Jihadhari na aina mpya ya wizi wa simu

masanilo hii kali kuliko nimecheka hadi basi, usiseme rushwa y 2000, sema 1400 tu! lol!
 
kweli inauma unakuta mtu yupo kwenye gari yake peke yake au familia yake si bebi mtu njiani bado watu wanakusema kweli lakini niliwahi kuibiwa mara mbili cm na laptop kwa kuwapa watu lifti na cm nilipakia mtu na mfahamu kashuka naangalia cm aipo nikajua nimshikaji kwani tulikuwa wawili tu kumpigia anasema ajaiona ila yukiwa nae nilipigiwa cm nilipomaliza nikaweka katikati ya kiti changu na chake
 
wapi wananchi wanaende nadhani ni madhara ya ukosefu wa ajira na umasikini
 
Pole sana muzee! Hiyo ndo bongo, mtu anakutoa roho kwa ajili ya 500 na traffic anaweza kupokea hata book. Kila 3 nyama ni karibia 15000/-. Pia inawezekana jamaa alionja nyama siku kuu ya pasaka!

Mbombo ngafu malafyale!!
...Mbombo ikafu fijo nnyambala!..Polisi wetu wanatia aibu nadhani hata njaa yao haina simile. Mi niliwahi kusimamishwa na polisi junction ya Livingstone na Uhuru kisa eti nilitanua wakati naigia na gari mtaa wa uhuru. askari walikuwa wawili na bunduki zao sijui walikuwa kwenye patrol wakataka tuende Central nikakubali tulipofika clock tower wakaniambia nirudi na mtaa wa nkrumah eti tuelewane nikasema poa. wakata niwape 10,000 nikawambia sina ila nina 5,000 tu na ndio akiba yangu siwezi kuwapa yote vinginevyo nitafute chenji tugawane wakakubali ili tupige pasu nikanunua vocha ya zain ya 1,000 nikabaki na 4,000 wao nikawapa 2,000 na mimi nikabaki na 2,000 tukaachana. NIlishangaa sana!!
 
Mtu akiomba lift muulize unaelekea wapi, akikwambia kushoto we mwambie unaelekea kulia. Bora lawama kuliko fedhea, ila mimi lift kwangu NO!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…