Jiji la Kigali-Rwanda mwaka 2040...!!!!

Kwa utajiri tulio nao, Tanzania tulitakiwa tuwe na maendeleo zaidi ya haya hapa...

Check barabara (ziko tano, zote zinaelekea direction moja, hakuna foleni...



Njia za reli za umeme (huu ndio mpango mzima)..

 

Mkuu yote haya yanawezekana tatizo ni moja tu, nalo ni...... CCM

Bila kuachana na utawala wa haya MaCCM kamwe hutakuja kukuta nchi inaendelea. Viongozi wa CCM wanaona Kinyesi kutiririka mtaani ni jambo la kawaida kwa kuwa kwa miaka 52 ya utawala wao wanaishi hivyo. Wanaona barabara za vumbi na matope ni sehem ya maisha ya kila siku. Ondoa CCM kwa maendeleo ya taifa.
 
Wadau hebu angalieni, ...
Hivi wa-Tanzania hatukaki kuwa na miundombinu kama hii mpaka vijijini..???
South Africa wameweza..sisi ni zaidi..!!







 

Yeah, umenena vyema sana...
Ila je unajua kuwa Tanzania ilitakiwa kuwa na maendeleo kuliko South Africa ??
Tanzania ina utajiri mkubwa sana wa ardhi, water bodies (lakes, rivers, etc), tourist attractions, madini, mafuta, gesi, n.k.
Sasa vipi ?? Mbona choka mbaya hapa TZ ?? Yaani hata Kenya wanatushinda wakati hawana chochote ..!!!

Hapo ndio kwenye Lengo !!!!
Angalia barabara na reli za South Africa ambazo sisi tulitakiwa tuwe na zaidi ya hizo...!!!
Umeziona reli za treni za umeme pale chini ya barabara ???

 
Naomba kuuliza kuhusu picha za plan ya hiyo miji...

Hiyo miji ikijengwa itakuwa hivyo hivyo kama kwenye picha?,nazungumzia majengo na plan ya bustani,kama ndio...Hayo majengo yote yatakuwa ni ya Serikali au ya watu binafsi?

Nauliza hivyo kwasababu kama yatakuwa ya watu binafsi hao watu wakati wanauziwa viwanja wanaambiwa na aina ya jengo linavyotakiwa?!

Kama yeye alikuwa na plan yake nyingine,asipojenga kama ilo itakuwaje?
 

Hayo majengo yatajengwa kama yanavyoonekana.
Wenzetu wana 'master plan' za ukweli. Hivyo kila kitu kinapangwa na majengo kuchorwa kabisa (iwe ya serikali au watu binafsi).
Kama uko Dar, unaweza kukumbuka jinsi Mlimani city ilivyokuwa inaonekana kwenye plan, na jinsi ilivyokuja kujengwa.
Jamaa walijitahidi kuitoa kama ilivyo, ingawa ni watu binafsi.
 
Sawa kabisa, ukuaji wa quantity, yes Tanzania tunaongoza.
Tatizo ubora..!!
Angalia Nairobi kwa mfano, jamaa wako juu sana kwa ubora wa barabara (na wala hawana utajiri mkubwa kama sisi).

Check hii ndio Nairobi....









kama sasa Nairobi iko hivi, je ikifika 2040 itakuwaje?, Duh!
 
mbona hata hawaifikii kigamboni tu ya mwaka 2035?
 
mbona hata hawaifikii kigamboni tu ya mwaka 2035?

Kweli hawafikii Kigamboni ya mwaka 2035.
Ila kwa wenzetu zile zote ni mali zao, sisi Kigamboni ni ya George Bush...!!!
Halafu mbaya zaidi, Rwanda wanaweza kujijenga kiasi kile bila kuwa na almasi, dhahabu, mafuta, gesi, tanzanite, n.k.
Sasa jiulize, wangekuwa navyo hivyo vyote wangekuwaje..??

Sisi tulitakiwa kuwa mbali sana mwaka 2000, wala sio mwaka 2035...!!!
Gesi tunayo kibao, mafuta, almasi, dhahabu kibao saaana, tanzanite, ardhi kubwa, watu wachache, n.k.
Lakini TZ angalia, choka mbaya, tunashindwa hata na Rwanda...!!!!
 
Mkuu Mu-Israeli, umesema "wenzetu zote mali zao" sijakupata vizuri unamaanisha wenzetu gani?

Unajua kwamba kwa "watani" hapo juu ukipita Namanga, sehemu kubwa ya nchi inamilikiwa na weupe?
South Africa pia ni ya weupe au hujui?

Tusijidharau kupita kiasi, mie nikiwa bongo najua nauli ya daladala kutoka nyumbani Mbezi Makonde hadi Posta, but nikiwa Nrb, siwezi ..maana nauli inabadilika kila wakati kutegemea na maamuzi ya kondo, inaweza kuwa Ksh.30 asubuhi na mchana ikawa 60 au hata 70!

Nimeomba mniwekee picha za Kibera na Mathare hamtaki..aibu tupu!
 
inaonekana Mu-Israeli ni Mnyarwanda, unasema Bongo inashindwa na Rwanda. Sikuelewi kabisa!

Ukichukua utajiri wa Dar, Mwanza na Arusha, ukauweka kwenye mji wa Moshi unafikiri itakuwaje? Lazima Moshi itasumbua Afrika nzima.

Rwanda utajiri[GDP] wa nchi yao ni dola bilioni 6 tu, kulingana na takwimu za 2011. Tanzania GDP, kwa mwaka jana ni dola bilioni 28! Sasa inashindwaje?

Tanzania inashindwa kwa sababu ina watu wengi? Ndiyo.

Lakini Rwanda ni mkoa tu kama Dodoma, Singida au Mwanza. Unapokosoa ni vema ukatoa vigezo ili akili zetu zijifunze kufikiri kuliko kulalamika tu, kama unavyofanya mkuu. Tunaishia kuwalaumu watoto wanaofeli, wakati sisi watu wazima hatutaki kufikiri..ajabu sana!
 
Unajua utajiri wa Rwanda unatoka wapi au unasema tu?

Mi nafikiri ni muhimu kusoma kwanza kabla ya kuanzisha thread!
:shock:
 
Kule Bungeni wako BUSY tu, Utasikia VISION 2025
 
Ni heri kuwa na mawazo ya maendeleo kuliko kuwa masikini wa mawazo na mali.
 

Hiyo riport ni ukuaji wa miji, yaani kuongezeka kwa idadi ya watu wala siyo uzuri na ufanisi wa mipango miji. Dar litaendelea kuwa na watu wengi lakini vijumba kama uyoga na mipango miji zero!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…