Jihadhari na wizi huu mpya

Jihadhari na wizi huu mpya

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2014
Posts
24,498
Reaction score
28,724
Njia mpya ya utapeli yaibuka wakishirikisha Jeshi la Polisi bila
kujitambua kuwa wanafanikisha dili za hawa matapeli.

Mfano: Matapeli wanaweza kukuuzia simu ya wizi ya bei kubwa ya kiasi cha shilingi laki nane ( 800,000/=) kwa fedha ndogo ya elfu sabini ( 70,000/=) ili kukuingiza kingi ukiingia tu imekula kwako.

Kwani simu hiyo unayouziwa ni ya mmoja wao (matapeli) na wanakuwa wamekopi IMEI number ya simu hiyo sehemu.

Baada ya wiki wanakupigia ili kuangalia kama uko hewani, huku wameshatoa ripoti polisi kuwa begi limeibiwa kwenye gari pamoja na vitu vingine na hiyo simu ikiwa ni mojawapo kati ya vitu vilivyoibiwa.

Na watatoa maelezo polisi thamani ya vitu vilivyoibiwa ni Tshs zaidi ya Milioni 7 (katika maelezo yake atakuwa ametaja laptop, fedha taslim na simu tatu au nne)

Wanapewa mpelelezi na hapo ndipo Jeshi letu linajikuta limeingizwa kingi bila ya kujijua.

Mpelelezi anaomba msaada cyber crime kuitafuta simu hiyo.

Ikipatikana biashara inaanza. Unawekwa chini ya ulinzi kulipa vitu vyote ambavyo hujawahi hata kuviona na kesi ya wizi unayo.

Nalishauri Jeshi la Polisi kuwa makini sana na hizi kesi za cyber. Labda mtakuja gundua kuwa simu hizi zinazotumika kutapelia watu zimekwisha ripotiwa mara mbili au tatu ndani ya miezi mitatu.

Ndugu zangu msikubali kuuziwa simu mkononi ambayo ni used, na kama utanunua simu hiyo ambayo ni used basi mlipe kwa cheque, kagueni IMEI number na umpige picha huyo aliyekuuzia pindi unapomkabidhi kiasi hicho cha Malipo.

Ikiwa hataki achana nae ndiyo salama yako.

Matapeli ni wengi sasa na wanabuni mbinu siku hadi siku ili kuyasukuma maisha yao.

Tunaitajika kuwa makini
 
Njia mpya ya utapeli yaibuka wakishirikisha Jeshi la Polisi bila
kujitambua kuwa wanafanikisha dili za hawa matapeli.

mfano: Matapeli wanaweza kukuuzia sim ya wizi ya bei kubwa ya kiasi cha shilingi laki nane ( 800,000/=) kwa fedha ndogo ya elfu sabini( 70,000/=) ili kukuingiza kingi ukiingia tu imekula kwako

Kwani simu hiyo unayouziwa ni ya mmoja wao (matapeli) na wanakuwa wamekopi Imei number ya simu hiyo sehemu.

Baada ya wiki wanakupigia ili kuangalia kama uko hewani. Huku wameshatoa ripoti polisi kuwa begi limeibiwa kwenye gari pamoja na vitu vingine na hiyo simu ikiwa ni mojawapo kati ya vitu vilivyoibiwa.

Na watatoa maelezo polisi thamani ya vitu vilivyoibiwa niTshs zaidi ya Milioni 7 (katika maelezo yake atakuwa ametaja laptop, fedha taslim na simu tatu au nne.)

Wanapewa mpelelezi na hapo ndipo Jeshi letu linajikuta limeingizwa kingi bila ya kujijua.

Mpelelezi anaomba msaada cyber crime kuitafuta simu hiyo.

Ikipatikana biashara inaanza . Unawekwa chini ya ulinzi kulipa vitu vyote ambavyo hujawahi hata kuviona na kesi ya wizi unayo.

nalishauri jeshi la polisi kuwa makini sana na hizi kesi za cyber. Labda mtakuja gundua kuwa simu hizi zinazotumika kutapelia watu zimekwisha ripotiwa mara mbili au tatu ndani ya miezi mitatu.

Ndugu zangu msikubali kuuziwa simu mkononi ambayo ni used, na kama utanunua simu hiyo ambayo ni used basi mlipe kwa cheque, kagueni Imei number na umpige picha huyo aliyekuuzia pindi unapomkabidhi kiasi hicho cha Malipo.

Noted mkuu!
 
Hizi simu za kununua Mkononi achana nazo kabisa. Bora ununue hata ya bei rahisi Dukani uonekane wa rahisi kwasababu ndio uwezo wako kuliko kujimwambafy na iphone10 kumbe umeuziwa bei ya Samsung s2. Simu haitakubadilisha bado utabakia level hiyo hiyo tu
 
Shukrani ila kuacha kitu cha laki nane kwa alfu sabini inataka moyo hasa kama uko kwenye maitaji ya simu
nafikiri kama wanakuachia na ukaondoka nayo basi kabla ya kaitumia unabadili hiyo IMEI
 
Imemtokea jamaa yangu juzi kati hapa mwezi wa 8. Tulijua ni trik tu lakin hatukuwa na jinsi maana polisi nao wanafanya yaliyo yao. Jamaa kalala ndani usiku mzima. Wakadai kulikuw na laptop. Simu mbili na laki nne. Tulilipa laki 6 tulijifunza kitu na hatuwezi tena kununua kitu mkononi.

