Raia mdogo
JF-Expert Member
- Jan 5, 2018
- 1,399
- 1,543
Kumbe story inaendea Pasipo mi kujua.
Msitudanganye tu kwamba nyie mnaomsema Mary kwamba ndio mko smart kiasi kwamba utachomoa kunasa kwenye ndaono kama hiyo...! Humu humu tu wengi tayari mmeingia kibra kwa inside. Ni vile tu ngumu kumtokeanilidhani Mary ni smart upstairs kumbe ni mpuuzi wa mwisho
Nawewe ukiwemo, ulitaka umtunuku kakuchomolea nini mkuu ?Msitudanganye tu kwamba nyie mnaomsema Mary kwamba ndio mko smart kiasi kwamba utachomoa kunasa kwenye ndaono kama hiyo...! Humu humu tu wengi tayari mmeingia kibra kwa inside. Ni vile tu ngumu kumtokea
Kesi ishakiwa ngumu😂😂😂Nawewe ukiwemo, ulitaka umtunuku kakuchomolea nini mkuu ?
Zamani hawakuwa wanafuatilia sana kama sasa. Sahivi ukitumia Njano kukamatwa ni rahisi, labda uwe mjanja sana.Mzee uliwezaje kufanya bolt/Uber miaka ypte hiyo na plate number ya njano pasipo, ulikuwa upati usumbufu wowote kwa Traff na majamaa wa TRA barabarani
Edo kissySEASON 03
CHAPTER 2
A TRUE STORY BY INSIDER MAN
PREVIOUS:
Nilipowasili kwa Jane, nje ya geti lake, magari yalikuwa yamejaa, yakipark kwa mpangilio usio wa kawaida. Nilishuka kwenye gari na nilisimama kimya kwa sekunde chache, nikibaki nayaangalia magari, haikuwa kawaida.
“Ni nini kinaendelea hapa?” nilijiuliza nikiwa bado nimekamatwa na mshangao.
CONTINUE:
Sikuwa nimetoa taarifa kwa Jane kwamba ningepita kumsalimia-nilitaka iwe kama surprise. Jumla ya magari yalikuwa tisa, yote ya kifahari, hakuna hata gari la kawaida. Nilisimama kwa muda nikitafakari cha kufanya, maana hata ule mzuka wa kugonga geti ulipotea ghafla. Nikaanza kutembea taratibu kuelekea getini, nikitaka angalau kuchungulia kidogo ndani.
Dereva wa Uber naye alishuka kwenye gari, akaniita kwa sauti ya chini. Ilikuwa imepita dakika kama tano bila mimi kumwambia chochote.
“Bro! Naona unaniweka njia panda, sijui hatima yangu ni ipi,” akasema.
“Nisubiri kidogo, naona hapa kuna ugeni mkubwa…, unanirudisha home.”
“Home wapi?”
“Mbezi Beach,” nikamjibu kwa kifupi.
Nilipokaribia geti, woga ukaanza kunipanda. Niliwaza labda kuna jambo lisilo la kawaida limetokea, ndiyo maana kulikuwa na huu ugeni wa kutisha. Wakati bado nipo kwenye mawazo hayo, ghafla nikamuona Vicky akitokea mlangoni. Alisimama kibarazani, akiongea na simu kwa utulivu. Papo hapo nikahisi ahueni, nikajipa ujasiri na kuanza kugonga geti.
Vicky alikuja kufungua geti. Mara tu alipoona ni mimi, akanyamaza ghafla, akaacha kuongea na simu yake na kunitazama kwa mshangao kwa sekunde kadhaa.
VICKY: “It’s you, Insider… au naota?”
MIMI: “Huenda kweli unaota. Hebu sogea karibu kwanza nikukumbatie… nimekumiss sana.”
Alinisogelea mpaka tukawa uso kwa uso, kisha tukakumbatiana kwa hisia sana.
MIMI: “Sikutegemea kukuona hapa. Umeshafunga chuo?”
VICKY: “Nimemaliza mitihani jana na nimerudi asubuhi. We mwanaume ulikuwa wapi? Maana simu zako hazipatikani.”
MIMI: “Nilisafiri nje kwa mambo ya kikazi. Hebu niambie, hapa kuna nini kinaendelea?”
VICKY: “Dada Jane aliugua sana pamoja na mtoto, hadi wakalazwa hospitali. Hivi ninavyokuambia, ameruhusiwa Jumapili tunamshukuru Mungu anaendelea vizuri.”
MIMI: “What? Mbona hakuniambia?”
VICKY: “Hivi ninavyolalamika kwamba simu zako hazipatikani, hata meseji hujibu, unafikiri naongea utani? Hebu angalia WhatsApp zako. Nilikutumia ujumbe nikikuambia Dada Jane anaumwa na amelazwa Rabininsia.”
Ilinibidi nitoe simu haraka ili kuthibitisha kama kweli Vicky anachosema kina ukweli. Baada ya kuangalia WhatsApp, nikajionea mwenyewe alikuwa amenitumia ujumbe kuhusu Jane kuumwa pamoja na mtoto wake, tena kupitia simu ya Jane. Lakini jambo lililonishtua zaidi ni kuona kwamba meseji hiyo ilikuwa imesomwa. Nilihisi huenda Iryn ndiye aliyeisoma, kisha akaamua kunyamaza kimya. Nikajiuliza kwa masikitiko-kama ningepata huu ujumbe, si ningekuwa nimerudi Dar mara moja kwa ajili ya Jane?
Nilijua fika jinsi Iryn anavyojua uhusiano wangu wa karibu na Jane, na naamini asingependa mimi kuondoka South mapema kama ningejua hali halisi.
Nikabaki nimesimama pale nikisikitika, huku najilaumu na nilijisemea “Kama jambo baya lingetokea, ningekuwa nimeanguka kwenye mtihani wa marehemu Pama.”
