Jino limetoboka nisaidieni wadau

Petrol Tank

JF-Expert Member
Jul 6, 2018
205
350
Jino langu lina tundu japo bado haliumi, nifanyaje?
IMG_20181027_215040.jpeg
 
Pole, nenda pale ubungo plaza waone kuna dokta pale ana ofisi yake, inaitwa jkb. Watakusaidia. Mi nilishatumia dawa yao. Ni ya kusukutua. Ila wanaangalia na hali ya jino. Kama limelika sana wanakushauri ukaling'oe
 
pole sana mkuu,inavyoonesha hupigi mswaki vizuri maana mdomo wako haupo normal hata kidogo anyway kwa ushauri zaidi namjua dokta ambaye yupo pale ubungo plaza kama mdau hapo juu alivyokushauri nenda atakusaidia kama upo dar lakini..
 
...jitaidi kusafisha meno kwa dawa ya meno ( colgate) angalau Mara 2 kwa cku utaona tu mabadilko Insha'Allah,apo inabid uache ubahili wa kichaga ununue miswaki bora ile ya buku au buku 2...
 
Hilo jino limelika na kuweka tundu. Jino lililotangulia kabla ya hilo ulilolibaini linaonekana linaanza kufanya tundu pia. Jino baada ya hilo lenye matatizo pia lina mabaki ya chakula yanaonekana wazi. Inaonekana umeishang oa magego mawili upande huo huo ishara kwamba tatizo lako la kuharibika meno ni endelevu.

Hilo jino lililotoboka linaweza kuzibwa kwa kutumia gundi mahsusi au risasi au kung olewa kabisa kama ulivyofanya kwenye meno mawili yaliyotajwa. huu hauwezi kuwa ufumbuzi wa kudumu kwa sababu kwa ushahidi uliouweka mwenyewe hapa, inaonekana hufuati utaratibu sahihi wa afya ya kinywa kwa maana ya kupiga mswaki kila baada ya kula.

Suruhisho ni kwenda kwenye kliniki ya meno iliyo karibu na eneo unaloishi ili kupata huduma ya kwanza na huko watakupa maelezo zaidi ya kitaalamu na hatimae watakushauri nini cha kufanya kuhusiana na jino lako. Kila la kheri
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom