JIMBO LA ALASKA (USA)

Marekani ilinunua alaska mwaka 1867 toka himaya ya urusi kwa kiasi cha $7.2million.

Sababu kubwa ya kuuzwa kwa alaska ni hofu ya mfalme wa urusi Alexander II.

Alexander wa II alihofia sana uingereza.

Hii hofu ilitokana na urusi kupokea kipigo kwenye vita ya crimea kutoka kwa uingereza na ufaransa bila kusahau ottoman empire.

Unaweza soma kiundani vita ya crimea kwenye hii link.
Crimean War - Wikipedia

Mfalme alioona alaska ni mzigo kiuchumi na watu wachache walikuwa wanaishi.

Hivyo alioona ni ngumu sana kuilinda alaska.

Alaska imepaka na canada koloni la uingereza wakati huo, sasa rusia akaona kuna uwezekano akaipoteza ardhi kwenda kwa uingereza pasipo kunufaika chochote.

Wakati huo urusi ilikuwa na uhitaji wa pesa na marekani na uingereza zilikuwa na uhasama.

Sasa urusi dhaifu iliona njia nzuri ni kuiudha hiyo ardhi.

Walijaribu kuzishawishi uingereza na marekani, uingereza alikataa kwa madai canada ilimtosha.

Urusi ikaona hii ni fursa ya kujilinda kwa kuiuzia marekani na hivyo marekani itakuwa imeuzunguka dola la uingereza(british columbia).

Hivyo makubaliano yakaanza kufanyika kati ya urusi na waziri wa mambo ya nje ya us wakati huo william steward.

Na hivyo ndivyo us ikaimiliki alaska, soma kiundani zaid hapa.
Alaska Purchase - Wikipedia
Leo hii gdp ya alaska $47 billion na pato la mtu mmoja mmoja ni $44,177.

Alaska ilikuja kugundulika kuna mafuta na uchumi wa alaska kwa kiasi kikubwa inategemea hii sekta.

Ukiangalia utaona pesa waliyotumia usa kununua alaska imerudi zaidi ya mara mia moja kama sio elfu moja.
 
Binafsi pia nachefukwa sana. Mtu kwenye L anaweka R. Na kwenye R anaweka L.
Mwenye nia ya dhati ya kusaidia anasaidia kwanza kisha ndiyo anarekebisha mazingira pale anapopaona hapako sawa.
 
Malekani ni wapi?
Watu wenye akili zilizo sawa watataka kujua kwanza Malekani ni wapi ili wampe ufafanuzi wa maswali yake.

Sent using Jamii Forums mobile app

Kwani Alaska iko wapi, tatizo watu ni kukejeli ili wajione wako juu kumbe ni ujinga tu, tatizo la watu walio na depression ni kutafta kosa kwa kila anaemuona

Anyways apo zamani kabla mipaka haijatengenezwa, ilikuwa eneo unaloliwahi ndo lako, ata uku Dar au popote pale nchini ndo ilivyokuwa hvyo, eneo unaloliwahi ndo lako kimsingi uwe na ubabe na wote wakae wakijua ilo ni eneo lako,

Apo kabla lilikuwa linamilikiwa na Urusi, ila baada ya Urusi kuona lina mpa gharama kuliendesha, hivyo akaliuza kwa mmarekani

Nchi nyingi mipaka yao ni ya ajabu, ata lesotho ni nchi japo iko ndani ya South Africa

Pia sehemu kubwa ya jimbo la Alaska kuna baridi kali na sehem kubwa yake ni barafu, kwa hiyo wakazi wa uko ni wachache tu, na nchi ya Marekani kulingana na muundo wake sio lazima kwa Raisi kutembeatembea ata majimbo mengi, otherwise kuna kitu kikubwa official au Raisi atake tu

Ila kikubwa ni haijawa ndani ya Canada maana hawakulinunua


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Ninya ndo nini? Nyumbu wewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ikumbukwe kuwa Russia lilikuwa ndilo taifa la mwanzo katika eneo la Alaska(Non native people) kabla ya ujio wa wageni kutoka Ulaya.

Gharama kubwa ya umiliki na uendeshaji kutokana na umbali ndiyo sababu iliyopelekea kuuza eneo hilo.

Katika mchakato wa uuzaji tangu 1821, kulikuwa na hujuma zilizokuwa zikifanywa ili kuathiri maslahi ya Canada katika Anglo- Amarican Interests hali iliyofanya Canada kuwa na chuki kubwa dhidi ya Uingereza kuliko ile dhidi ya U.S, hivyo kuwa rahisi kwa Marekani kufanikiwa kulinunua eneo hilo.

Kuhusu viongozi wa juu wa Marekani kutembelea Alaska sina taarifa sahihi lakini Rais Obama aliwahi kufika, kitokana na umuhimu wa jimbo hilo, ni wazi kuwa wanafika japo kwa uchache.
Alaska inachangia uchumi kupitia sekta ya Uvuvi, Gesi asilia na Mafuta. Pia uwepo wa vituo muhimu vya kujihami U.S Armed Forces bases na Utalii.

Mwingine aongezee nyama kidogo


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wa-Tanzania wengi mna matatizo sana ya kujifanya kujua hujui....
JAH Rastafari Morning Africa.Trust JAH respect nature
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…