Kulikuwa na ukimya wa takribani dakika moja, kisha Vicky akaendelea kuongea. Wakati huo tulikuwa tumeegemea nyuma ya moja ya magari ya kifahari yaliyokuwa yamepaki karibu na geti.
VICKY: “Insider, usijilaumu kwa hili. Naelewa una familia na unapambana na maisha. It is not your fault-cha muhimu, amepona na yuko salama pamoja na mtoto.”
MIMI: “Na haya magari yote ni ugeni wa kina nani?”
VICKY: “Ni ndugu wa Pama. Wamekuja kwa pamoja kwa masuala ya kifamilia.”
MIMI: “Ahsante kwa taarifa, Vicky. Kwa kuzingatia mazingira ya hapa, wacha niende kwanza… nitakuja kesho.”
VICKY: “Hapana, usiishie nje. Karibu ndani, au nikuitie Dada Jane?.”
MIMI: “Hapana, muache na wageni wake. Naomba pia usimwambie kama nilikuja.”
VICKY: “Usijali..lakini zawadi zangu je?”
MIMI: “Zipo kwenye begi, za kutosha kabisa. Tuwasiliane kesho, maana mazingira unayaona.”
Baada ya mazungumzo haya yaliyodumu kama dakika 15, nilimuaga Vicky kisha nikaanza safari ya kurudi nyumbani, nikiwa na mawazo tele.
Nilipofika nyumbani, giza lilikuwa linaanza kuingia taratibu, hewa ikiwa na ule harufu wa jioni baada ya siku ndefu. Elena alitoka mlangoni kunipokea, na mara tu aliponiona alikuja spidi na kunipa kumbatio zito, alinonekana amenimiss sana. Alinikumbatia kwa nguvu kana kwamba hakutaka kuniachia, kisha akanipokea mabegi mikononi mwangu bila hata kuuliza.
Tulipoingia ndani, nikamkuta Sister Seblen amekaa. Alisimama kwa shida na kuja kunikumbatia mdogo wake. Lakini macho yangu yalibaki yakitua kwenye tumbo lake lilikuwa limekua sana. Ile safari tuliyokuwa wote South, tumbo lake lilikuwa dogo na kawaida lakini sasa, hakuna cha kuficha tena ujauzito wake ulikuwa wazi.
“Pole sana, dada yangu… naona mambo si haba,” nilimwambia nikimwangalia kwa huruma.
“Nashukuru, mdogo wangu… na wewe pia pole na safari,”
Kwa upande mwingine, mama J hakuwepo nyumbani na Junior alikuwa amelala usingizi mzito. Tukakubaliana tutoke nje, tukakaa kwenye kibaraza, ili tuzungumze masuala ya kifamilia kabla mama J hajarudi.
SISTER: “Insider, kuhusu suala la maisha ushatoboa mdogo wangu, kwa hili nakupa hongera. Yaani kama unaweza ku-afford nyumba ya laki tano kwa mwezi, wewe siyo level yangu tena.”
MIMI: “Hahaha! Najibana tu, dada yangu. Unaona sasa, level niliyofikia kupanga nyumba kubwa hakuwezi kuepukika, hasa kwa ajili ya wageni.”
SISTER: “Sasa vipi biashara zako za Dodoma? zinaendaje?”
MIMI: “Namshukuru Mungu, zinaenda vizuri sana, dada yangu. Lakini kwanza nianze kukupa pole, maana najua ninakuchosha kuja Dar na huku ulipaswa upumzike.”
SISTER: “Mimi na wewe tumetoka mbali sana, umesahau kipindi tunakua, ulikuwa unanipa assist nakwenda kwa shem wako, halafu tunarudi pamoja home?”
Maneno yake yakanirudisha mbali sana. Nakumbuka kabisa, bila mimi, alikuwa hawezi hata kutoka kwenda kwa shemeji yangu, ambaye sasa ndiye mume wake. Mimi nilikuwa nampeleka, kisha wakiniacha seblen nikicheza PlayStation. Wakati huo Sister alikuwa Form Six.
MIMI: “Yaani! Nilikuwa mjinga sana… nakupeleka ukaliwe kisa PlayStation? Nikikumbuka nacheka sana na najiona mjinga.”
SISTER: “Ndomana anakuitaga bonge la shem.”
Nilianza kwa kugusia jambo ambalo lilikuwa zito moyoni mwangu ambalo ni suala la Iryn na mtoto. Hili halikuwa jambo la kawaida, kwani lilihitaji umakini wa hali ya juu na busara kubwa. Na kwa hali ilivyo, mtu pekee ambaye nilihisi anaweza kunisaidia na kupita salama, alikuwa yeye. Nilihitaji mbinu, si za kawaida, bali zile muhimu ambazo zingehakikisha natoka kwenye hili tanuri la moto.
MIMI: “Wifi wako wa South anataka tumpeleke Aria kwa babu na bibi zake huko mkoani, na yuko very serious. Naona kuna haja ya kuanza hizi process mapema kabla haijawa too late… au unasemaje?”
SISTER: “Mhh… mdogo wangu, tulia kwanza. Give it time… angalau baada ya miezi sita ndipo uanze.”
MIMI: “Miezi sita? Bora nianze process mapema, hata mzee ajue kinachoendelea. Wifi yako si muda ataanza kelele, na nimemuahidi juu ya hili.”
SISTER: “Iryn asikupatie presha. Jambo alilofanya anajua kabisa kazingua, na wewe unahitaji muda wa kuliweka sawa na familia. Huyu niachie mimi, halafu sioni sababu ya kumueleza mzee kuhusu hii ishu ni bora ukaongea na mama direct.”
MIMI: “What? Niongee na mama tena, na si mzee? Kumbuka wewe ndiye ulikuwa unanipa ushauri wa kuongea na mzee? Iweje leo unasema hivi?”
SISTER: “Hadi nasema hivi ujue sijakurupuka. Wewe na mzee hamjawahi kwenda sawa tangu zamani. Ninyi ni watu wasio na bond kabisa tofauti na mama ambaye mmeshibana. Sidhani kama mzee atachukua hili suala kwa uzito kama mama atakavyolichukulia. Kwahiyo, kwa sasa huwezi kunielewa, lakini ipo siku utanielewa kwanini nasema hivi. Kumbuka, nilisema subiri angalau miezi sita kabla hujaanza process.”
MIMI: “Ukweli unanichanganya, maana wewe ndiye….”
Alinikatisha nikizungumza…,
SISTER: “Did I ever fail you?”
Nilitikisa kichwa kuonesha hapana…. Na aliendelea kuzungumza;
“Naanda mpango mzuri kabisa ambao jambo litawafikia wazazi bila tatizo lolote na kwa wakati muafaka. Kumbuka, wewe si mwanaume wa kwanza kuzalia nje.”
MIMI: “Nikiona pia hali uliyonayo, najisikia nimechoka naishiwa nguvu kabisa.”
SISTER: “Ondoa wasiwasi, kila kitu kitakwenda sawa hivi karibuni. Usijipe stress.”
Mada ikabadilika, tukaanza kuzungumzia kuhusu mama J, ambapo Sister alisema hana shida na amesamehe. Mama J kwa upande wake, anachukulia mambo ya kugombana na kutofautiana kati ya wapendanao kuwa ni kawaida, hivyo hana tatizo na tayari alisamehe. Aliongeza kuwa ataondoka Ijumaa, na kesho tutafanya kikao cha pamoja na wife ili kuweka mambo sawa kabisa.
Maongezi yetu yalidumu kwa takribani saa na nusu. Nilipoona muda umefika, niliondoka nikiwa na mawazo mengi, nikaenda chumbani kuoga na kupumzika.
Ukweli sikumuelewa Sister juu ya kubadili msimamo wake wa awali. Nilidhani huenda mimba ilikuwa ikimchanganya, ndio maana akabadilisha mawazo kuhusu suala hili. Nilifikiria sana na kuamua kuzungumza naye tena kabla ya kuondoka, ili kuweza kuthibitisha kama msimamo wake ni wa kweli. Hata hivyo, nilipata wakati mrefu nikiishiwa nguvu, nikiwa kitandani nikijaribu kufikiria mambo mengi na hatimaye usingizi ukanikamata.
Baadaye, niliamshwa na wife kwa ajili ya chakula cha jioni. Aliketi pembeni yangu, akiniangalia kwa macho makali-kisha alianza kuzungumza:
WIFE: “Hatimaye umeamua kurudi home tena bila kutoa taarifa.”
MIMI: “Hujapenda mimi kurudi home?”
WIFE: “Mara mia ungeendelea kubaki huko, kwa dharau uliondoka bila kuaga na hata simu haukupiga kujua hali ya mwanao.”
MIMI: “Simu nilikuwa napiga, hata meseji nilikuwa natuma.”
WIFE: “Ulipiga simu mara moja tu.”
MIMI: “Mara nyingi wewe hukupokei. Na kwanini wewe usipige simu unijulishe hali yangu?”
WIFE: “Je, ulikuwa unatarajia mimi nipige simu, mwanaume ambaye hujui hata umekosea na haukuomba msamaha?”
Kama kawaida ya wanawake, alianza kuzungumza kwa maneno mengi bila kupumzika. Nilimsoma huyu atakuwa na upwiru na anahitaji kushughulikiwa, hivyo niliamka kisha nikakamata mkono na kumvuta karibu nami, nikazungusha mikono yangu kwenye kiuno chake kwa taratibu.
“Baba J niache, please sitaki!.” Aliongea kwa ukali huku akijaribu kujinasua.
Sikukata tamaa, nikampushia kitandani, nikaanza kupapasa hips zake kwa taratibu. Ingawa nilikumbana na upinzani wa awali mkali, mashambulizi yangu yaliendelea kwa nguvu na uvumilivu, hadi hatimaye alikubali kuachia goli wazi bila mpinzani.
Mchezo ulianza kwa presha kali, lakini baada ya dakika chache hali ikatulia kidogo. Nilianza kushambulia kwa kasi kubwa, nikifanya “pressing” kali, lakini bao bado halikupatikana. Ghafla, Junior alitokea kuvuruga mchezo mzima, kwani alikuwa anagonga mlango kwa nguvu, huku akiita ‘mama’ akihitaji kufunguliwa haraka.
Baada ya kupata chakula cha jioni, nilirudi chumbani kulala nikiwa na uchovu mwingi. Nilijua kesho ingekuwa na ratiba ndefu sana na ilibidi nipumzike vizuri ili niwe na nguvu za kukabiliana na mambo yote niliyokuwa nimepanga kwenye ratiba yangu.
*******
Asubuhi ile niliamka mapema sana, maana siku hiyo ilikuwa na ratiba nyingi. Nilipanga kuanza na safari ya kwenda ofisini Masaki kufuatilia maendeleo ya kampuni, kisha kuonana na wakili kwa ajili ya suala la Iryn, na jioni kuhitimisha safari yangu Mbweni kumtembelea Jane.
Baada ya kifungua kinywa, niliondoka nyumbani saa mbili asubuhi. Kituo changu cha kwanza kilikuwa Masaki, getini mwa ofisi. Mlinzi ambaye siku nyingi hatukuwa tumeonana, ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza kunipokea. Tulipiga stori chache za kufungua siku kabla sijaingia ndani kuendelea na majukumu.
Nilipokuwa nikiingia ofisini, Winny alitoka barazani akiwa ana ongea na simu. Aliponiona, alinikimbilia kwa kasi, akanikumbatia kwa furaha, na mara moja tukaanza mazungumzo. Tulitembea pamoja hadi ndani ya ofisi, tukiendelea kufurahia maongezi yetu. Zaidi ya yote, alitaka kujua maendeleo ya mtoto na mama yake.
