Pia kisayansi ukilala chali unadisturb equilibrium ya ubongo na moyo ndo sababu ya kisayansi ya hayo mauzauza. Inashauriwa usilale usingizi ukiwa chali position. Vifo vya ghafla usingizini pia usababishwa na kulala chali
atoto na we unalalaga chali dada'ngu? njoo huku umsikie shostito cute b na mauzauza yake, kumbe siku ile tunamtafuta alipatwa na mauzauza ya kulala chali bana
kama huo ndio ukweli basi wajawazito wenye mimba kubwa wangepoteza maisha wengi sana
Mkuu wezi wale wanakuja na dawa za "kizungu" na wanakupulizia.
Ni afadhali wakuweke kwenye chaga tu. Wanaweza kukufanyia kitu mbaya.
godogo ndio lugha gani?
Habari zenu wakuu,
Kuna vitu ambavyo naviwaza sivipati majibu mwenye uelewa kuhusu hili anisaidie.
Ni kwanini mtu unapolala kwa kuangalia juu yani bati anakuwa anaota ndoto mbaya za kutisha na kama vile kuna kukabwa flani hivi na hii sio kwangu tu nimewasikia watu wengi pia wakilalamika.
Je, jambo hili linahusiana na mambo ya kichawi kama wengi wanavyozani? Au kuna namna kisayansi lazima itokee endapo mtu akilala hivyo labla kuna vitu vinaforce ubongo kuhisi hivyo?
Wataalam naombeni msaada wenu
Al Habib ahsante sana.Ndoto na jina mizi ni vitu 2 tofauti. Ndoto unaota Jinamizi ni shetani anaye kukaba wakati unapo lala.
Kisayansi ukilala chali ulimi unaweza kurudi nyuma na kuziba koo la hewa, na ndio maana unahisi kukabwa (kukosa hewa/kushindwa kupumua) kwa kuwa upo usingizini hauwezi kujitambua hivyo utahangaika hadi utakapoamka utaweza kuurudisha ulimi na utasikia ile hali imeondoka.
Kwanza lazima uelewe kuwa dunia ina pande tisa , nane Zinajulikana na kutajwatajwa lakini nne ndio maarufu zaidi nazo ni kaskazini kusini mashariki na magharibi na upande wa tisa usiotajwa sana ni kile kitovu au Shina linalounganisha hizo pande linaitwa central axis
Pili hili anga limejaa roho na mapepo yaliyozagaa kila mahali na kama ujuavyo roho/pepo ni energy kitu chepesi kabisa kisichoonekana wala kushikika
Kwahiyo kinachotokea ni kwamba unapolala chali na kuangalia juu ni kama unakuwa kwenye central axis ya dunia yanapopita roho na mapepo yote lakini vilevile ni kama unayaalika kwakuwa unakuwa kama uko kwenye cental gravity ya dunia
Yale yanapopita yatakuachia upepo fulani ndio hayo mauzauza yale yanayovutika kuja ndio majinamizi
Kwahiyo haishauriwi kulala chali kwakuwa unaalika nguvu zisizofaa kualikwa
Angalia ibada nyingi za kishetani humlaza mtu akiwa uchi chali ameangalia juu
Pia kisayansi ukilala chali unadisturb equilibrium ya ubongo na moyo ndo sababu ya kisayansi ya hayo mauzauza. Inashauriwa usilale usingizi ukiwa chali position. Vifo vya ghafla usingizini pia usababishwa na kulala chali
atoto na we unalalaga chali dada'ngu? njoo huku umsikie shostito cute b na mauzauza yake, kumbe siku ile tunamtafuta alipatwa na mauzauza ya kulala chali bana
Kwani kulala unaplan kuwa ulale vipi? Hiyo inatokea tu ukiwa usingizini unajikuta ushalala hivyo.
Ukitaka kuota ndoto za kugegedana na demu chukua kanga isokote vizuri halafu itupe chini ya ufungu mwa kitanda kesho yake asubuh utakuta umetoboa godoro kwa kuligegeda!
18+ only
Yaani hii kwangu imeshakua ugonjwa hunikuti nalala hivyo na nikilala siwezi pitisha ata lisaa limoja tu lazima nikurupuke kwa ndoto mbaya
Kisayansi ukilala chali ulimi unaweza kurudi nyuma na kuziba koo la hewa, na ndio maana unahisi kukabwa (kukosa hewa/kushindwa kupumua) kwa kuwa upo usingizini hauwezi kujitambua hivyo utahangaika hadi utakapoamka utaweza kuurudisha ulimi na utasikia ile hali imeondoka.
Siku nyingine ukitaka kulala chali niite niweke ulinzi.
Mimi ni Sheikh Kifyatu na huu ndio utabiri wangu:
Katika siku za nyuma wewe ulimkwaza binti mmoja, mzuri sana, maji ya kunde, mtanashati, na anaishi kaskazini ya hapo ulipo.
Huyu binti alikwenda kwao kijijini hivi karibuni (na alikuaga), na aliporudi tu ndio hizo njozi zako mbaya zilipoanza.
Kafara lake:
Vunja nazi mbili mbata, weka vipingili viwili vya muwa hapo juu, kata miche saba ya mmea uitwao mvunja-hukumu na uiweke pamoja na hizo nazi na hiyo miwa.
Mishale ya saa saba usiku, nenda njia panda yoyote ile ilioko karibu na makazi ya huyu binti. Weka hili kafara halafu washa miche miwili ya UDI. Wakati unaondoka basi usiangalie nyuma. Matatizo yako yote yatakua kwishney.
Kama ukifanikiwa na nilichokwambia basi wape JF mchango wako sawa na mshahara wako wa mwezi mmoja.
Just kidding folks.
Leo niko kwenye mood nzuri ile mbaya.
Mami kulala chali ni balaa nimeshaota hadi mimi mwenyew nimekufa
Kula vizuri, kunywa maji ya kutosha, oga kwa sabuni sahihii ya kuogea, lalia shuka safi, kitanda kiwe kizuri, chumba kiwe na hewa ya kutosha, na akili iwe na uhakika wa kesho, hata ulale kichwa chini miguu juu huwezi ota ndoto za ajabu.