Jimbo la Nyamagana kurudi CCM-2015

Jimbo la Nyamagana kurudi CCM-2015

Nipo mwanza takriban miaka 2 ccm kurudisha jimbo la nyamagana ni sawa na fisi kusubiri mkono ukatike wananchi wa nyamagana kwa ujumla wanamkubali mbunge wao wenje
 
Wala si mihemuko km unavyodai shilatu na dialo ni walewale so kwa sasa mwanza hata umulete mwenyekiti wa chama cha ccm taifa asimame hata na mwanachama wa kawaida kabisa wa chadema kwenye jimbo la nyamagana au ilemela lazima mwenyekiti atashindwa labda kura zichakachuliwe

pole yako ndomana na kwambia mihemko hiyo,tusibishane sana let us wait 2015 sio mbali,Mungu akitujalia uhai tutakuja hapa kuyathabitisha tunayosema
 
Unapoandika vitu vijavyo weka na neno kama mungu akimuweka/akituweka hai hadi hiyo 2015 unajuwaje kama hao wote unaowataja ikiwemo mimi na wewe kama tutafika hiyo 2015
Trueeeeeeeeeeee,huyu jamaa,ajui jins mwanza ilivyoooo,mwacheni awepi watu moyo.:kev:
 
Ccm, shllatu? Mwz wapi na wapi? Kamwambie shilatu avae viatu kwanza mwz ni cdm tu. Kama unabisha njoo mwaloni usikie mwenyewe.
 
Shilatu yule Raphael nimjuaye au mwingine? Kama ni Raphael Shilatu wa Buhongwa binafsi nasema "NO" tena BIG NO! Huyu bwana tuangalie alipo na alichofanya kwa watu anaowaongoza.....ni afisa uhusiano wa Sahara Media ambayo ni kampuni mama ya RFA,KISS FM&STAR TV ukiachilia mbali uenyekiti wa CCM Nyamagana alouchukua juzi hata impact yake bado hatujaijua hivyo hatuwezi kumzungumzia kupitia uenyekiti huo. Kwa Sahara media kakalia hicho kiti miaka ya kutosha, sasa je,ameweza kuongoza Sahara kwa uzuri na akwawa fair kwa mwajiri na waajiriwa wenzake? Majibu hapa yako wazi kabisa,huyu bwana ni wale bendera fuata upepo....amenyanyasa sana waajiriwa wa Sahara Media kwa kuwafurahisha mabosi wake. Huyu anaekuja na singo ya Raphael Shilatu anapendwa sana na wana Nyamagana, sina uhakika na anachosema. Huyu bwana tuna historia yake tu vizuri toka alivyokuwa mwalimu baada ya kutoka Butimba TTC alipewa shule moja kule Bwiru ikiwa chini ya bodi ya mamlaka ya shule za wakulima mkoani Mwanza enzi hizo,alichofanya ni kituko...Sina uhakika kama wana CCM wanaangalia tu ukabila na si utendaji kazi wake. Waende Sahara waulizie utendaji kazi wake mkubwa huyu halafu wajiridhishe kama kweli watakuwa wamepata the right candidate. Upande wa Wenje sina uhakika na alichosema aliepost uzi huu,amemsifia kuwa amekuwa ni mtetezi wa wanyonge halafu tena akasema CDM hawawezi kutetea jimbo! Tunataka mbunge gani kwani!? Mtetezi wa mabosi kama Shilatu au mtetezi wa wanyonge kama Wenje?
 
kama unatumia kichwa kufugia nywele pekee kama ww lazima ushindwe kujitambua

Mkuu mi nipo hapahapa mwanza, nipo mwanza kwa zaidi ya miezi 8 sasa naijua vizuri sana mwanza, any way hapa mimi siyo CCM wala Chadema wakuu maana naona watu wamechangia kwa misingi ya vyama vyao badala ya uhalisia, halafu mimi natoka jimbo la Rorya la Lameck Airo na nimezaliwa hapo hapo na kusomea Rorya, naijua fika, Bado hajafanya kitu, hata kama ana pesa hawezi kujenga barabara za lami kwa pesa zake! hoja hapa ni kuwa azungumze bungeni tu hizo kero za wananchi sasa serikali itekeleze isitekeleze ni jambo lingine ila cha msingi azisemee bungeni!!

