Jiji la Mwanza lajivua vurugu za wamachinga

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,302
2,000
[h=2] Jumamosi, Novemba 17, 2012 Na John Maduhu, Mwanza [/h]
HALMASHAURI ya Jiji la Mwanza, imetoa pole kwa wakazi wa jiji hilo kutokana na vurugu zilizotokea juzi kati ya mgambo wa jiji na wamachinga zilizosababisha kifo cha mtu mmoja na wengine watatu kujeruhiwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Meya wa Jiji la Mwanza, Stanslaus Mabula, alisema halmashauri hiyo imesikitishwa na vurugu hizo.

Alisema kwamba, juzi hakukuwa na operesheni maalumu iliyoandaliwa na Jiji la Mwanza kwa ajili ya kuwaondoa wamachinga bali mgambo wa jiji walikuwa katika shughuli zao za kila siku za kuhakikisha wamachinga hawafanyii biashara katika maeneo yasiyoruhusiwa.

“Napenda kuwapa pole wananchi waliopoteza ndugu yao kwa kupigwa risasi katika vurugu hizo na pia ninawaomba wamachinga wazingatie makubaliano baina yao na jiji.

“Vurugu kama hizo, hazitakiwi kujirudia tena na zisihusishwe na masuala ya siasa kwani ni tukio ambalo limetokea kwa bahati mbaya na pia halmashauri imejipanga kuhakikisha tatizo hilo halitokei tena.

“Nayasema haya kwa sababu kuna wenzetu ambao tayari wameshaanza kulifanya suala hili kuwa la kisiasa, wanasiasa wasipende kudandia hoja kwa lengo la kusaka umaarufu kwani suala hili hivi sasa liko katika vyombo vya dola,”alisema.

Wakati huo huo, Shirika la Umoja wa Wamachinga jijini Mwanza (SHIUMA), limelitaka Jeshi la Polisi mkoani Mwanza pamoja na Halmashauri ya Jiji la Mwanza, kuwachukulia hatua mgambo wa jiji na viongozi wao ambao wamekuwa wakiwakamata wamachinga kwa masilahi yao binafsi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa jana, Katibu wa SHIUMA, Venatus Anatory, alisema baadhi ya mgambo na wasimamizi wao, wamekuwa kero kwa wamachinga kwa kuwa wakiwakamata wanawatoza fedha nyingi.

“Tunao ushahidi wa wazi wa namna mgambo na viongozi wao wanavyochukua fedha kwa wamachinga, tunaomba wachukuliwe hatua. Pia tunatoa pole kwa wamachinga wenzetu kutokana na tukio la jana (juzi),” alisema Anatory.

Kuhusu hali za wamachinga wenzao waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa Bugando, alisema hali zao zinaendelea vizuri. Aliwataja waliolazwa kuwa ni Chacha Ryoba pamoja na Hussein Martin
 

Mwanaweja

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
3,576
1,195
ulitegemea jipya hapo maana wote policcm na dolawalisha lishwa kiapo cha kubadili ukweli kuwa uongo na uongo kuwa ukweli na ndio seara yao ndani ya ccm. huyo mama kama ulimsikiliza jana alivyokuwa anaongea unajua alipewa kazi kwa njia ya chupi wala si kutoka na taaluma aliyoitafuta yeye kama yeye.
 

Kokolo

JF-Expert Member
Mar 20, 2008
863
1,000
jumamosi, novemba 17, 2012 na john maduhu, mwanza


halmashauri ya jiji la mwanza, imetoa pole kwa wakazi wa jiji hilo kutokana na vurugu zilizotokea juzi kati ya mgambo wa jiji na wamachinga zilizosababisha kifo cha mtu mmoja na wengine watatu kujeruhiwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, meya wa jiji la mwanza, stanslaus mabula, alisema halmashauri hiyo imesikitishwa na vurugu hizo.

Alisema kwamba, juzi hakukuwa na operesheni maalumu iliyoandaliwa na jiji la mwanza kwa ajili ya kuwaondoa wamachinga bali mgambo wa jiji walikuwa katika shughuli zao za kila siku za kuhakikisha wamachinga hawafanyii biashara katika maeneo yasiyoruhusiwa.

“napenda kuwapa pole wananchi waliopoteza ndugu yao kwa kupigwa risasi katika vurugu hizo na pia ninawaomba wamachinga wazingatie makubaliano baina yao na jiji.

“vurugu kama hizo, hazitakiwi kujirudia tena na zisihusishwe na masuala ya siasa kwani ni tukio ambalo limetokea kwa bahati mbaya na pia halmashauri imejipanga kuhakikisha tatizo hilo halitokei tena.

“nayasema haya kwa sababu kuna wenzetu ambao tayari wameshaanza kulifanya suala hili kuwa la kisiasa, wanasiasa wasipende kudandia hoja kwa lengo la kusaka umaarufu kwani suala hili hivi sasa liko katika vyombo vya dola,”alisema.

Wakati huo huo, shirika la umoja wa wamachinga jijini mwanza (shiuma), limelitaka jeshi la polisi mkoani mwanza pamoja na halmashauri ya jiji la mwanza, kuwachukulia hatua mgambo wa jiji na viongozi wao ambao wamekuwa wakiwakamata wamachinga kwa masilahi yao binafsi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa jana, katibu wa shiuma, venatus anatory, alisema baadhi ya mgambo na wasimamizi wao, wamekuwa kero kwa wamachinga kwa kuwa wakiwakamata wanawatoza fedha nyingi.

“tunao ushahidi wa wazi wa namna mgambo na viongozi wao wanavyochukua fedha kwa wamachinga, tunaomba wachukuliwe hatua. Pia tunatoa pole kwa wamachinga wenzetu kutokana na tukio la jana (juzi),” alisema anatory.

Kuhusu hali za wamachinga wenzao waliolazwa katika hospitali ya rufaa bugando, alisema hali zao zinaendelea vizuri. Aliwataja waliolazwa kuwa ni chacha ryoba pamoja na hussein martin
std seven
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom