Mkuu umeongea mengi sana lakini kwa jiji la Mbeya na vitongoji vyake unaweza kuona yafuatayo:
Mbeya ni Mkoa /Jiji tajiri sana hasa kutokana na position yake kijiografia.Jiji la Mbeya ni njia kuu kuelekea Congo,Zambia na Malawi.
- Barabara nyingi hazina lami umiacha zile barabara kuu.Sehemu za Mwanjelwa,kwa Mama Joni, Sai,Mwakibete.Sehemu hizi Jiji limepiga "marufuku" barabara hizi kuwekewa lami.
- Majumba mengi ya jiji la Mbeya ni ya UDONGO! katika karne hii ya 21!!!! Lazima uwepo mkakati maalum wa kuondoa nyumba hizi na kuweka sheria ndogo ya kuweka viwango vya nyumba zitakiwazo katikati ya Jiji.
- Kiwanja cha Sokoine katikati ya Jiji la Mbeya ni aibu ya mwaka.Uwanja huu ni gofu lisilotazamika
- Hakuna mkakati wowote wa kuendeleza CBD(Centra Business District) kwa kubomoa nyumba za udongo sehemu zinazozunguka soko la Matola.Sehemu ambazo ziko katikati ya Jiji
- Kutokamilika kwa kiwanja cha ndege cha kimataifa, Songwe inapunguza sana hadhi ya Mbeya kuwa Jiji.
Ni miji michache nchini yenye oppurtunity kama hii.
Viongozi wa Jiji la Mbeya lazima wawe na vision ya kuona mbali

Kuna Hospitali maarufu sana ya akina mama pale Uyole inaitwa Uyole Hospital au Hospitali ya Sijabaje. Wakti wa mvua wagonjwa ili wafike huvushwa kwa baiskeli au kwa migongo ya watu. Jiji wamshindwa kuweka Karvati kwa muda mrefu: hii hospitali ni tegemeo la wote Nyanda za juu Kusini na hata wengine wanatoka nje ya hiyo Kanda.