Kwanza kabla sijatoa tiba, dawa ya jino sio kung'oa ila dawa yake nikulitibu. Mara nyingi ugonjwa wa meno husababishwa na bakteria wanaoathiri kinywa ndio mtu akashauriwa apige mswaki kila baada ya kula ama hususan usiku kabla ya kulala. Kwa tiba chukua mdaa, shabu na karafuu zote zikiwa unga na ujazo dawa changanya na utie kwa pamba na uweke sehemu ilioathirika. Utafanya Mara tatu kwa siku.