Jikoni na Beelove

Jikoni na Beelove

Beelove

Member
Joined
Aug 29, 2016
Posts
12
Reaction score
16
Kwa wale wapenzi wa kupika ntakua nashare baadhi ya mapishi tofauti tofauti:
mapishi haya unaweza ongeza au kupunguza vitu kutokana na upendeleo wako (hivyo sifungamani na mtu yyt yule).
1. UPISHI WA TAMBI ZA MAYAI
MAHITAJI:
download.jpeg

Tambi nusu pacti, vitunguu maji 2 vikubwa, hoho 1, karoti 1, vitunguu swaumu (kata vipande vidogo dogo), kijiko 1 cha chai, carry powder kijiko 1 cha chai ( sio lazima, ila mm napendelea), njegere zilizochemshwa nusu kikombe ( sio lazima), mafuta kwa kiasi upendacho, mayai 2 makubwa yakiwa madogo 3, chumvi kwa radha upendayo.

JINSI YA KUPIKA:
1. Bandika sufuria jikoni, weka maji kiasi, chumvi na mafuta kidogo, tia tambi acha zichemke mpaka ziive kisha chuja maji yote kwenye tambi kupata tambi kavu
2. katika bakuri pasua mayai yako na uyachanganye vizuri, chukua kikaaango (flampain au sufuria) weka mafuta kiasi,vitunguu maji, swaumu, hoho, karoti, carry powder kaanga kwa pamoja katika moto mdogo kwa dk moja hakikisha haviivi kabisa,
3. ongeza tambi na njegere katika kikaango, geuza geuza ili kuchanganya vizuri. tia mayai katika mchanganyiko wako wa tambi na geuza vizuri mayai yaive pande zote, hakikisha moto ssio mkali ili usiunguze na hakikisha ute wote wa yai umekauka (kama upikapo chipsi yai) hakikisha tambi zako hazikatiki katiki waka kuata kwenye flampain. baada ya dk 5 tambi zako zitakua zimeiva.

epua na serve kwaajili ya kula:
Tambi hizi zinaweza shushiwa na fresh juice au soda
#cheers
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom