Wazo zuri, naunga mkono hoja.
Mji huu naona bora uitwe Mzizima kama hapo awali ulivyojulikana. Pia sio mbaya kama ukaitwa Azania
haya lete maoni yako, ndio kweli waafrika tuko hivi haswa kama unavyosema, lakini tufurukute wengine wachache kutafuta makosa yetu au tujichimbie kaburi? mi naona tusichoke kumbuka Rome was not build in a day!Na. Tatu umechemka. Huwezi kusema Bongo wakati watanzania hawastahili. Mfano: 1. Wasomi wengi hufikiria magari tu wala sio namna ya kujenga mtazamo wa kutatua foleni kwanza. 2. Wanapenda sifa zilizojaa mipango dhaifu km kumiliki simu kali wakati huna pa kuishi. 3. Wanapuuzia umuhimu wa kuwa watafiti kwanza (uvivu). Ubongo wetu uko wapi? It is said that the level of social dev. is determined by level of knowledge of people of that society. Hadi hapo Sisi Wabongo na huu umasikini? Acha uvivu, fikiria kabla ya kujenga hoja.
Watanzania wenzangu wenye mawazo mapya na wasiokumbatia kwa itikadi, kwa nini huu mji uitwe jina la kutukuza Sultani wa Zanzibar aliyekuwa anavusha watumwa kutoka kijiji cha MZIZIMA, na kwa jinsi biashara ilivyokuwa laini akaamua kuiita BANDARI YA SALAMA, kwani wazaramo hawajampa upinzani wowote kuichukua watumwa.
nchi ngapi Duniani zimebadili majina ya miji mikuu? au kwa sababu waliooongoza mji mkuu huu ni wazee wajinga wasiofikiri chochote bali ukubwa tu watukuzwe?
au ndio LAANA ya mwafrika inaendelea? nawaombeni kwa Heshima ya Babu zetu walioteswa na kufa, Tubadilishe jina hili la Adui aliyewatesa Babu zetu.
najua mtauliza, ndio, napendekeza turudishe jina lake la kale au tuchague haya:
1 Mzizima, jina lake la mwanzo kabla ya uvamizi wa waarabu.
2 Tanganyika, ili jina kubwa hili lisife, aminini Duniani linajulikana kuliko Tanzania.
3 Bongo, ni jina ambao linamaanisha ubongo wa akili, ni zuri
4 Tanzania, ili endapo muungano utavunjika hili jina lisipotee lishajulikana duniani.
5 Zaramo, wenyeji wa asili.
Naomba mashujaa wa Taifa wachangie.
Hapo kwenye RED siamini kama ni sahihi vinginevyo tuamini hata wewe kuwa na mawazo tofauti na wazee hao basi wewe ni kijana mjinga unayedharau kila kitu cha wazee wako na kuwaza kubadiri kila kitu
sawa Kitumbo, tusifunge mlango na kupigana, mimi narudisha maneno mabaya juu ya wazee walioongoza jiji mpaka sasa, na nina heshima kubwa kwao kwani ni watangulizi, lakini sasa tukubali mabadiliko na mawazo mapya ya kuboresha nchi yetu, unajua Rome was not build in one day? sawa shekhe wangu Kitumbo? naomba radhi kwa maneno ya mwanzo.
unakuwa vigumu hata kwa wanaotangaza nchi nje, kwani ukitaja jina tu la mji, watu wanajiuliza kwani ni arabuni? mbona jina la kiarabu? si nchi yenu iko africa? kidogo inakuwa aibu.