Nchi hii ushabiki umezidi, mara nyingine watu hata hawajui wanashabikia nini? Sijui ni kwa sababu hatuna mafanikio ya kushangilia? Sasa huyu kuwaahidi vijana usafiri ana maana gani? Halafu haya mawazo ya mtu kutaka uongozi kwa kusema atanunua hiki kwa fedha zake, ni lazima aulizwe anazipata wapi?
uaweza kuthibitisha manaeno haya?Akufukuzae hakwambii toka, Sitta muda wako wa kukaa CCM umeshakwisha...your targeted...
Lyatonga naye alibebwa juu juu akaambulia patupu. Labda kama hao waandamanaji wamejiandikisha kupiga kura na watapiga kura hizo. Kama hajawa mbunge tayari anaandamana na magari ya kifahai 30 na mapikipiki 70 anadhibitisha ufisadi wake hata kabla hajakalia kiti. Hamjasikia yule mhindi fisadi wa Tabora analalamikiwa na watu wake kwamba hawamwoni kusikiliza matatizo yake? Mwenye shibe hamjui mwenye njaa. Kwamba Sita aligoma kuhudhuria asitupiwe mawe hata bila kujua sababu yake. Labda hakualikwa?
Umeneno vema mkuu, Watanzania ndio tuliwao. naona na huu ni mradi wa watu fulaniCheap politics!~
watTZ ndo wanapenda hii............nitawanunulieni usafiri.
Jimbo la Urambo leo lilizima kwa maandamano makubwa ya kumpokea kamanda mteule Bwana Ally Maswanya ambaye ni kurugenzi wa kampuni ya Zain kanda ya Ziwa, maandamano hayo yalikuwa na lengo la kumsimika u-kamanda bwana maswanya ambaye pia anatajwa kulinyemelea jimbo hilo.
Maandamano hayo yaliyotanguliwa na msafara wa pikipiki karibu 70 na tax 50 zilizofuatiwa na magari ya kifahari karibu 30. hata hivyo katika hali ya kushangaza Bwana Spika aligoma kuhudhuria sherehe hizo zilifanyika mbele ya jengo la ccm wilaya ya Urambo, habari zaidi zinasema mgeni rasmi katika sherehe hizo alikuwa bwana Edwin sanda (MNEC Uvccm) ambaye alimwakilisha katibu mkuu Uvccm Martin Shigela aliyetakiwa kuwa mgeni rasmi.
akihutubia wananchi wa Urambo Bwana Maswanya ambaye kwa umri bado anaonekana kijana aliwaahidi vijana wa Urambo kuwapatia vyombo vya usafiri baada ya kuona kuwa vijana hao wamekosa mtu wa kuwajali kwa kipindi kirefu
Unataka ushahidi gani Mkuu wakati kila kitu kipo wazi? kaka kuwa targeted si lazima bastola iwe sikioni - ni matendo tu anayofanyiwa huyu kamanda kweli yanaashiria mwisho wa Sitta CCM. na hata akin'gan'gania kubakia humo bado atakuwa na misukosuko mingi sana kuelekea uchaguzi mkuu.uaweza kuthibitisha manaeno haya?
Mkuu kwa Sendeka, lazima apite, jina lake limepanda sana hasa baada ya kushinda kesi ya Millya. Millya pia alikosea alipofuatwa na wazee wa kimila wa kimasai kwa kuombwa suluhu akawatoroka. Hata Askofu naye alimwomba kuwa patana na ndugu yako akakataa pia. Sasa kwa desturi za Kimasai mtoto ambaye hasikii wazazi ni mtovu wa nidhamu. Halafu pia imewachukiza sana baadhi ya Wamasai kwa kitendo kile ambacho kijana inaonekana anatumiwa na kigogo!!!!Unataka ushahidi gani Mkuu wakati kila kitu kipo wazi? kaka kuwa targeted si lazima bastola iwe sikioni - ni matendo tu anayofanyiwa huyu kamanda kweli yanaashiria mwisho wa Sitta CCM. na hata akin'gan'gania kubakia humo bado atakuwa na misukosuko mingi sana kuelekea uchaguzi mkuu.
Kitendo cha UVCCM kukabidhiwa majimbo yote ya hawa wapiganaji kuhakikisha yanachukuliwa na wao ni kitendo tosha kwamba wameshawachoka.
Mtera - Jimbo limekabidhiwa wa UVCCM
Urambo - Jimbo limekabidhiwa wa UVCCM
Nzega - Jimbo limekabidhiwa wa UVCCM
Simanjiro - Jimbo limekabidhiwa kwa UVCCM nk
UVCCM watapata kila support kutoka makao makuu kuhakikisha list hii hapa chini hairudi bungeni kwa tiketi ya CCM
Kwa hiyo, Sintashangaa kutowaona Malecela, Selelii, Sitta, Sendeka, Mwakyembe, Sherukindo, Shibuda kwenye bunge lijalo - ni vizuri tu waanze kujipanga mapema kukabiliana na vita hii ndani ya CCM.