Jimbo la Muheza bila CCM inawezekana

Jimbo la Muheza bila CCM inawezekana

MLINGANO

Member
Joined
Nov 26, 2013
Posts
15
Reaction score
2
JIMBO LA MUHEZA.

Kwanza ya yote napenda sana Kutoa poleza dhati kwa Wana_UKAWA wote na wapenda mabadiriko kuondokewa na mwenyekiti mwenza bwana #EMANUEL MAKAIDI M/mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi amina.Napenda pia kutoa Pongezi kwa Makamanda wote wanaoelimisha wananchi juu ya mabadiriko ya kweli na ujio wa #Tanzania Mpya.

Dhumuni Langu Ni kuongelea JIMBO LA MUHEZA mkoani Tanga. Mimi ni mwanaharakati wa mabadiriko ya kweli na Ninashiriki kikamilifu katika kuleta ukombozi kwenye wilaya yetu. Hapo Zamani wilaya hii ilikuwa ni vigumu sana kusikia Kama kuna Upinzani wa kisiasa , Siku zote CCM ndio makao yao makuu na kwenye uchaguzi wowote ule ilikuwa ni lazima Hawa Jamaa washinde. Jimbo hili limeongozwa na CCM Kwa muda mrefu na ahadi nyingi sana lakini mpaka sasa hivi hakuna kitu kilichofanyika.

Mfano katika mkoa wa Tanga wilaya ya Muheza ni miongoni mwa wilaya zinazoongoza kwa vyanzo wa Maji lakini cha ajabu Wananchi wanakosa maji na Maji ya wilaya ya muheza yanapelekwa Tanga mjini pamoja na maeneo mengine huku barabara ni mbovu sana. Wilaya inakosa barabara za lami na kweli kuna matatizo mengi.

Uchaguzi wa sasa.

Mwanzoni katika harakati zangu niliona kama CCM wanaweza tena kutetea Jimbo hili la wilaya ya Muheza kwa sababu wa Umaarufu wa #Balozi Adadi kwenye Kampeni zake na support anayopata kutoka kwa wanasiasa na watu wenye fedha kutoka mikoani.

Lakini Kweli vijana na wazee pamoja na wakina mama wanataka mabadiriko. Huyu mgombea wa CCM Balozi adadi katika kipindi kifupi kwenye Kampeni yake mambo yamebadirika. Huyu alikuwa ni polisi na amekuwa mtu wa kufanya mambo kwa kutumia nguvu sana ya Polisi.

Juzi takribani vijana 20 walikuwa maeneo ya kwake huku wakiimba nyimbo za chadema na kumsema vibaya juu ya ufisadi lakini sababu huwa anatumia nguvu alichofanya ni kutumia askari kwenda kukamata vijana mmoja mmoja kila nyumba. Hii ni siasa na inahitaji uvumilivu.Katika hali hiyo watu wengi wamemtoa Balozi Adadi akilini kabsa.

Huwa ana jazba,ana maamuzi ya hasira na pupa na kuwatumia askari vibaya kabla ya hata Hajawa Mbunge.
Mgombea wa CHADEMA-UKAWA Bwana Peter # Msingwa. Hapo mwanzo watu walikuwa hawakumuelewa ila Bwana msigwa hakukata tamaa.

Huyu ndiye mwanaharakati wa kweli Jaman. Amepiga Kampeni nyingi akiwa pekee yake bila #SUPPORT kubwa mpaka watu wamekuja kumuelewa vizuri kabsa. Katika Kampeni zake wananchi ndio wanamchangia fedha kwa sasa katika kutafuta mabadiriko ya kweli. #Lowassa alipita Jimbo la muheza lakini hawakupata muda wa kumpigia kampeni.

Wananchi ya wilaya ya Muheza kwa sasa wanataka Mabadiriko na upepo umebadirika kwa Balozi Adad. Juzi nilikuwepo kwenye Mkutano wa Mgombea Udiwani wa kata ya Genge katika wilaya ya Muheza – Yani watu walikuwa ni wengi sana kama mkutano wa Mgombea urais . Hii Yote inaonyesha watu wako tayari kwa mabadiriko.

Ushauri wangu
Kwa kuwa wananchi ya wilaya ya Muheza wameshakubali Mabadiriko sasa ni wakati Wa chama cha Chadema/Ukawa kwa ujumla kutuma wanamabadiriko kuja wilaya ya Muheza ili waje kuongeza Nguvu ya mabadiriko.

Huyu Mgombea Ubunge Peter Msingwa anahitaji support kubwa sana ndugu zangu wa wana ukawa. Yeye pekee yake hawezi kushinda. Mfano #Godbless _Lema na #Joshua _Nassari Majimbo yao yana uhakika Nawaombeni sana mje huku MUHEZA Kuja kuelimisha watu Jamani. Watu tayari wapo kwenye mstari.

Uzuri Ubunge wa Arusha Mjini umesogezwa Mbele sasa LEMA kuliko kuwapigia kampeni Madiwani ni bora pia uje kumpa msaada ndugu Peter msigwa katika Jimbo la Muheza.

Narudia Tena Naomba sana UKAWA na Makamanda wote Tujaribu kupeana Taarifa hizi hadi ziwafikie wahusika wakubwa . Yoyote mwenye ukaribu na #Joshua Nassari ama #Gobbless Lema aweze kufikisha salamu hizi.

JIMBO LA MUHEZA BILA CCM INAWEZEKANA.
Mimi wako
kmarishaa@yahoo.com
 
Kaka Msigwa huyu si yule wa Iringa. Huyu Ni wa Muheza. Unashangaa majina kufanana?]
 
Ahsante kwa update kamanda,naamini timu ya kampeni kupitia katibu na mwenyekiti wake wamekusikia,soon Battalian itashuka muheza kumpa support mh Msingwa na hahika Muheza itakombolewa.

Viva Ukwa Viva Lowasa Viva Msingwa Viva Ascerta.
 
Back
Top Bottom