Muda huu, ofisi ilikuwa kimya kabisa. Ni Winny pekee ndiye aliyekuwa amewahi kufika. Kwa kawaida, siku za katikati ya wiki, muda rasmi wa kufika ni saa nne asubuhi. Winny alikuwa amewahi kwa sababu alikuwa na miadi na mteja wake. Baada ya maongezi mafupi, aliniaga na kuniacha nikiendelea na kazi.
Nilitulia ofisini na kuanza kupitia ripoti zote ambazo nilikuwa nimetumiwa kipindi nikiwa sipo. Nilitumia takribani saa moja kuhakikisha kila kitu kiko sawa. Baada ya hapo, nilienda kukagua mashine ya EFD kujiridhisha, kisha nikakagua pia hesabu za stoo.
Nilijikuta nikitabasamu moyoni, Hilda alikuwa amenivutia sana kwa kazi yake. Ripoti zake zilikuwa safi bila dosari hata moja. Kwa hakika, alikuwa anafanya kazi nzuri mno.
Baada ya kumaliza ukaguzi wa stoo, nilitoa simu mfukoni na kuingia Whatsapp, nikagundua kuwa Iryn alikuwa amenipigia video call mara mbili. Bila kusita, nikampigia papo hapo. Jana usiku alikuwa kanitafuta, lakini sikupokea kutokana na mazingira ya nyumbani kutokuwa rafiki kwa mawasiliano yetu.
Simu iliita kwa sekunde kadhaa na baada ya kupokea simu, alianza mara moja kwa kuuliza kwanini sipokei calls zake?. Nikamweleza hali halisi kwamba nimerudi nyumbani, na kwa sasa awe makini asipige simu kiholela. Nilimpa pia taarifa za ofisi kwa ujumla kuwa kila kitu kiliendelea vizuri na hakuna tatizo lolote. Alifurahi sana kusikia hivyo, kisha alinijulisha kuwa amewasiliana na mama Janeth, ambaye tayari amerudi Dar es Salaam.
Tulizungumza mambo mengi kuhusu mtoto na ugeni anaoutegemea kutoka Ethiopia. Pasipo kusahau alinikumbusha tena suala la yeye kuwatambua wazazi wangu. Baada ya kuagana, nilibaki kimya nikitafakari maneno yake.
Ghafla mlango ulifunguliwa kwa nguvu. Hilda akaingia kwa kasi kana kwamba alikuwa akikimbizwa.
“Insider…”
Aliita kwa sauti yenye mchanganyiko wa mshangao na furaha. Bhasi, nilipomuona, niliinuka haraka na tukakumbatiana kwa nguvu.
“Nimeona gari yako pale uwanjani nikajua ni wewe…” Hilda alisema huku bado akihema.
Tulitembea hadi kwenye sofa na kukaa.
MIMI: “Nilitaka nikusuprise, mummy.”
HILDA: “Nimefurahi sana kukuona, Insider. Mtoto hajambo?”
MIMI: “Aria mzima wa afya. Hata muda si mrefu nimetoka kumsalimia.”
Nilitoa simu mfukoni na kumuonyesha picha za mtoto, baadhi akiwa na mama yake.
HILDA: “Katoto kazuri sana… na Iryn kapendeza sana akiwa na mtoto.”
MIMI: “Hata wewe ukizaa utakuwa kama Iryn. Ni suala la muda tu.”
HILDA: “Insider, umebadilika sana. Hivi ungekaa mwezi, si tungekusahau?”
MIMI: “Jamani… nimebadilika sana hivyo?”
HILDA: “Sana! Inshort, nimefurahi sana kukuona, hata hamu ya kufanya kazi imepotea.”
MIMI: “Kwahiyo una hamu ya kufanya nini?”
HILDA: “Hata sijui… yaani nishinde na wewe tu tupige stori. Nilikumiss sana.”
MIMI: “Lucy yuko wapi?”
HILDA: “Dada Lucy yuko kwenye mitihani, nafikiri anamaliza wiki hii. Mama Janeth pia karudi na jana tulikuwa naye hapa na alikuulizia.”
MIMI: “Pia niseme ahsante kwa kuisimamia kampuni kipindi chote nikiwa sipo-umeifanya kazi vizuri sana.”
HILDA: “Usijali, haya ni majukumu yangu ndomana mnanilipa mshahara. Yule dada wa website development alisema wamemaliza kazi, nikamwambia bossy akirudi atakutana na wewe.”
MIMI: “Umefanya vizuri. Ngoja nikaonane naye ili nione kazi iliyofanyika, halafu nikirudi mchana, tutaenda lunch pamoja, utachagua sehemu ya kwenda. Wiki hii yote hadi ikimalizika, lunch na dinner zote zitakuwa juu yangu.”
Nilipoanza kuondoka, Hilda aliuliza
HILDA: “Sasa unaenda wapi, Insider?”
MIMI: “Naenda kumcheki dada IT… au twende wote?”
HILDA: “Hapana, uwahi kurudi basi tukale lunch.”
MIMI: “I told you, wiki nzima hadi inaisha, suala la lunch na dinner ni juu yangu.”
Hilda alitabasamu tu na nilimwacha ndani ofisini. Niliwasalimia wafanyakazi wengine waliokuwa wamefika, kisha nikaondoka kuelekea ofisini kwa Immaculate.
Nikiwa njiani, nilipata wazo la kwenda kumsalimia mama Janeth. Nikampigia simu Jessie, mfanyakazi wake wa pale nyumbani, ili nijue kama mama yupo. Baada ya mazungumzo mafupi, Jessie aliniambia mama ameondoka asubuhi kwenda kazini.
Safari haikunichukua muda mrefu hadi kufika ofisini kwa dada. Baada ya kupark gari, nilienda moja kwa moja hadi mapokezi. Pale, nilimkuta dada wa reception, nikamsalimia kisha nikamuuliza:
MIMI: “Hi, Immaculate nimemkuta?”
