whether ni jini mahaba au ni pepo wa ngono, hayo yote ni majanga! Kwa uelewa wangu, jini mahaba huwa linampata mtu na kufanya naye tendo la ndoa katika hali isiyo ya kawaida. Na hayo huleta mfarakano wa mtu na mumewe/mkewe/mpenzie mara jini mahaba anaomuingia mmoja wapo wa wapendanao. Humjengea mpenziwe chuki, na kutokufurahia mahusiano na binadamu wa kawaida. Nimewahi kusikia pia mara nyingi humfanya mtu asipate mchumba na kuoa au kuolewa kutokana na wivu wa haya majini. Yakimpata mtu humfanya kujihisi anafanya tendo la ndoa usiku na kitu asichokifahamu. Akiamka asubuhi, anaweza kujikuta kachafuka sehemu za siri. Inasemekana baadhi ya migogoro ya ndoa hutokana na watu kuingiliwa na na viumbe vya namna hii ambavyo humfanya mmojawapo wa wapenzi kumchukia mwenzake.
Pepo la ngono ni tofauti kidogo. Nasikia kuwa hili likimuingia mtu, mtu huyo anakuwa anapenda ngono kuliko kawaida. Yeye muda wote anawaza ngono tu na mtu huyu hachagui mtu, yeyote atakayekatiza mbele yake, anamchukua. Haya pia huwafanya wanandoa kutokuwa waamanifu mara tu yanapowaingia. Baadhi ya ndoa zenye wanandoa wazinzi saa nyingine huchangiwa na mapepo ya namna hii.
Nimekupa tofauti kidogo ya hayo mapemo, pengine kutokana na utofauti huo nilioueleza unaweza kugundua sifa zake. Ni hatari kuwa na viumbe wa namna hivyo na kama kwa bahati mbaya unavyo ni vyema kufika kwenye maombi au kwa viongozi wako wa kiimani ili ukasaidiwe kufunguliwana kuwekwa huru.