Bad enough alieuza simu hata hajulikani. Alikuja ofisini kupata huduma siku tatu tofauti yanne akaleta mzigo. Dogo akaupenda katoa pesa bila hata kupeana namba. Haikuchukua miez miwili jamaa wakatrack gps kweli na kupiga kwa mtu anaewasiliana mara kwa mara na alienunua simu.mwisho wa siku walikuja hadi ofisini. Walisema neno moja tu. Funga ofisi tunakuhtaji kituoni. Harakati zikaanzia hapo.
 
Njia mpya ya utapeli yaibuka wakishirikisha Jeshi la Polisi bila
kujitambua kuwa wanafanikisha dili za hawa matapeli.

mfano: Matapeli wanaweza kukuuzia sim ya wizi ya bei kubwa ya kiasi cha shilingi laki nane ( 800,000/=) kwa fedha ndogo ya elfu sabini( 70,000/=) ili kukuingiza kingi ukiingia tu imekula kwako

Kwani simu hiyo unayouziwa ni ya mmoja wao (matapeli) na wanakuwa wamekopi Imei number ya simu hiyo sehemu.

Baada ya wiki wanakupigia ili kuangalia kama uko hewani. Huku wameshatoa ripoti polisi kuwa begi limeibiwa kwenye gari pamoja na vitu vingine na hiyo simu ikiwa ni mojawapo kati ya vitu vilivyoibiwa.

Na watatoa maelezo polisi thamani ya vitu vilivyoibiwa niTshs zaidi ya Milioni 7 (katika maelezo yake atakuwa ametaja laptop, fedha taslim na simu tatu au nne.)

Wanapewa mpelelezi na hapo ndipo Jeshi letu linajikuta limeingizwa kingi bila ya kujijua.

Mpelelezi anaomba msaada cyber crime kuitafuta simu hiyo.

Ikipatikana biashara inaanza . Unawekwa chini ya ulinzi kulipa vitu vyote ambavyo hujawahi hata kuviona na kesi ya wizi unayo.

nalishauri jeshi la polisi kuwa makini sana na hizi kesi za cyber. Labda mtakuja gundua kuwa simu hizi zinazotumika kutapelia watu zimekwisha ripotiwa mara mbili au tatu ndani ya miezi mitatu.

Ndugu zangu msikubali kuuziwa simu mkononi ambayo ni used, na kama utanunua simu hiyo ambayo ni used basi mlipe kwa cheque, kagueni Imei number na umpige picha huyo aliyekuuzia pindi unapomkabidhi kiasi hicho cha Malipo.

Ikiwa hataki achana nae ndiyo salama yako.

Matapeli ni wengi sasa na wanabuni mbinu siku hadi siku ili kuyasukuma maisha yao.

Tunaitajika kuwa makini
Usinunue simu kwa mtu usiyemjua. Au simu ambayo imetumika.
 
Ni kosa kununua simu kwa mtu???

Mbona magari mnanunua na hakuna mtu anayewaona washamba.
Acheni kuonesha uzuzu... Kasome Sheria za TCRA kwanza ndio uje jf kushangaa vitu vingine vipowazi ila naomba niache kukulamu pengine tunapishana uwezo kifikra na ufuatiliaji na utii wa Sheria... Ila Kama wewe ni mtumiaji wa Simu zilizo chini ya mamlaka ya Nchi ya Tanzania.. Ni Kosa kununua Simu kwa Mtu usiyemjua.. hata kumpa simu yako atumie kwa matumizi yake binafsi kikiwa kibaya atakayehukumiwa ni wewe... hii ipo wazi tahadhari kwa raia wote.. so kuingizwa mkenge na mtu mwingine ni kwamba kakufanya mpumbavu.
 
Ni kosa kununua simu kwa mtu???

Mbona magari mnanunua na hakuna mtu anayewaona washamba.
Ndugu jifunze Kunata na beat.
Ukinunua gari used unapewa card. Jee huyo wa simu amekupa risiti na imei yake?(vile vikaratasi vinavyokuwa ndani ya box)
 
Hizi simu za kununua Mkononi achana nazo kabisa. Bora ununue hata ya bei rahisi Dukani uonekane wa rahisi kwasababu ndio uwezo wako kuliko kujimwambafy na iphone10 kumbe umeuziwa bei ya Samsung s2. Simu haitakubadilisha bado utabakia level hiyo hiyo tu

Bora umwambie........mambo ya kununua smartphones mkononi mbona yalishapitwa na wakati......?.......
 
Back
Top Bottom