RECEPTION: “Imma ametoka muda mrefu sana, unaweza msubiri pale kwenye kochi.”
MIMI: “Nimsubiri mtu ambaye sijui ameenda wapi? Na akichelewa kurudi je?”
RECEPTION: “No, ametoka lunch.”
Niliangalia saa yangu na ilikuwa inasoma ni saa sita kasoro mchana. Nikajisemea huyu dada anaongea tu.
MIMI: “Alright, mwambie Insider alikuja. Kama atawahi kurudi, basi anipigie simu. Kuna sehemu naenda mara moja.”
RECEPTION: “Karibu sana, Bossy.”
Niliondoka kuelekea ofisini kwa mama Janeth, nikapaki gari nje, kisha nikashuka kuendelea kwa miguu hadi getini. Walinzi waliponiona, walinisalimia kwa bashasha, asilimia kubwa yao wananijua, hivyo mara nyingi hawanisumbui na maswali ya ni wapi naelekea.?
“Mtoto wa Bossy, karibu. Vua mkanda wako, saa, toa simu, weka kwenye mashine humu ili tuscan,” mmoja wao alisema kwa utani huku akiendelea na taratibu za ukaguzi.
Baada ya kumaliza utaratibu wote wa pale getini, niliingia ndani na kuelekea moja kwa moja hadi mapokezi kumuulizia mama Janeth.
Pale reception, nilimkuta dada mgeni, sikuwa nimemwona hapo kabla, hii ilikuwa mara yangu ya kwanza kabisa.
“Habari yako, naitwa Insider. Namuulizia Ms. Carter, nina shida ya kuonana naye.”
“Do you have an appointment scheduled with her?” akauliza kwa Kiingereza.
“No, I don’t have. Please call her and let her know I’m here, and listen to what she’ll say,”.
“Okay, wait for a second,” akasema huku akichukua simu kumpigia.
Baada ya kuzungumza naye kwa muda mfupi, aligeuka kuniambia,
“You can go to her office. Do you know the way?"
Nilitikisa kichwa kuonesha ndiyo, kisha nikaelekea moja kwa moja hadi ofisini kwa mama.
Baada ya kufika ofisini kwa mama, nilianza kwa kumsalimia PS wake (Personal Secretary). Alinifungulia mlango kwa kutumia code, kisha nikaingia ndani ya ofisi. Ile nataka kusalimia, mama kashaanza kuniita jina ,
MAMA: “Insider…”
MIMI: “Naam mama! How are you doing? It’s been a while.”
MAMA: “Karibu, ukae.”
Mama alinuka na kuja kukaa kwenye sofa. Ofisi yake ilikuwa na sofa tatu za kukaa (one sitter), pamoja na meza nzuri katikati. Alitoa wine kwenye fridge pamoja na glass mbili, akaniminia kidogo, kama nusu glasi, kisha tukaanza maongezi.
“Iryn alinitumia picha za Aria asubuhi, mmefanana kweli sana!”
MIMI: “Ahsante mama. Asubuhi nilipita ofisini kuangalia maendeleo ya kampuni , na Hilda akanipa taarifa kwamba uliniulizia. Ndomana nimekuja nikusalimie pia tuzungumzie masuala ya kampuni.”
MAMA: “Hilda ni mchapakazi, anajitahidi sana kusimamia kampuni.”
MIMI: “Kweli sana, hata mimi sikutegemea hesabu zote zingewezekana kuwa na balance nzuri hivi. Sasa mama, nilikuwa na wazo au ushauri kuhusu maendeleo ya jumla ya kampuni, lengo langu ni kuona value ya company inaongezeka na faida ikawa kubwa.”
MAMA: “Nakusikiliza, endelea….” Kisha akaketi kwa mkao mzuri wa kusikiliza kwa makini.
Nilimpa mama ushauri wa kujaribu kuwekeza pesa pamoja na faida tulizopata kutoka kwenye portifolio tofauti kama vile Treasury bills, Bonds, au kununua hisa za kampuni mbalimbali ikiwemo uwekezaji katika taasisi kama UTT. Lengo langu lilikuwa ni kuhakikisha faida inakua zaidi na kuendelea kuinua thamani ya kampuni.
“Kwenye akaunti zetu kuna pesa nyingi sana, na tukisema tuendelea kuziweka tu, haiwezi kusaidia kukuza biashara. Ni bora zile pesa tukazifanyia investment zenye tija ili tuendelee kuchumw faida na thamani iweze kuongezeka kwa wakati.”
Pia, nilishauri kuhusu umuhimu wa kutumia software za kisasa kama inventory valuation katika majukumu ya kila siku. Hii, nilieleza, itasaidia sana kuongeza ufanisi katika usimamizi wa stock, kuokoa muda mwingi na pia kutoa taarifa sahihi za mzunguko wa bidhaa katika kampuni.
Maongezi yetu na mama yalikuwa marefu sana na ya kina kuhusu hali na maendeleo ya kampuni. Kwa upande wake, mama alikubali ushauri wangu kwa moyo wote na alinipa baraka zote za kuanza kushughulikia yote tuliyoyazungumza.
Katika mazungumzo hayo, nilibaini kuwa kampuni mara nyingi huwekeza pesa nyingi benki, na benki hutoa faida ndogo mno, hali inayofanya uwekezaji huo kuwa kama aina ya kusaidia benki badala ya kuinufaisha kampuni kikamilifu. Hili nililiona ni tatizo kubwa na hivyo nilipendekeza kubadili mkakati wa kuweka pesa benki na kuanza kuwekeza kwa njia zenye tija zaidi.
Hii siku rasmi nilipewa password ya benki pamoja na ruhusa kamili ya kufanya malipo yote ya kampuni bila hata kuwajulisha wengine. Nilipokea kwa uzito jukumu hili na nikamshukuru sana mama kwa imani aliyonionyesha, nikimuahidi kuendelea kufanya kazi kwa uadilifu na kujituma kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa.