Wale waliokaribu naye wamshauri kuwa angalau awasilishe hoja hizo bungeni ikiwa ni maji, barabara na umeme, Mbunge wangu ongea tu bungeni au basi hoja hizo kama unaogopa kuongea wewe mpe Mbunge wa Tarime akusaidie kuzisemea!! ni wazi kuwa kwa pesa zako mwenyewe huwezi kujenga barabara za lami! huwezi kuvuta maji toka sota au kinesi au sonjo au Nyangabho na kuyasambaza jimboni humo! utafilisika!!

Haya ndio maswali ninayokuomba uulize bungeni mara tu bunge litakapoanza:

Mh. Spika, naomba kumuuliza waziri wa ujenzi kuwa, ni lini barabara ya Mika-kinesi, mika-shirati, na mika-sonjo zitajengwa kwa kiwango cha lami,

swali la nyongeza, Naomba uwahakikishie wananchi wangu rasmi leo kuwa ni kweli bajeti ijayo barabara hizo zitatengewa fedha. Tayari umemaliza kazi yako mbunge wangu kaa.

hivo hivo kwa Maji na Umeme!!
 
Huyu naye ni kibaraka.Kwa akili yake ndogo anadhani kwa maisha mabovu ccm iliyowasababishia watanganyika itasalimika?
 
Dhuluma,ufisadi na danganya toto hatutaki tena, Chadema ni chaguo la wananyamagana,Mnakula na kumwaga huku watanzania wanahuzunika....kamwe haturudi nyuma, ila jifarijini kwa namna hiyo,M4C DAIMA.
 
Awe Shillatu,Mabula au Kahungwa wote hao kwa Wenje sijui.

Nawashauri mkawaulize Masha,Ndikilo na Mkurugenzi Kabwe.

Ila Shilatu na hao jamaa zake kwa kuhudhuria misiba ya makada wao nawasifu. Sijui wanafurahia wapiga kura wao kupungua? Maana akifa mtu ambaye sio mwanaccm huwaoni kabisaaaaa.

Kaaazi kweli kweli akili ndogo kuongoza.
 
mkuu mi nipo hapahapa mwanza, nipo mwanza kwa zaidi ya miezi 8 sasa naijua vizuri sana mwanza, any way hapa mimi siyo ccm wala chadema wakuu maana naona watu wamechangia kwa misingi ya vyama vyao badala ya uhalisia, halafu mimi natoka jimbo la rorya la lameck airo na nimezaliwa hapo hapo na kusomea rorya, naijua fika, bado hajafanya kitu, hata kama ana pesa hawezi kujenga barabara za lami kwa pesa zake! Hoja hapa ni kuwa azungumze bungeni tu hizo kero za wananchi sasa serikali itekeleze isitekeleze ni jambo lingine ila cha msingi azisemee bungeni!!

Wale waliokaribu naye wamshauri kuwa angalau awasilishe hoja hizo bungeni ikiwa ni maji, barabara na umeme, mbunge wangu ongea tu bungeni au basi hoja hizo kama unaogopa kuongea wewe mpe mbunge wa tarime akusaidie kuzisemea!! Ni wazi kuwa kwa pesa zako mwenyewe huwezi kujenga barabara za lami! Huwezi kuvuta maji toka sota au kinesi au sonjo au nyangabho na kuyasambaza jimboni humo! Utafilisika!!

Haya ndio maswali ninayokuomba uulize bungeni mara tu bunge litakapoanza:

Mh. Spika, naomba kumuuliza waziri wa ujenzi kuwa, ni lini barabara ya mika-kinesi, mika-shirati, na mika-sonjo zitajengwa kwa kiwango cha lami,

swali la nyongeza, naomba uwahakikishie wananchi wangu rasmi leo kuwa ni kweli bajeti ijayo barabara hizo zitatengewa fedha. Tayari umemaliza kazi yako mbunge wangu kaa.

