Jihadhari na wezi wanaojiita AFRICELL

Jihadhari na wezi wanaojiita AFRICELL

Lujula S

New Member
Joined
Mar 29, 2021
Posts
1
Reaction score
2
Mtanzania kuwa makini na Hawa wezi wanaojiita AFRICELL CAPITAL INVESTIMENT wanasema wanafanya biashara ya kuwekeza hela na unalipwa 100% ya hela uliowekeza ndani ya siku 3, wanasema wamesajiliwa na BRELA, TCRA, na TRA, kumbe hizo nyaraka zao ni feki na pia wanasema makao makuu Ni mwanza.

Kampuni halali ya Africell makao makuu Ni London, na website yao halali Ni www.africell.com, na hii kampuni haifanyi shughuli hio. Kuwa makini mtanzania
 
Kupitia account yangu ya what's up waliniunga kwenye group lao .Nashukuru Mungu Hadi Leo sijawahi kuwekeza licha ya kunitaka nifanye hivyo.
 
Pesa ingekua inapatikana kwa urahisi hivyo basi wengi tungekua millionaires
 
Pesa ingekua inapatikana kwa urahisi hivyo basi wengi tungekua millionaires
 
Nasema hivi acha wapigwe tu kwani inaonekana kila siku watu hawasikii na DPP, alishawaambia kuwa ni marufuku kwa mtu kuja kuiambia serikali kuwa amezulumiwa pesa zake!!na hata hao wahusika wakitaifishiwa pesa zao zinakuwa mali ya serikali.na awamu hii hakuna cha pccb kuingilia huko kama zamani mala, umekubaliana na mtu huko, unashindwa kufuata makubaliano yenu, unakimbilia pccb, kulia??ndio maana rais amewaambia kwani hapo kuna kuwa rushwa???
 
Hao Matapeli ndiyo wale wanaojiita Champion Investment pale Mwanza. Wana nyaraka za kughushi za TRA,BRELA na MANISPAA.

Wanachofanya ni kukuunga kwenye group lao pasipo taarifa, Cha ajabu utashangaa Kuna maadimin kumi na tano.

Sasa kwa kuwa namba zao ninazo.namalizia hatua za mwisho kupata ushauri wa kisheria ili nijiunge nao niwaangushie jumba bovu.
 
Umeonaee yani utashangaa umeungwa kwenye group la WhatsApp bila wewe kujua. Washenzi Sana hawa. Hivi serikali haioni?
 
Nami nimejikuta kwenye group lao la whatsapp aisee.

IMG-20211026-WA0002.jpg

IMG-20211026-WA0003.jpg

IMG-20211026-WA0001.jpg
 
Kifupi usinubali kuwekeza hisa zako kwenye kampuni ambayo haijasajiliwa soko la hisa lakini inakutaka uwekeze hisa kwao utalia kilio Cha mbwa Deci liliwakuta watu wakawekeza huko wakati haijasajiliwa soko la hisa wanalia Hadi leo.Hata wawe na vibali na leseni lakini ukiona hawako soko la hisa achana nao
 
Back
Top Bottom