Baada ya kumaliza majukumu ya maendeleo ya kampuni, tulianza mazungumzo kuhusu suala la Iryn. Mama alikuwa na hamu kubwa ya kujua nilivyopanga hili, hasa ukizingatia mimi tayari nina mke na mtoto. Nilimweleza kuwa bado natafuta njia nzuri ya kuwasilisha suala hilo kwa wazazi wangu, na kwamba nitahakikisha kila kitu kinakuwa sawa na kinashughulikiwa kwa busara.
Niliomba msaada wake ili kuhakikisha suala hilo linakuwa imara na linashughulikiwa vyema upande wa Ethiopia. Mama aliahidi kutusaidia kwa dhati, na alisisitiza sana nihakikishe kwamba ninatengeneza “bond” za watoto mapema ili kuhakikisha usalama na maendeleo yao.
Nilitumia takriban masaa mawili na mama katika mazungumzo na mipango ya kampuni. Baada ya kumaliza, tulitoka pamoja, kwaajili ya kupata chakula cha mchana. Katika maongezi yetu tukiwa tunakula nilimwambia mama kuwa nitaenda kuonana na dada IT aliyekuwa anahusika na website development ya kampuni.
Baada ya lunch nilimpa mama ride hadi ofisini kwake, kisha nikaendelea na safari yangu kuelekea Haille Selassie Road kwa ajili ya kuonana na dada. Nilipofika kwenye parking cha magari ya ofisi yao, nilimpigia simu kumjulisha kwamba nimefika. Alinijibu mara moja akisema niende moja kwa moja ofisini kwake kwani alikuwa ananisubiri tayari.
Nilikuwa nina haraka sana na sikutaka kupoteza muda hivyo niliomba aanze kunionesha kazi ailiyokuwa amefanya. Imma alianza kunionesha kazi walizofanya kwenye tovuti, akifungua na kuelezea kila kipengele na jinsi tovuti itakavyofanya kazi kwa ufanisi. Nilivutiwa sana na muundo mzuri wa tovuti, ilikuwa rahisi sana kwa mteja kuingia na kuitumia bila usumbufu wowote.
Baada ya kuridhika na kazi walizozifanya, nilimwambia nitahakikisha malipo yaliyobaki yatalipwa haraka iwezekanavyo ili waweze kupandisha tovuti hewani kwa haraka zaidi. Nilitumia kama dakika 20, kisha nikamuaga naondoka kwa kumpa ahadi ya kufanya malipo kabla ya ijumaa na nikaomba tuonane tena hio siku.
Nikiwa nimetulia kwenye parking, mawazo yalikuwa yanapita kichwani mwangu kwa kasi, mpango baada ya mpango, lengo baada ya lengo. Nilikuwa nimepanga mambo mengi ya kukamilisha leo, lakini muda haukuwa rafiki. Saa yangu ilionesha ni saa 9 kamili mchana na dakika zikiendelea kukimbia. Nilijua wazi kuwa mipango mingine sinabudi kuiacha.
Nilijisemea moyoni, “Lazima leo niende Mbweni kumwona Jane. Hili siwezi kuliahirisha.” Lakini kwa upande mwingine, nilikuwa na ahadi kwa Hilda- ya kumpeleka lunch kama nilivyomuahidi. Nilipima muda nikaona hilo halitawezekana kabisa.
Ninafanya nini sasa? Na nilimpa ahadi nilijiuliza kwa msisitizo.
“Hilda nita deal naye kesho, lakini nikijiroga nikampigia simu sasa, basi ndo nimeharibu,” nilijiambia huku nikitabasamu kwakuwa niliona ni wazo zuri.
Kabla sijawasha gari kuondoka, nilipiga simu kwa Vicky kuulizia hali ikoje pale kwao. Akaniambia wageni wako kwenye maandalizi ya kuondoka, hivyo hakuna haraka sana, naweza kufika taratibu.
Kwa upande mwingine, mawazo yangu yaliteleza hadi kwa Mary. Nilijikuta nikimkumbuka sana na kutamani kumuona leo. Nikajisemea kimoyomoyo, “Huyu lazima nimtafute nikitoka Mbweni, kwa namna yoyote ile lazima tuonane.”
Nikiwa bado kwenye parking, nilimuona Immaculate akija moja kwa moja kulifuata gari langu. Nilihisi kama alikuwa na jambo muhimu la kuniambia. Alipofika, hata kabla hajagonga, nilishusha kioo taratibu na tukaanza mazungumzo.
IMMA: “Bossy, hujaondoka bado…?”
MIMI: “Ndo nataka kutoka hapa. Vipi, kuna jambo hatujamaliza?”
IMMA: “Hapana! Sijui unaelekea wapi? Nilitaka unipe support.”
MIMI: “Naelekea Mbweni…”
Kabla sijamaliza, aliniingilia kwa haraka.
IMMA: “Naelekea Makumbusho, Millennium Tower ni sawa tukienda pamoja?”
MIMI: “Yes, twende, nikupe ride.”
Nilikanyaga wese, tukaanza safari ya kuitafuta Alli Hassan Road tukiwa tuko na Haile Seillassie Road.
IMMA: “Niliambiwa ulikuwa nje ya nchi naweza kujua ulikuwa wapi?”
MIMI: “Nilikuwa France, kisha nikaenda China na India.” Nilimdanganya.
IMMA: “Waoh! Exposure ya kutosha. Natamani hiyo nafasi ingekuwa yangu.”
MIMI: “Kwani nyie kampuni yenu haiwapi tours za kusafiri?”
IMMA: “Mhh! Hapana… labda kwa maboss. Sisi wengine itokee tu kwa bahati.”
MIMI: “Lakini kampuni yenu ni international, nilitegemea mnasafiri sana. Na wewe una muda gani toka uajiriwe?”
