Jiji la Mwanza hovyo kabisa, uchafu umekithiri sana

Kinkunti El Perdedo

JF-Expert Member
Nov 28, 2020
4,485
11,037
Hivi hili suala la harufu mbaya katka eneo la Mswahili(Mkuyuni) viongozi hamlioni? maana ni kero kubwa kwa wakaazi,wafanyabiashara na wapita njia.

Naunga juhudi suala la hawa wakina mama kujishughulisha ili kujipatia kipato ila sehemu wanayofanyia shughuli sio sehemu sahihi maana ni eneo la shughuli nyingi za watu hivyo kuwa na mazingira salama ni jambo jema sana kwa afya za watu ni vyema watafutiwe eneo lingine la kufanya shughuli zao za kuanika uduvi.

Pia upande wa soko mazingira ni hovyo sana yanatia kinyaa kabisa ila utakuta ushuru unakusamywa yaani pesa kwanza ila kutegeneza mazingira salama ya eneo pesa inakotoka sio jambo muhimu sana

Viongozi msikae maofisini tembeeni muone mazingira yasivyo rafiki kwa wananchi.

IMG_20210215_120421_8.jpeg
IMG_20210215_120102_9.jpeg
IMG_20210215_120049_9.jpeg
 
Sawa mkuu bila shaka wahusika wamekusikia,Sasa labda ungeweza kupendekeza kabisa sehemu inayodhani kuwa itafaa wao kuhamia.
 
Moja kati ya majiji bora ya kuishi na kibiashara ndani ya Tz, Mwanza the best. Hata kwa usafi pia wanajitahidi sana ukilinganisha na mikoa mingine. Labda baadhi ya maeneo machache.
Mkuu pita Nyegezi stedi nyuma, soko la Buhongwa, mswahili na Kamanga.
 
Back
Top Bottom