Ndugu yangu
Maganga Mkweli at times tunabidi tuweke siasa na vyama vyetu pembeni tuwe rational and realistic
Nimeongea na ndugu yangu ambae ni staff wa Red Cross Society na ni dhahiri kuwa hali haikuwa njema na ilihitajika kutumia busara zaidi
Kwanza watu walikuwa wakiendelea kuongezeka eneo la mkutano lakini watu walishaanza kuzimia na kufikia hatua hata wao wanazidiwa kuwahudumia
Hivyo ikalazimu washauriane kutoendelea na mkutano maana idadi ya watu inazidi kuongezeka na wanaozidi kuzimia pia wanaongezeka
Na hofu ikawa kama wangeendelea mpaka giza likaanza (ukumbuke Tanga huongoza kwa jua kuzama na giza kutanda mapema sana) hivyo wangezidi hali ingekuwa mbaya thereafter
Ndiyo wakakubaliana asimame tu ashukuru, aombe kura lakini wafunge mkutano wasiendelee
Shabikianeni mambo yenu na mavyama yenu lakini inapofika mahali pa usalama wa Watanzania hili ni muhimu zaidi
#KunaMaishaBaadaYaUchaguzi