IMMA: “Naelekea mwaka wa tatu sasa. Na huku Mbweni ndo unaishi, ni home?”
MIMI: “Hapana, huku naenda kumsalimia dada yangu. Mimi ninaishi Mbezi Beach karibu.”
IMMA: “Ahsante… nitakaribia siku moja.”
MIMI: “Wewe unaishi wapi?”
IMMA: “Kigamboni, karibu pia.”
MIMI: “Basi nitakaribia, usijali. Wakati wowote nitakupigia simu-uwe tayari kumpokea mgeni.”
IMMA: “Hahaa karibu sana. Nimezipenda sana product zenu, ila bei zitanishinda.”
Muda huu tulikuwa tumeshawasili kwenye kituo cha daladala cha Makumbusho (Bagamoyo Road). Nikaegesha gari pembeni, kisha nikamgeukia huku nikitabasamu
MIMI: “Kwa mrembo kama wewe bei si kikwazo. Utanitumia WhatsApp product uliyoipenda, nami nitaangalia namna ya kukupunguzia.”
Muda huo simu ya Vicky ikawa inaingia.
IMMA: “Okay thank you Insider, and thank you for the ride. See you later.”
MIMI: “Okay, byee…”
Nilimtazama Immaculate akishuka kwenye gari taratibu, nikafuatilia hadi alipovuka barabara upande wa pili. Nikajisemea kimoyomoyo, “Hii ni kazi” nikaendelea na safari yangu kuelekea Mbweni.
Nilitumia takribani dakika 40 kufika Mbweni. Vicky ndiye aliyetoka kunifungulia geti, nami nikaingiza gari ndani na alionekana kushangaa sana gari nililokuwa naendesha, na ile kushuka alianza maswali kama kawaida yake;
VICKY: “Insider, una Benz siku hizi?”
MIMI: “Hapana, nina Vitz.”
VICKY: “Msiuuu! Unajibu kwa shombo wewe mwanaume.”
MIMI: “Unauliza swali wakati tayari unajua jibu… unazingua. Shem wangu yuko wapi?”
VICKY: “Yuko sebleni… karibu.”
Niliingia ndani, ambapo sebleni kulikuwa na wageni wengine wawili. Jane aliponiona tu, alinyanyuka na kunisogelea huku tabasamu likimchora usoni. Tulikumbatiana, kisha nikasalimia wageni wengine ambao kwa kweli sikuwa nawajua, ndo mara ya kwanza nawaona machoni pangu.
JANE: “Insider, karibu sana… umetuchunia sana.”
MIMI: “Nisamehe sana, kwanza niliondoka bila kukuaga. Ilikuwa haraka sana.”
JANE: “Usijali, uliniambia na nilikuelewa. Vipi za huko China? Na umetuletea zawadi gani?”
MIMI: “Zawadi zipo, usijali. Jembe langu liko wapi?”
JANE: “Johnson kalala… Vicky alikuwa ananisumbua sana kuhusu wewe. Nafikiri akikuona atafurahi sana.”
Kisha akaanza kumuita Vicky…
MIMI: “Huyo tulionana jana, mbona nili…”
Jane akanikatisha, macho yake yakionyesha mshangao.
JANE: “Mlionana jana where?”
MIMI: “Jana nilikuja kukusalimia. Nilikuwa nimetoka safari, nikaona si busara kwenda nyumbani bila kukuona. Nilipofika, nikakuta ugeni mkubwa sana nje, nikaogopa hata kuingia. Vicky ndiye aliyetoka na kunieleza kinachoendelea.”
JANE: “Kwanini hukuingia? Ningetoka hata tuongee jamani.”
Wakati huo, Vicky akaingia na kukaa kwenye sofa.
JANE: “Vicky, umemuona Insider? Amenepa, sasa kawa HB zaidi. Haya sasa kazi kwako, maana ulikuwa unalalamika sana kwamba Insider hapatikani.”
VICKY: “Sio kunenepa tu, kaja na Benz mpya, kapaki hapo uwanjani. Kuonesha kwamba huko alikokuwa mambo yalikuwa mazuri.”
JANE: “Insider, si ndiyo ile ulosema ya ofisi kipindi kile?”
MIMI: “Yes, ndiyo ile. Sina uwezo wa kumiliki Benz jamani, labda atokee wa kunihonga.”
VICKY: “Bonge la Benz, hadi nimesisimka.”
Sote tulicheka, kisha Jane akaniomba tutoke nje tuendelee na mazungumzo yetu faraghani.
MIMI: “Pole sana kwa kulazwa na mtoto. Niliumia sana baada ya Vicky kunipa taarifa hizi. Nilipata ujumbe lakini sikuona sababu ya ubusy, nisamehe sana shem wangu.”
JANE: “Usijali, Insider. Naelewa unapambana kwa ajili ya familia, na sikutaka kukuchanganya na mambo yako ya kazi. Hata Vicky nilimwambia asikwambie, akuache. Lakini yote namshukuru Mungu, niko salama na mtoto.”
MIMI: “Jana kulikuwa na ugeni wa nini?”
JANE: “Ni ndugu wa Mzee Pama walikuja kunisalimia na kumuona mtoto.”
MIMI: “Waoh! Mary yupo?”
Jane akanitizama kisha akatabasamu.
JANE: “Naona umemkumbuka mchepuko wako. Mary yupo, na tulikuwa wote Jumapili. Ila Insider, alimind sana kuondoka bila kumpa taarifa. Alikasirika kweli.”
MIMI: “Tulishayazungumza na kumaliza.”
JANE: “Mimi siwezi kuingilia wapendanao… but be careful.”
MIMI: “Na vipi kuhusu Mzee Juma? Atakuwa ananitafuta sana, na vile sipatikani sijui nitamuingiaje.”
