Uko sahihi sana mkuu, ni jina la hovyo sana. Nadhani sababu mojawapo ya upuuzi huu ni lile dude linaloitwa muungano, maana kama ingeitwa kwa moja ya majina ya mbuga zetu au Kilimanjaro, wale jamaa wanaosubiri kuzama baharini wangeiweka kwenye kero za muungano! Haiingii akilini kuwa tuna mlima mrefu kuliko yote Afrika, ziwa kubwa kuliko yote Afrika, Ziwa lenye kina kirefu, mbuga kibao, creta nk lakini timu yetu ina jina la kiajabu hivi.