Uchaguzi 2020 Jimbo la Siha kurejea upinzani tena

Feb 26, 2014
22
17
Jimbo la Siha Kurejea Upinzani Tena

Maamuzi ya Kamati Kuu ya Chama yanasubiriwa kwa shauku kubwa sana, Kila mwananchi anatamani kusikia jina linalorudi kutoka Dodoma.

Leo nitazungumza kuhusu hili Jimbo langu la Siha, Jana nilieleza kuhusu Arusha Mjini,Arumeru Magharibi na jinsi Chama kitapata Ushindi.

Jimbo la Siha na Hai ushidi ni Kamati Kuu kuleta jina wanalolihitaji zaidi wanananchi.
Leo tuzungumze Siha.

Siha kwa sasa imesikika sana katika siasa
Kunasiri katika Jimbo hili na ni mtego Mkubwa kwa Chama chetu cha Mapinduzi.
Kwanza ni aina ya tofauti ya Kura zilivyokuwa nitakuja kueleza
Pili ni Aina ya Eneo la kijographia katika Jimbo hili.
Tatu
Uwezo wawagombea na uhitaji wawananchi.

Tukianza na tofauti ya kura, toka kuanzishwa kwa Jimbo la Siha hapajawahi kujitokeza wagombea wengi kama mwaka 2020
Wagombea walikuwa wengi na kulifanya Jimbo kuchangamka.

Idadi hii ya watia nia inaweza ikawa ilichagizwa na moja aina ya Mbunge aliekuwepo Mh Dr Mollel au aina ya mahitaji ya wanachi katika mfumo wa siasa

Unajuwa wanachi wakiona Mbunge ajafanya kitu, mtu anachukuwa fomu nae akisema kama yule ameweza kuwa Mbunge hata Mimi naweza kuwa Mbunge maneno hayo huchochochea sana idadi kuongezeka.

Mwaka 2017 baada ya Mollel kuondoka Chadema na kurudi ccm yapo mambo makubwa wananchi waliyategemea sana katokana na yeye kuhamia Mapinduzi

Waliweka matarajio makubwa katika ahadi za Aridhi zilizotolewa na viongozi,.Matamarajio katika Afya Elimu nk.

2020 tuliona utitiri Mkubwa sana wawagombea na utitiri huo ulichagizwa na Mwanry Mollel huku Vijana wasikuwa na majina Makubwa mwenye Media kusikaka jimboni

Mollel 148 huku akifuatwa na Mzee wa Sukuma Ndani Mwanry aliambulia kura 147
Tumsifu Kweka 53
Eunice Mmari 37
Meijo Laizar 8
Filbert Mwacha 3

Nje na Jimbo la Siha watu walimuona Mwanry ni tishio na atahinda sana wakasahau wanachi wahuku Siha hawako kama walivyokuwa wanafikiri

Ukiwa Lawate Nasai Ivany ukimzungumza Mwanry wanamuweka katika kundi la mbinafsi hivyo wanasiha wanamjuwa sana mtoto wao toka 1996 akiwa kiongozi.

Mollel wengi walimuweka katika kundi la kukosa kutokana na aina alivyoonekana njee ya siha
Ukiwa Karansi Ngarenairobi ukimtaja mtuu huyuu kwa wanachi watakwambia hafai hafai ikiuliza zaidi utasikia sio mkweli na,Ila utajiuliza alizipataje zile kura,ndio utaelewa bado wajumbe sio watu wazuri

Wajumbe waliwakilisha hisia zao au walishawishiwa nirahisi kushawishi wajumbe ila sio wananchi.

Mollel hata baada ya Unaibu Waziri wengi waliona angetikisa sana kumbe wajumbe walikuwa na jambo lao.
Ubunge wake Unaibu wake asingepata zile kura kama ninavyowaelewa watu wa Siha

Mwanry na kelele zote zile bado alijikuta namba mbili.
Nakusema Kuto Nimetumwa,Mimi nimeteuliwa bado wajumbe wakafanya yao.