JANE: “Weeh! Nilimweleza umepata dharura na umeenda mkoani kwenye msiba. Alielewa, hana shida. Amesafiri, akirudi mtafute. Nafikiri wiki ijayo atakuwa amerudi.”
MIMI: “Ahsante sana kwa kuniwekea sawa kuhusu hili.”
Tuliendelea kuongelea masuala yake ya biashara na alikiri kuwa biashara yake inaendelea vizuri. Kutokana na ndoto yake ya kufungua biashara zingine, nilimshauri afungue kampuni ili aweze kuendesha biashara zote chini ya jina moja la kampuni. Kwa upande mwingine, Jane alipendekeza tuingie ubia kufungua biashara pamoja. Alinipa suala hilo na kusema nilishughulikie na nitampa mrejesho mbeleni.
Baada ya mazungumzo marefu, nilianza kufanya ukaguzi wa mazingira ya nyumba. Kwanza nilikwenda kuwacheki mbwa, ambao walionekana kukua kwa kasi sana. Baada ya hapo, nilitoka nje ya fensi kukagua mazingira ya nje ya nyumba. Nilipomaliza, nilirudi ndani na nikakumbuka kuwa sijashika simu kwa muda mrefu, nilijua nitakuwa natafutwa kwa kupigiwa simu.
Nilipokwenda kwenye gari kuchukua simu yangu, niligundua kuwa nilikuwa nimepishana na simu nyingi kutoka kwa watu mbalimbali akiwemo-Hilda, Lucy, Sister, Mama yangu mzazi, Sanchi, Prisca, Bob na wengine wengi. Kwani nilikuwa nimerudisha namba yangu ya kawaida ambayo huwa nipo nayo mtandaoni kila mara.
Kwanza nilianza kumpigia Sister, kwa sababu nilishtuka kuona missed calls za mama. Nilihisi ni bora kuzungumza na Sister kwanza ili kujua kama kuna jambo lolote muhimu ambalo niweze kujua mapema kabla sijampigia mama.
Baada ya kuongea naye, Sister alinieleza kuwa mama anataka kuzungumza nami kuhusu suala la mama J. Aidha, alinikazia sana niwahi kurudi nyumbani na nisimsahau mama J, hasa ukizingatia kwa kuwa ni muda mrefu hatujawa pamoja.
Baada ya kumalizana na Sister, nilijisemea nitamcheki mama baadaye kwa utulivu. Kisha nilimpigia simu Sanchi nilihisi atakuwa na jambo muhimu la kuniambia. Simu yake iliita mara kadhaa bila kupokelewa, nikaipiga tena mara mbili bila majibu hivyo, nikaamua kumpigia Mary.
Simu yake iliita kwa muda mrefu kabla hajapokea. Baada ya kupokea, nilimweleza nia yangu ya kuonana naye jioni hiyo kwa sababu nilimmiss sana. Nilimwambia kuwa niko Mbweni kwa Jane na nikitoka nitamtembelea kwake. Hata hivyo, Mary aliniambia yuko kwao Mbezi Beach na alisisitiza sana niwahi kwenda kwa sababu mzee wao yupo.
Mary alikuwa na maswali mengi, kubwa zaidi ni mimi kurudi bila kumtaarifu, nilimsoma hakupendezwa na nilichofanya. Nilimpanga kuwa tutazungumza tutakapo-onana, sikumpa nafasi kabisa ya kuongea.
Muda ulikuwa umeenda sana, ilikuwa karibu saa 12 kasoro jioni. Nilikuwa nikitafakari gia ya kutokea kwa Jane, kwani yeye alitaka niwe nimekula dinner kabisa kabla ya kuondoka. Niliendelea ku-buy time huku nacheza na Johnson pale seblen huku napiga story na Vicky.
Ilipofika saa 12 kamili, nilimuaga Jane kuwa nataka kuondoka. Nilimweleza kuwa nina mgeni nyumbani ambaye ni dada yangu, Jane alikubali hivyohivyo hakuwa na jinsi. Nilimpa ahadi ya kuja kumwona tena kesho, na kabla sijaondoka, nilichukua zawadi zake kwenye gari, nikampa kisha nikaondoka nikimuacha akiwa na furaha nene.
Njiani, nilikuwa na spidi kali nikitumia barabara ya chini inayotokea Ununio kuelekea kwa Mary. Niliendelea kukimbiza gari hadi kufika Kunduchi, pale sasa ndo kumpigia simu na kumpa taarifa kuwa nakaribia kufika. Kwa upande wake alisema alikuwa anakaribia kutoka home na tukutane kwa Zenna madukani, kwani atakuwa akinisubiri hapo.
Nilikuwa na hamu kubwa ya kufanya mapenzi na Mary, nikijisemea moyoni kwamba lazima niondoke naye, atakubali au laa!. Nilipofika kwa Zenna, nilimuona Mary akiwa akinisubiri kwa mbali. Nilimkaribia kwa gari, na yeye baada ya kuniona alikuja kwa haraka, akapanda, kisha nikaendelea na safari yetu.
Mary alionekana kupendeza sana, alizidi kuwa mzuri. Nilijikuta nikiwa mzito na kupagawa na hisia kali za ngono zilizidi kuzipamba hisia zangu zote.
Tulianza kuangaliana kwa ukimya kidogo, Mary akachanua tabasamu zuri na kali.
MARY: “Baby…”
Nilimkatisha kwa upole,
MIMI: “Yes, mummy. Samahani, najua nilikuchunia, ukweli ni kwamba unajua nilikokuwa. Lakini upendo wangu kwako umeongezeka zaidi kuliko hapo awali.”
Nilihisi kama nilimuwin na kuteka moyo wake, naye aliishia kuniangalia kwa upole na shauku.
MARY: “So, where are you taking me?”
MIMI: “Watch me…” huku nikitabasamu!
TO BE CONTINUED©️
Shukrani brother ✊
Hahahahaha poleni sanaMaskini mama J, mwanaume hana time anapuyanga tu lol!