi na zisizo rasmi halafu unaanza kuhangaika na uwekezaji unaotoa ajira elfu moja! Hivyo ndivyo chama kinavyoua ajira nchi kwa kuangalia maslahi yao ya kutawala badala ya maslahi ya nchi.
 
Kituo kinachofuata ni ajira ccm na yenyewe kukata roho!
 
Aione Pascal Mayalla kwenye jalada.
 
Pascal Mayalla Kuna siku alikuwa anahojiwa mahali akasema alitaka kurudisha kipindi kama cha "kitimoto" ya zama zile lakini ilishindikana.

Kwa maelezo yake mwenyewe anadai hakuna kituo Cha televisheni kilichokubali muswada wake wa kuanzisha kipindi kama kile. Aliambiwa ni hatari kuwa na kipindi cha aina hiyo.

Fikiria Pasco angeajiri watu wangapi?
 
Hata Waandishi wa habari pia hawako huru. Uminywaji umekuwa mkubwa kiasi wanashindwa kuwa wabunifu. Sidhani kama tutazalisha wakina Kikeke wengine kwa miaka hii.

CCM imeshikilia Mateka sekta nyingi sana asee. Kwa akili ya kawaida tu unahisi Simba na Yanga hazikupenda kuombeleza maisha ya Watanzania waliouwawa October 29?

Kwa kila siku ambayo CCM itaendelea kuwa madarakani maisha kiujumla, ubunifu, uzalishaji, sanaa itaendelea kuwa ya wasiwasi hivi hivi.

Kupata waandishi wa habari nguli ni ndoto mkuu kwa sasa!huu mtaala mpya wa elimu ni tatizo!

Inawezekana watekelezaji hawajauelewa au wenyewe tu una makosa!
Ngoja tuone tutaishia wapi😓😓
 
Hata Biashara ya T-shirt za M4 C, People's Power, CHADEMA ✓,No Reforms No Election nk.zimekufa.Zamani ukinunua T-shirt 10 nyeupe za Mitumba,ukachapa hayo maneno,watoto wanakula nyama.: CCM ni hovyoo
 
Kabisa... Hata mauzo ya mashati ya Kadet pamoja na nguo za Khaki.
 
Nakumbuka miaka ya 2006-2010 nilikuwa mtumiaji mkubwa wa magazeti
1. Mwanahalisi
2. RaiaMwema
3. Mwananchi
4. Mwanasport
5. Africa this week, sijui nimeipatia.
6. Daily News
Ilikuwa ni lazima niyasome tena kwa kila toleo,kutokana na majukumu wakala alikuwa ananiletea namlipa mwisho wa mwezi.

Tokea ujinga ujinga kwenye habari ianze, niliachana na habari ya kununua magazeti tokea 2011. Nikajiunga jamiiforum 2012 baada ya kuwa msomaji wa mada motomoto kuanzia 2007. Nakumbuka mdahala wa Zomba (ccm) na Zito (CHADEMA) ndani ya jamiiforum tena mdahalo online.
CCM wakabuni njia ya kuangamiza jamiiforum kwa kuanzisha kitengo cha propaganda ndani ya jamiiforum kwa kuelekeza vijana wake kuwa na ID zaidi ya 1 ili waeneze upotoshaji kwa wingi.

Enzo zile akina Mwigilu, Mnyika, Zito, Ben Saanane, Pasco, Zomba, Melo, Mtoi, Rejina Mtema, Nape, Mkandara, Dk. Slaa, Arusha One, MTK, The BOSS na wengine wengi sana. Ulikuwa ukiona new topic inakulazimu kumaliza kwanza kazi ndipo utafute muda wa kusoma mada husika.

Kule jukwaa la great thickers, mada inamaliza wiki hakuna mchangiaji kwasababu kama hauna ushaidi basi unashindwa namna ya kuandika porojo.

Siku hizi kila awamu inakuwa na wapiga propaganda ndani ya jamiiforum, awamu hiyo ikiisha na hizo ID pia zinapotea.
Kulikwepo na members kipindi cha awamu ya nne, ilipoingia awamu ya tano wale members wakapotea na kuanzishwa tena members wengine. A

Awamu ya tano ilipokoma ID zile nazo zikapotea, awamu ya sita nako ikaanzisha members wengine.
Cha kushangaza, ID hizi mpya zinazoanzishwa zinajikita zaidi kutetea ccm na serikali. Mijadala yao yanabase zaidi kwenye utetezi bila fact tofauti na waliokuwa wanatetea serikali na ccm huko nyuma 2006-2010.

Wazee wangu; Ukwaju, barafu, buzirayombo,mlenge, mchambuzi, makumi, mlipotelea wapi?
 
Fikiria CHADEMA inataka kufanya mkutano ama kikao kwenye ukumbi wa kukodishwa, lakini mwenye ukumbi anaogopa kuwakodisha CHADEMA kisa CCM.

Huyo mwenye ukumbi anakosa fedha kiasi Gani? Halafu hapo hapo watu wa Kodi wanataka makusanyo ya Kodi yawe makubwa.
 
Back
Top Bottom