Siha itazamwe kwa upekee wake, Tofauti na Majimbo mengine utaona Mshindi wakwanza hadi watano walivyochuwana katikati ya Manaibu Mawaziri wawili na wote wakiwa wamepewa nafasi hizo na Rais

Sio kwamba wamekata kusikiliza kauli au kumuelewa Rais hapana wanaangalia mtuu atakaewavusha na atakae fanya kazi na jamii bila ukabila.


Leo kuna Kundi la Mwanry na Mollel
Ukikaa karibu na wananchi utawasikia wakiwakata wote hao wakisema "Afadhali Mshindi wa tatu wanne hata watano kuliko hao watu wawili
Wanasema
Mshindi wa 3,4,5 hata uongozi wawanachi wajashika ila wamekuwa karibu na jamii na wala kura zao zinapatikana tuu bila shida.

Upinzani Siha wao wanashangilia Ujio wa Mwanry na Mollel ukiwasikiliza na kuwauliza nani ambaye akija ni rahisi kushindwa utasikia
Mollel na Mwanry hao mchana kweupe nenda Kirua nenda Ngarenairobi nenda Makiwaru zunguka kata 17 utaona wapi kwanini wapinzani wanashangilia.

Wapinzani hawataki kabisa kusikia habari ya Mshindi wa Tatu Wanne wala watano

Ngoja niwaeleze kwa kifupi Mshindi wa Tatu NNE na Tano.

Tumsifu Kweka Kura 53
Ni mkazi wa Sanya Juu amekulia Sanya Juu moja ya kata kubwa kwa idadi ya wapiga kura
Ameshiriki majukumu mengi ya Kijamani,amekuwa akishirikia kazi nyingi Moja niile aliyoshiriki ya Ujenzi wa Shule ya Namwai Makiwaru Sanya Day Fuka na hospital kazi hizii zimempatia jina sana, Kesi za Masikini wanao onewa amekuwa msaada Mkubwa sana kwao, Kinachombeba katika jamii ya wafugaji ni wakati Baba yake akiwa Polisi Sanya Juu aliwasaidia sana Jamii hiyo,katika mifugo,
Japo nae ameonekana akiwa karibu na wananchi ila nimtu Fulani hivi anatajwa kama mpole na msikivu


Eunice Mmari
Yeye amekulia Nasai kwa maelezo ya fomu yake ya kuomba ridha Changamoto kubwa hafamikii sana na ushawishi wake ni mdogo ila ni Mgombea mzuri akiwekewa mazingira ya Ushindi
Alipata kura 37 na kushika namba nne.
Kitakachomtesa Mgombea huyuu ni kwamba aishii Siha ameolewa Dodoma hapo ndio mziki ulipo.

Meijo Laizar huyu ni Kijana wa Chama amekoma ndani ya Chama, siasa zake huitwa siasa za kitume amekuwa mnyenyekuvu Mkubwa kwa Chama na watu wake, Ameshika nafasi nyingi sana ndani ya Chama
Chama kikimleta basi watakuwa wamleta mtuu sahihi pia kwa wakati huu hana Makando makando,useme utayasema.
Meijo Laizer alipata kura nane 8

Filbert Mwacha huyuu ni kijana wa Chama, amepata kura 3 ni mtumishi wa Halmashauri kinachomtesa ajakulia hapa Siha na kibaya zaidi tuhuma za Hospital zimelekezw kwake

Kazi ni Kamati Kuu kuangali katika hayo majina.
Kamati ya Siasa Wilaya waseme Ukweli.Mkoa nao waseme Ukweli,Mkuu wa Usalama nae asemw Ukweli juu ya hili.

Upinzani unavyoshamiri Siha nidhahiri Mgombea dhaifu atakitesa Chama zaidi tutawapa wapinzani ajenda yakusema.
Kesho ni Hai.
 
Kuna watu walidanganywa ndani ya miaka hii 5 ya wao kuongea peke yao eti upinzani utabakia na mbunge mmoja.....

