Jinamizi la wimbo kugoma laitesa TFF | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jinamizi la wimbo kugoma laitesa TFF

Discussion in 'Sports' started by kilimasera, Jan 7, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 7, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  SHIRIKISHO la soka nchini Tanzania, TFF limeunda kamati ya watu watano kuchunguza tukio la kushindwa kupiga wimbo wa taifa kwenye mchezo kati ya Taifa Stars dhidi ya Morocco, Oktoba 9 mwaka jana uliofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

  Rais wa TFF, Leodegar Tenga aliwaambia wanahabari kwenye ofisi za Shirikisho hilo jana jijini Dar es Salaam kuwa licha ya kuomba radhi kwa rais Jakaya Kikwete, wageni waalikwa kutoka Morocco na maelfu ya watazamaji kwa hali iliyojitokeza hawana budi kutoa adhabu kali kwa wahusika na kuhakikisha hali hiyo haijitokezi tena.

  "Hatuwezi kulifumbia macho hata kidogo suala hili la aibu kwa nchi yetu, lazima tulifuatilie kwa kina zaidi na kuwabaini wahusika wa tukio lile," alisema Tenga.

  "Tunawaomba wahusika wote na wadau wa soka nchini kutoa ushirikiano unaostahili kwa wanakamati ili kubaini ukweli kuhusiana na aibu iliyojitokeza na kupendekeza hatua za kuchukua ili tukio kama hili lisitokee tena kwenye medani yetu ya soka," alisisitiza.

  Alisema kuwa kamati hiyo ameipa muda wa wiki tatu kukamilisha jukumu hilo na inatarajiwa kutoa taarifa za uchunguzi huo ifikapoJanuari 31 mwaka huu.

  Kamati hiyo inaundwa na mwanasheria mkuu wa zamani wa Zanzibar na makamu mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya TFF, Hamidu Mbwezeleni ambaye ni mwenyekiti wa kamati hiyo.

  Wajumbe ni Yussuf Nzowa, afisa wa Ikulu na mjumbe wa kamati ya nidhamu TFF, Ahmed Msangi mkuu wa upelezi kanda maalum ya Polisi ya Dar es Salaam, Gasper Mwembezi mkurugenzi wa sera na mipango wizara ya habari, utamaduni na michezo na Zena Chande mhariri wa michezo gazeti la Habari Leo.

  Mambo ambayo kamati hiyo itayafuatilia ni pamoja na kupokea taarifa kwa kamati maalum ya uwanja wa taifa juu ya jukumu la kuhakikisha nyimbo za taifa zinapigwa bila ya dosari yoyote.

  Kuchunguza utekelezaji wa jukumu hilo kwa mujibu wa maelezo ya kamati maalum ya uwanja wa taifa, kuwahoji wote waliohusika na kupata maelezo, kubaini wahusika waliosababisha kutopigwa kwa nyimbo hizo kwa wakati.

  Baada ya kutokea kwa tukio hilo la aibu mbele ya rais Kikwete na balozi wa Morocco, shiriksho la soka nchini TFF lilimsimamisha aliyekuwa afisa habari wake Florian Kaijage kwa kushindwa kutoa maelezo ya kueleweka na kusimamishwa kwa muda usiofahamika.

  Kufuatia tukio hilo TFF ilichukua hatua za dhati kabisa kuhakikisha hali hiyo hatokei tena na kuanzisha utaratibu wa kuweka bendi za Jeshi ama Polisi kwa ajili ya kupiga nyimbo za taifa.

  Katika hatua nyingine TFF kupitia Kamati yake ya Nidhamu imefuta adhabu aliyokuwa akitumikia kipa wa Simba Juma Kaseja pamoja na kumuomba msamaha kwa tukio hilo.

  Mwenyekiti wa kamati ya nidhamu TFF, Alfred Tibaigana aliwaambia wanahabari jana kwenye ofisi za shirikisho hilo kuwa kamati hiyo ilipitia rufaa hiyo na kusikiliza pande zote mbili na kubaini kuwa kitendo hicho hakukifanya kwa makusudi hivyo kamati yake imeamua kutengua kifungo hicho na wamemwachia huru.

  "Kaseja alimtuma wakili wake akidai kuwa hakufanya kwa makusudi bali alijisikia kiu na alivyokwenda kuchukua maji kwenye benchi la timu yake akakuta wachezaji wake ndiyo wanamalizia kuwapa mikono waamuzi wa mchezo huo," alisema Tibaigana.

  Alisema kuwa shirikisho hilo linawataka radhi Kaseja na klabu yake ya Simba kwani tayari alishaanza kutumikia kifungo hicho kwa kukosa mchezo wao dhidi ya Majimaji ya Songea.
   
Loading...