Hivo hivo kwa maji na umeme!!

kwani mlilazimishwa kumchagua??? Mchagueni tena labda atajenga barabara za juu ,na mabomba yatatoa maziwa,,,,,,,,unamfundisha mbunge kazi??? Kura yako kwa chadema ndio jibu la matatizo ya wananchi wa rorya
 
Huyu naye vipi? Ni Nyamagana gani hiyo anayoingelea? Masha na huyo Shilatu ni nani jembe? acha kuweweseka wewe,Nyamagana usiilinganishe na Nzega kwa Kigwangala!
 
Inaweza kuwa kinyume chake; Nyamagana ikabaki hapo ilipo na hilo la Rorya nalo likaondoka.
 
Watu wa mwanza ni watu makini sana,,,kama kura zingekuwa gari basi lawrence kego masha angekuwa mbunge mpaka sasa,,wanaangalia ni chama gani kina sera nzuri zinazotetea wanainchi,,,mpaka dakika hii,,mh wenje bado hajapata hata wakuthubutu kumnyanganya jimbo la nyamagana.
 
Sasa imethibitika rasmi kuwa Jimbo la Nyamagana jijini mwanza litarudi CCM bila kupepesa macho, taarifa za ndani ya CCM na

Chadema zinatanabaisha kuwa Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Nyamagana ndugu Raphael Shillatu atagombea na anaungwa

mkono sana na wananchi wa jimbo hilo, habari za kina zinaeleza kuwa tayari Mbunge wa Nyamagana amepata taarifa hizo na

ameamua kwenda kugombea Jimbo la Rorya mkoani Mara ambalo nalo Mbunge wake wa sasa Ndugu Lameck Airo

amenukuliwa

mara kadhaa akisema kuwa hatagombea tena Ubunge mwaka 2015 anataka akae atulie asimamie biashara zake. Kwa ujumla,

kwa wale wanaomfahamu ndugu. Raphael Shillatu watakubaliana nami kuwa ni mtu wa watu, mpole na msikivu sana hapa

simpigii debe ila ukweli utabaki kuwa ukweli, Ndugu Wenje ni mzuri kwa maana ya kupigania maslahi ya wananchi wake huyu

kila mmoja anamfahamu na ameona kazi yake, huyu Airo kwa ujumla ameshindwa, ameshindwa kuzungumza bungeni juu ya

matatizo lukuki ya Rorya, Jimbo la Rorya kwa ujumla lina barabara kuu tatu, barabara ya MIKA-KINESI, MIKA-SHILATI, na

MIKA-SONJO au NYANGABHO. Lakini cha kushangaza hazina lami, lami imeishia Utegi hapo, Umeme kidogo upo ila baadhi ya

maeneo kama Utegi, shirati, kowack, buturi na huu umeme ameukuta! ameshindwa kuwasilisha kilio cha wananchi wake

kuwa umeme usogezwe katika maeneo ambayo haujafika kama Kuutoa NYAROMBO na kuupeleka MANILA, MUHARANGO,

NYAMAGARO, NYANGABHO, NA SONJO!! yeye amejitahidi kutoa mabati katika shule mbalimabli jimboni humo, Maji nayo

ameshindwa kujenga hoja bungeni ili serikali iangalie uwezekano wa kupeleka maji, cha ajabu toka aingie Bungeni ameuliza

au kuchangia mara moja tu, maswali mengine amekuwa akimpa mbunge wa tarime Nyambali Nyangwine amsaidie kuuliza.
Kajifunze kuandika vizuri, kiini cha habari yako mara kinageuka ghafla na kumuongelea Lameck Airo. Mbona sisi tunaoishi hapa mjini hatukijui hicho kitu na huyu Shilatu ndo nani hapa Mwanza? Utamchagua wewe mwenyewe na Maccm wenzio, hebu jipeni moyo hii ndo Mwanza bwana.
 
Mleta mada naona ni jinsi gani alivyo na mpango wa kuwagombanisha maccm ya Nyamagana hapa Mabula hapa Shilatu wapi Masha
 
Back
Top Bottom