Kampeni bado...mziki munene wa Lissu wameanza kuhangaika....na bado kina Mdee, Bulaya, Mantiko, Heche, Mbowe, Mnyika, Sugu, Msigwa, Lema na Prof.....

Mmekwisha!!
 
We ukabila wa kichagga ndio inakusumbua mnafiki wewe...kawadanganye wajinga..kwani Mollel akipata si anatekeleza ilani ya chama cha mmapinduzi kwa wananchi wa siha..hata hao unaowatetea hawatakuja na ilani zao.

Changamoto ambazo zipo SIHA ni za kusemea ndani ya bunge..na hakuna mbunge anayekuja na pesa zake.
 
Uko hata msijisumbue, atashinda mpinzani na atakuwa wakwanza kununuliwa na ccm
 
Kuna watu walidanganywa ndani ya miaka hii 5 ya wao kuongea peke yao eti upinzani utabakia na mbunge mmoja.....

Kampeni bado...mziki munene wa Lissu mmeanza kuhangaika....bado kina Mdee, Bulaya, Mantiko, Heche, Mbowe, Mnyika, Sugu, Msigwa, Lema na Prof.....

Mmekwisha!!
Maskini wanaweweseka
 
Kuna watu walidanganywa ndani ya miaka hii 5 ya wao kuongea peke yao eti upinzani utabakia na mbunge mmoja.....

Kampeni bado...mziki munene wa Lissu mmeanza kuhangaika....bado kina Mdee, Bulaya, Mantiko, Heche, Mbowe, Mnyika, Sugu, Msigwa, Lema na Prof.....

Mmekwisha!!
Maskini wanaweweseka
 
Kuna watu walidanganywa ndani ya miaka hii 5 ya wao kuongea peke yao eti upinzani utabakia na mbunge mmoja.....

Kampeni bado...mziki munene wa Lissu wameanza kuhangaika....na bado kina Mdee, Bulaya, Mantiko, Heche, Mbowe, Mnyika, Sugu, Msigwa, Lema na Prof.....

Mmekwisha!!
Hao uliowataja possibility ya kupenya ndogo Sana.
 
Majimbo yote ya mkoa wa Kilimanjaro na kata zake, CCM unatakiwa owe makini kupata wagombea Safi na wanaokubalika.vinginevyo 2025 upinzani utarudi upya,na 2022 uchaguzi wa chama tawala utakuwa wa rushwa tupu.
 
Majimbo yote ya mkoa wa kilimanjaro na kata zake, CCM unatakiwa owe makini kupata wagombea Safi na wanaokubalika.vinginevyo 2025 upinzani utarudi upya,na 2022 uchaguzi wa chama tawala utakuwa wa rushwa tupu.
Sio kweli kati ya jimbo ambalo ccm itashinda kwa kishindo ni same mashariki Anne kilango anakubalika sana
 
Mwanri anashinda asubuhiii,japo mollel katumia umbali wa mwanri na Jimbo la siha ktk kutengeneza mtandao kwa wajumbe,Ila potential player ni mwanri tu,na mollel alishinda hapo Siha kwa upepo wa CHADEMA NA LOWASSA 2015 TU
 
Mzee wa Toronto ange gombea Toronto ange shinda kwa kashinda.
 
Kuna watu walidanganywa ndani ya miaka hii 5 ya wao kuongea peke yao eti upinzani utabakia na mbunge mmoja.....

Kampeni bado...mziki munene wa Lissu mmeanza kuhangaika....bado kina Mdee, Bulaya, Mantiko, Heche, Mbowe, Mnyika, Sugu, Msigwa, Lema na Prof.....

Mmekwisha!!
Maskini wanaweweseka
 
Ningekuwa mimi, na nafikiri hili linaangaliwa pia na KK, mgombea anayetetea kiti chake akipishana kura chache sana na mshindi wa pili definitely mshindi wa pili ana influence kuliko yeye. Mengine tusubiri KK.
 
Back
Top Bottom