Jini Kabula ataka wasanii waache kutoa kafara wasanii wenzao ili wafanikiwe

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Sep 7, 2016
17,415
21,111
Msanii Miriam Jolwa (Jini Kabula) ameonesha kukasirika sana kutokana na vifo mfululizo vya wasanii .Kabula hakusita kuvihusisha vifo hivyo na imani za kishirikina huku akitoa maneno makali kwa baadhi ya wasanii wanaoongoza kutoa kafara wenzao ili wafanikiwe katika kazi zao za sanaa.

Kabula ameyasema haya muda mchache baada ya msanii Ommy Dimpoz hali yake kuwa mbaya kupitiliza hivyo basi Kabula akaamua kukinukisha kwa wasanii wenzake waache kurogana na kuuana kisa mafanikio ya kisanaa ,badala yake wajikite katika kufanya kazi kwa bidiii na sio hiyo tabia ya kutembelea nyota za watu na mwisho wa siku kuuana kabisa.

Kabula alipotafutwa kujibu tuhuma hizo alikuwa mkali sana na kudai hataki mahubiri ya aina yoyote ,yeye akishasema amesema.

20180825_154146.jpg
 
Huyu atakuwa anaumwa maana ukizaliwa inabidi ujue lazima ipo siku utakufa there is no way you can escape that.... watu kila siku TZ wanakufa na wasanii ni kati ya watu.
 
UJUE WASANII WAKO KIBAO SIKUHIZI NDIYO MAANA INAONEKANA WANAKUFA WENGI TOFAUTI NA KITAMBO
KUNA WATU NAWAJUA(KAMA 10) WALIKUWA WALIKUWA NA LENGO NA KUWA WASANII
WOTE WALIKUFA MWAKA MMOJA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom