Teknolojia ni Yetu sote
JF-Expert Member
- Apr 28, 2020
- 1,221
- 2,425
Jihadhari sana unapotumia Whatsapp wahalifu wa mtandaoni wamekuja na mbinu mpya ya kudukua taarifa za watu kupitia Whatsapp.
Uhalifu huu ulianzia mwaka 2019 wahalifu walikua wanatumia mfumo wa video calling kukutumia kirusi kwenye kifaa chako na kuweza kukuibia taarifa mbalimbali kwenye simu yako.
Sasa Whatsapp wameleta mbinu nyingine ya kuiba taarifa za watu na kusambaza virusi kupitia njia ya voice call chati zilizopo kwenye group, ambapo wanatumia mfumo wa kutengeneza group voice calls.
Wahalifu wanaweza kuingia kwenye group la kikundi chenu kisha akajifanya kama member wa group kisha ataweza kujiunga na groups video call / voice call kisha ataunda link ambayo ukijiunga voice call utaombwa six digit utakazotumiwa kwenye Whatsapp yako sasa kama utajaza hizo taarifa muhalifu ataweza kuingia kwenye akaunti yako na kuifanya atakavyo.
Virusi hivyo vinafanya kazi ikiwa Mtumiaji ataweza kupokea ujumbe wq kujiunga kwenye voice chati ya kikundi halafu akakubali ku join ataweza kuathirika.