Napenda kutoa tahadhari kuhusu wizi wa mtandao unaoendelea hapa mjini. Mmiliki wa simu yenye namba. 0658-051817 kwa jina la CHRISOSTOM MWABULANGA simu yake inatumika kwa kazi hiyo na ipo hewani. Kinachafanyika ni kwamba anao uwezo wa kutumia namba ya simu yako kuandika sms kwenda mtu mwingine akielekeza hela kutumwa kwake bila ya wewe kujua. Mfano ni sms hii. 'Samahani nipo kwenye kikao.Naomba unisaidie kumtumia hela mwenye namba hii 0658051817 Mr mwabulanga Tsh 300,000 nitakupatia nikitoka! nimebanwa sana! Nadhani elimu hii ipo juu anaweza kupata msaada kwa wataalam wa kampuni ya TIGO. Naomba TIGO wafuatilie akaunti ya tigo-pesa na watu wa usalama kwani huenda watu wengi wameibiwa pesa kwa utapeli huu. Pia uingiliaji wa mtandao wa watu wengine ni kosa la jinai.