Jinsi Bidhaa feki zinavyoshughulikiwa

Abunwasi

JF-Expert Member
Jun 25, 2009
5,486
3,468
Wana JF mara nyingi tumekuwa tukishuhudia kupitia luninga zetu namna bidhaa feki zinavyo haribiwa. Tumekuwa tukiona TV pamoja na vifaa vya elektroniki vikipondwapondwa na mabuldoza na watu wakifurahia hali hiyo.
Lakini jee! tunajiuliza kama njia tunayotumia ya kuharibu bidhaa hizo haitatuumiza baadaye?
Wenzetu wanakuwa waangalifu sana katika kushughulikia vifaa kama TV ambapo ile tube[CRT] hutolewa kwa uangalifu sana na vifaa ambavyo vimetengenezwa kwa kutumia madini sumu navyo pia hutolewa kwa uanghalifu mkubwa kabla ya kuharibiwa.
Juzi niliona vipodozi ambavyo inasemekana ni hatari kwa binadamu vikipondwa na buldoza.
Suala linakuja jee hiyo ardhi ambayo kila siku inatumika kuharibu vitu hivyo haiathiriki? Jee hayo madini au kemikali sumu zikipenya ardhini na kubebwa na maji ya mvua hadi kwenye mito ambayo ndiyo chanzo kikuu cha maji ya kunywa hatutaathirika
icon5.gif
NEMC ipo jee inashirikishwa kwenye hili?
Hivi kwa ninin tunapenda kujipiga risasa miguuni mwetu kwa makusudi halafu tukichechemea kutokana na vidonda hivyo tunaanza kulalamika.
Hivi hali hii itaendelea hadi lini
icon5.gif
 
Back
Top Bottom