JIFUNZE KUWA MUWAZI.

JIFUNZE KUWA MUWAZI.

Bwana Muki

Member
Joined
Dec 13, 2018
Posts
13
Reaction score
9
Masalkheri ndugu,

Wengi wetu hatupendi kukosolewa. Hii hutokana na kuogopa kuonekana mbaya na pengine kuachwa. Tabia hii hutufanya tulazimishe maisha yetu yaenande na ya watu wengine. Lakini tukumbuke, TUKO TOFAUTI. Unaweza kuchukia kitu fulani ila mimi ninakipenda. Na tutafahamiana vipi?? Jibu ni sote kuwa WAWAZI.

Ni vema kuwa muwazi. Hata kama watu wakikuacha, umeokoa MUDA. umeokoa muda wa kughushi maisha ya watu wengine na kukumbatia vitu ambayo havikupendezi. Mfano
Wafanyakazi wenzako wanapenda kwenda club na kupiga likwidi kila wikiendi na wewe hupendi, ni vema kuwa muwazi. Hata wakisepa, uzuri wewe utabaki na maisha yako na roho inapenda.

Mahusiano mengi yanafeli sababu yanakosa uwazi ndani yake. Watu wanachukuana huko kwa jina la mihemko, wanaburuzana na mwisho unakuwa mbaya siku zote. MAPENZI YA DHATI NI UWAZI.

KUWA MUWAZI. UWAZI UNAOKOA MUDA.
 
HII ISSUE INA_APPLY KWA ZAIDI HUKO KWA MKOLONI, HUKU KWETU UKIWA MKWELI NDIYO UNAHARIBU KILA KITU.
 
HII ISSUE INA_APPLY KWA ZAIDI HUKO KWA MKOLONI, HUKU KWETU UKIWA MKWELI NDIYO UNAHARIBU KILA KITU.
Ukweli unajichuja tu mjomba. Titapiga ndarire nyingi lakini tunarudi pale pale.
 
Moja vitu ambavyo wasiojulikana hawataki kuvisikia ni kuwa muwazi, ukiweza jua kuna kupelekwa kusikojulikana, jela kukuhusu au risasi kutumika ni hatari sana kuwa muwazi nchini Tanzania
 
Kuna gharama ya kuwa MUWAZI. Mfano kushindwa kuendana na jamii iliyojaa USIRI.
Hata hivyo kuna gharama kubwa zaidi ya kuwa MSIRI. Mojawapo ni kukosa amani ya nafsi na msaada stahiki.
 
Kuna gharama ya kuwa MUWAZI. Mfano kushindwa kuendana na jamii iliyojaa USIRI.
Hata hivyo kuna gharama kubwa zaidi ya kuwa MSIRI. Mojawapo ni kukosa amani ya nafsi na msaada stahiki.
Bora uwazi sasa [emoji1]
 
Na ukiwa muwazi unaweza kukosa hata mke wa kuoa. Lakini ukidanganya utaoa kila siku. Wenzetu hawataki ukweli. Ukisema mimi masikini, anakuuliza sasa nikusaidieje?! Ukimdanganya siku akiha kuujua ukweli inakuwa too late kwake.
 
Ukiwa mkweli hapa tz utajikuta unatengwa hadi na ukoo wenu ..tz kila mtu muongo ile mbaya
 
Na ukiwa muwazi unaweza kukosa hata mke wa kuoa. Lakini ukidanganya utaoa kila siku. Wenzetu hawataki ukweli. Ukisema mimi masikini, anakuuliza sasa nikusaidieje?! Ukimdanganya siku akiha kuujua ukweli inakuwa too late kwake.
Hata ukidanganya mwisho wa siku mtaachana tu.
 
Back
Top Bottom