Jimbo la Mbinga mashariki

Oremus

Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
46
Reaction score
9
Mimi ni mkazi wa Mbinga ninaomba kuchukua nafasi kumkumbusha Mbunge wetu Gaudance Kayombo, hadi sasa hakuna ahadi aliyoitimiza hata moja tangu uchaguzi wa mwaka 2010 uishe,yeye hukaa dar tu na ametusahau kabisa huku Mbinga.
Namuomba mheshimiwa atimize ahadi zote alizo tuahidi wana Mbinga, akumbuke 2015 sio mbali asije akaanza kutafuta mchawi.
Mbinga tuna utajiri mkubwa wa Madini,Kahawa, n.k lakini bado tuko kwenye lindi la umasikini,na hii ni kutokana na tabia ya viongozi wetu kukimbilia dar sisi wenyewe wananchi tukiachwa hoi.
 
Poleni sana , kwani alipita bila kupingwa au mlibahatika kuwa na wagombea wengine ? Mtamchagua vipi mkazi wa DSM ? Namkumbuka alipokuwa anatoka mapovu baada ya neno DHAIFU kutamkwa rasmi bungeni , Mmevuna mlichopanda .
 

unakumbuka mchango wake wa mara ya mwisho bungeni ? Je kati yake na komba nani ni nafuu ?
 
unakumbuka mchango wake wa mara ya mwisho bungeni ? Je kati yake na komba nani ni nafuu ?





Hakuna mwenye nafuu wote ni tatizo kwa Mbinga
2015 tunatakiwa kufanya mabadiliko makubwa
 
Ndugu zangu wana Mbinga achaneni na dhana ya kuishi kwa ndoto na ahadi za Wabunge, mnapaswa kubadilika, ni mweli Mbinga imejaa utajiri lakini wana mbinga ni masikini, mmenyimwa haki ya kuujua ulimwengu unavyokwenda, halafu wasomi wa Mbinga wamejaa ubinafsi mkubwa, mwisho acheni ushirikina, uchawi Mbinga umepamba moto, mambo hayo yanawarudisheni sana nyuma kimaendeleo, ingawaje mbunge pia hamna, namfahamu huyu mheshimiwa nadhani inatosha tuunganishe nguvu tuiufue Mbinga yetu
 
Mlipomchagua mlituuliza?

Labda cha kuwasaidia ni kwamba mchagueni mara nyingine ili atimize ndoto zake au mlitaka kutajirika kwa miaka mitano tu?
 
Hao watu wanawatumia wana mbinga kwa kujipatia vipato
hebu badirikeni ndugu zangu chagueni hata mawe kuliko kuwachagua hao hasa huyo kayombo hafai
hawezi kuwawakilisha huko ni nyumbani kwangu lakini anachokufanyieni huyo mbuge ni kama ninyi ni wanyama

kwani hiyo wilaya ni Tajiri sana hasa jimbo lake lina mkaa wa mawe lakini yeye kazi yake ni kupiga deal tu
apate yeye badirikeni ndugu zangu.
 
Mbinga ni vichekesho sana hasa kule Hagati, mbangamao, litembo, nyoni, mikaranga, ugano, myangayanga, matiri, kilimani na sehemu kibao hasa mbinga mjini mitaa ya msimbazi, tank la maji na lusonga kuelekea mkwaya noma sana.
 
Nilikuwa Mbinga mwezi December nikakuta wenyeviti wa mitaa wanawatumia RAIA namba Fulani hivi kuwa ikipigwa wasipokee eti ni namba ya UKAWA ni watu wabaya sana.niliona kichekesho sana na nikaona kuna haja kuwa sana ya kufanya mabadiliko then komba alipita kwa nyimbo zake tu bila Sera yoyote sasa maendeleo yatatoka wap?hadi sasa sijajua msaada unaowafaa Ndugu zangu wa Mbinga na waliosoma kiukweli ni wanafiki sana na wana wivu sana na maendeleo ya wengine.ccm mbinga ndio mungu wao
 
Poleni watanzania wenzangu, polen wana mbinga
Silaha iliyobora ya kushinda ujinga ni elimu, wekezeni kwenye elimu, amjachelewa peleken watto shuleni.
 

Comrade Oremus; Aliyelala usimuamshe; ukimuamsha utalala wewe!! jipangeni muingie kazini kuleta mapinduzi ya fikira na maendeleo hapo Mbinga; Kayombo karidhika; umesahau Escrow; labda alipata mgao Ma_B!!

Mtindueni; akija kuzinduka atakuta mtoto si wake tena, keshachukuliwa. Go go Oremus!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…