Jimbo la Kawe ni Moto wa Kuotea Mbali

SOCIOLOGISTTZ

JF-Expert Member
Jun 16, 2013
2,615
925
Mimi napenda kulipongeza Jimbo la Kawe kwa mambo mbalimbali ya kimaendeleo
walivyojipanga baada ya Uchaguzi Mkuu 2015. Kuna madiwani wachapa kazi sana wakiongozwa na Mmbunge wao Rais wa Marais Kamanda Halima Mwana wa Professor James Mdee. Rais wa marais ameshazungukia kata mbalimbali za Jimbo la Kawe kwa mambo mawili (1) Kuwashukuru wapiga kura kwa kumchagua tena kwa kishindo lakini (2) kusikiliza kero za wananchi. Sasa kati ya kero ambazo alizisikiliza zimeanza kufanyiwa kazi na madiwani wa CHADEMA kwa maagizo yake. Pamoja na figisufigisu za kisiasa kwenye jimbo hilo lakini Rais wa Marais anapiga kazi usiku na mchana kuhakikisha ahadi alizozitoa kwenye kampeni anazitimiza 150%. Wote tuungane kumpongeza Rais wa Marais Kamanda Halima. Viva CHADEMA, Viva Kamanda Halima, Viva Madiwani wa UKAWA.
 
Nimekuambia amefanya mambo mawili
1. Kushukuru wapiga kura
2. kusikiliza kero za wananchi na (b) yake Kero zimeanza kushughulikiwa na madiwani kwa maagizo ya Rais wa Marais.
 
Mimi napenda kulipongeza Jimbo la Kawe kwa mambo mbalimbali ya kimaendeleo
walivyojipanga baada ya Uchaguzi Mkuu 2015. Kuna madiwani wachapa kazi sana wakiongozwa na Mmbunge wao Rais wa Marais Kamanda Halima Mwana wa Professor James Mdee. Rais wa marais ameshazungukia kata mbalimbali za Jimbo la Kawe kwa mambo mawili (1) Kuwashukuru wapiga kura kwa kumchagua tena kwa kishindo lakini (2) kusikiliza kero za wananchi. Sasa kati ya kero ambazo alizisikiliza zimeanza kufanyiwa kazi na madiwani wa CHADEMA kwa maagizo yake. Pamoja na figisufigisu za kisiasa kwenye jimbo hilo lakini Rais wa Marais anapiga kazi usiku na mchana kuhakikisha ahadi alizozitoa kwenye kampeni anazitimiza 150%. Wote tuungane kumpongeza Rais wa Marais Kamanda Halima. Viva CHADEMA, Viva Kamanda Halima, Viva Madiwani wa UKAWA.
Rais wa Marais ???? Wewe una jambo. Unataka kuchukua mzigo nini?
 
IMG-20160128-WA0059.jpg
IMG-20160128-WA0060.jpg
IMG-20160128-WA0062.jpg

Haya Baadhi ya Kazi zinazofanyika kwenye Jimbo la Kawe, Hapa ni diwani wa kata ya wazo akisimamia uchimbaji wa mitaro pamoja na ujenzi wa Culverts ili barabara zipitike muda wote na wananchi waweze kujishughulisha na shughuli za Kiuchumi. Diwani wa Wazo ni ni Mheshimiwa Joel Mwakalebela.

Haya wenye swali la nyongeza?
 
Halima Mdee ni mmoja wa wale wanaosusa na kutoka nje, waliompigia kura hawakumtuma kususa na kutoka nje ya ukumbi wa Bunge. Kapigiwa kura na watu wa kila aina, kuna wavuvi, maprofesa, wanasheria, madaktari na makundi mengine. Anapoanza kuropoka hovyo kabla hajaruhusiwa kwa mujibu wa sheria, anawadharaulisha wapiga kura wake ambao ni wengi sana. Anapotoka nje ya ukumbi wakati bunge linaendelea, anawadharaulisha wapiga kura wake. Hakutumwa kwenda kususa bungeni, ametumwa kuyawakilisha matatizo ya watu wa jimbo la Kawe.

Watu wenye uwezo mkubwa kiuchumi na wale wenye mamlaka serikalini wanaishi Kawe, chochote anachokifanya mbunge Mdee kinatoa picha mbaya ya ukubwa na umaarufu wa Kawe. Abadilike, aachane na kiburi cha mtaani, akue kimaadili, asipeleke usista du bungeni.
 
Nasikia juzi walimkatia shanga zake Kubenea ametujuza.
Ha ha ha ha, nasikia siku hizi Khanga zinaitwa kubenea. Dada mmoja kwenye daladala kajisahau t-shirt yake ikapanda juu, shanga zikaonekana, mlevi aliyekaa siti ya nyuma akaropoka, oyaaa dada ficha hizo kubenea zako, unatutamanisha, watu hawana mbavu kwa vicheko.
 
Hahaaaaaa mzeee mbavu Mimi sina
 
Mkuu mbona kama sijakuelewa vizuri uliposema "alifanya ziara za kuwashukuru wananchi kwa kumpigia Kura pia kusikiliza kero zao" wakati huo huo ameahidi kutekeleza ahadi zake za kipind cha kampeni.
Je ahadi alizozitoa kipindi cha kampeni ni tofauti na hizi kero alizoenda kusikiliza kipindi akiwa mbunge tayari..?
 
Halima Mdee ni mmoja wa wale wanaosusa na kutoka nje, waliompigia kura hawakumtuma kususa na kutoka nje ya ukumbi wa Bunge. Kapigiwa kura na watu wa kila aina, kuna wavuvi, maprofesa, wanasheria, madaktari na makundi mengine. Anapoanza kuropoka hovyo kabla hajaruhusiwa kwa mujibu wa sheria, anawadharaulisha wapiga kura wake ambao ni wengi sana. Anapotoka nje ya ukumbi wakati bunge linaendelea, anawadharaulisha wapiga kura wake. Hakutumwa kwenda kususa bungeni, ametumwa kuyawakilisha matatizo ya watu wa jimbo la Kawe.

Watu wenye uwezo mkubwa kiuchumi na wale wenye mamlaka serikalini wanaishi Kawe, chochote anachokifanya mbunge Mdee kinatoa picha mbaya ya ukubwa na umaarufu wa Kawe. Abadilike, aachane na kiburi cha mtaani, akue kimaadili, asipeleke usista du bungeni.
Wanaobaki ndani ya bunge hua wanafanya Kazi yenye Tija gani??? 1UKAWA =50 sisiem.
 
Angalau kubaki kwao ndani ya ukumbi kunaonyesha ni jinsi gani wanavyo waheshimu waliowapigia kura. Kumbuka kuwa mbunge mmoja analipwa mshahara ambao ni kodi yako wewe na mimi, jasho lako na langu. Kama jasho lako hulionei huruma, mimi la kwangu sitaki liendelee kuchezewa. Iwekwe sheria, mbunge anayesusa na kutoka nje, asipewe posho ya siku atakayofanya mgomo. Kwa ufupi posho itolewe jioni na ipatikane baada ya mbunge kuthibitisha ushiriki wake bungeni. Huko nje tunaoneka mapimbi fulani ambao hawana hata uwezo wa kujiendesha. Sikatai kuwa hata mabunge mengine kunakuwepo na kutokuridhishwa na maamuzi ya kisiasa, lakini sisi hapa Tanzania imekuwa too much. Tunaonekana wapuuzi, watu ambao hawawezi kufanya maamuzi ya busara.
 
Back
Top Bottom